Wanawake mnao bet na kushabikia mpira mtatuulia watoto wetu

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Ndugu zangu natumaini mko salama kabisa , basi na kwa wale wenye changamoto Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amina

Michezo ya mipira ya miguu au inayofanana na hiyo ni burudani na kushabikia mpira siyo kosa kwa wanawake hali kadhalika na kubet siyo kosa kwa wanawake kama tuu unafata sheria, kanuni na taratibu na haubughudhi au kuhatarisha usalama wa maisha ya watu wengine

***Wanawake wanao bet na kushabikia mchezo wa mpira wa miguu msipokua makini watatuulia watoto wetu kwa kipigo kikali sana huku tunajionea hivi hivi kwa hasira waliyo nayo baada ya kuchaniwa mikeka waliyo bet au timu wanayoishabikia kufungwa

***Wanawake wanao bet na kushabikia mpira pindi timu zao zinapofungwa au kuliwa hela yake aliyobet anakua na kisirani cha hali ya juu na kushindwa kujizuia pale mtoto anapo kosea, utakuta hasira na uchungu wote ana uhamishia kwa watoto huku akiwatukana na kuwasusa wanae, pamoja na kuwapa watoto kichapo kikali kisicho cha kawaida

*** Wanawake wanao bet wataua watoto wetu kwa kwashakoho, wana bana hela za chakula tunazo waachia ili wakaweke kwenye betting badala ya kununua chakula cha kutosha watoto wale wawe na afya njema

***Wanawake wanao bet na kushabikia mpira wengi wao wanapanic na kushikwa na tatizo la afya ya akili kwa haraka linalopelekea kuwasusa watoto wake kwa muda ili apate tulizo la moyo, hatojua watoto wameenda wapi , hatojishughulisha kwa sababu anatafuta tulizo la akili na moyo wake hivyo kupelekea watoto kupata matatizo ya kimazingira na wakati mwingine hata kudumbukia kwenye ndoo za maji

Ndugu wanaume kama mkeo /mwanamke wako /mzazi mwezako anabet pamoja na kushabikia mpira kuwa makini sana pale timu yake inaposhindwa kufanya vizuri au pale unapogundua mkeka aliobet umechanika, na yote haya ni kuwa makini ili watoto wawe salama
 
Nahitaji mwalimu anifundishe kubet๐Ÿ˜ƒ
Una uwezo wa kuzuia hili ๐Ÿ‘‡

***Wanawake wanao bet na kushabikia mpira wengi wao wanapanic na kushikwa na tatizo la afya ya akili kwa haraka linalopelekea kuwasusa watoto wake kwa muda ili apate tulizo la moyo, hatojua watoto wameenda wapi , hatojishughulisha kwa sababu anatafuta tulizo la akili na moyo wake hivyo kupelekea watoto kupata matatizo ya kimazingira na wakati mwingine hata kudumbukia kwenye ndoo za maji
 
Ninao๐Ÿ“Œ

Mi napenda demu mwenye anafuatilia mpira tu ila sio Ile mpaka anakua amebobea sana apana awe tu anajua labda Yanga anacheza na Mamelody na ajue ni mashindano gn na matokeo bas inatosha ili hata nikimwambia leo na vibe tutoke Yanga wameshinda bas anielewe
 
Back
Top Bottom