Rangi za bendera ni ujumbe, uzalendo au urembo?

Hovyohovyo,

Asante sana.
Hizo taarifa za nimelala kwa nani, nimekula nini zimekujaje hapa? Mengine ya kwenye blogu ni ya kwenye blogu. Wanaonifuatilia kwenye blogu huwa wanajua imetokea wapi. Maana, mengine ya kwenye blogu yakifika hapa ni kuwachanganya wajao hapa. Yabaki huko huko Mjengwablog!
Samahani sana mkuu. Naomba unisamehe bure.
 
Samahani sana mkuu. Naomba unisamehe bure.

Hovyohovyo,

Ya kawaida haya, na mengine ni ya utani. Nahisi wewe ni ama, Msukuma au Mnyamwezi, maana watani zangu hao ndio ' Watu wa Hovyo Hovyo'. Ni Msukuma au Mnyamwezi tu ndiye anayeweza kuyachukua ya kwenye Mjengwablog akayaleta JF, hakyamungu!
 
Hovyohovyo,

Ya kawaida haya, na mengine ni ya utani. Nahisi wewe ni ama, Msukuma au Mnyamwezi, maana watani zangu hao ndio ' Watu wa Hovyo Hovyo'. Ni Msukuma au Mnyamwezi tu ndiye anayeweza kuyachukua ya kwenye Mjengwablog akayaleta JF, hakyamungu

ha ha ha. mi chio nchukuma wala nnyamwezi. Kila la heri bwana.
 
Kuna babu mmoja alikuwa jirani yetu, alifungwa kisa alikutwa na bendera ya taifa.
 
Lakini hairuhusiwi kupeperusha bendera ya taifa kwa mtu yoyote isipokuwa ofisi za serikali na nyumba za viongozi wakuu.

Hilo ndilo jibu na sidhani Maggid alitakiwa kushangaa kwamba watu hawapeperushi bendera ya taifa. Nakumbuka miaka ya nyuma jinsi bendera ya taifa ilivyokuwa inaogopwa sijui nani angethubutu kuwa nayo achilia mbali kuipeperusha? Nadhani ilikuwa miongoni mwa nyara za nchi kama ilivyo ngozi ya chui. Bendera ya CCM ndio ilikuwa ikipeperushwa kwa wajumbe wa mashina na baada ya kukaribia vyama vingi CCM wakazigawa bendera kwenye matawi ya wakereketwa. Huo ndio mwanzo wa bendera za vyama kuanza kupepea kila mahala hata kwenye vijiwe vya bangi.

Baada ya JK kuingia madarakani alikuja na sera ya uzalendo ndio akasema bendera ya Taifa iwe jambo la kujivunia basi hapo ndio tukaanza kuona hata nguo zenge bendera ya Taifa na akina Mwigulu wakaanza kuvaa bendera ya taifa kama skafu shingoni, watu wakaenda na bendera za taifa huko uwanja wa Taifa na vibendera vya taifa vile vya karatasi vikaanza kuuzwa. Lakini sijui kama kuna uhuru wa kupeperusha bendera ya Taifa kwenye shughuli zako ama ofisi yako binafsi au nyumbani kwako!
 
Asante sana kwa kuniruhusu kuiona website hiyo tena. Hata hivyo sikuona bendara ya Taifa kama ulivyotaarifu, ila nadhani kuwa wafanya biashara wale walikuwa wanatumia ndoo zenye rangi za bendera ya taifa; not sure.
 
Asante sana kwa kuniruhusu kuiona website hiyo tena. Hata hivyo sikuona bendara ya Taifa kama ulivyotaarifu, ila nadhani kuwa wafanya biashara wale walikuwa wanatumia ndoo zenye rangi za bendera ya taifa; not sure.

Kichuguu,

Karibu sana!

Kuhusu mfanyabiashara yule, ni kuwa, bendera ya taifa aliipeperusha kwenye paa la banda lake. Niliiona. Safari ijayo nitasimama kabisa na kuongea naye.

Maggid
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Hivi kwani bendera ya taifa inaruhusiwa kupeperushwa hovyohovyo kama za vyama vya siasa na mimi niweke mlingoti nje ya kibanda changu
 
kuna kpindi walipiga marufuku kupeperusha bendera hovyo, kutumia kama vtambaa, mapazia au shuka sababu etu tunadharirisha bendera ya nchi, ina maana wamesharusu saizi bcoz n rahs zaidi kupata bendera ya US kuliko ya tz

Umenikumbusha siku aliyekuwa waziri wa Habari, Bw. George Mkuchika alipopiga marufuku kutumia wimbo wa taifa kwenye miito ya simu. Alisema "sio uzalendo bali ni kudhalilisha wimbo wa taifa!". Safari bado ni ndefu sana sababu huyu jamaa bado ni waziri!
 
Aliyezoea ubinafsi na ubaguzi utamjua tu. Mtu akizoea kula nyama ya mtu ataendelea tu hata umzuieje.
 
Ndugu wana jamvi ni siku nyingi najiuliza hivi kwa nini bendera yetu ya Taifa inapepea kuanzia asubuhi hadi jioni na usiku inashushwa? katika maana na dhumuni la bendera ya Taifa ndivyo inavyotakiwa kuwa? vipi nchi nyingine zinafanya kama sisi na kama ni tofauti, utofauti huo unaletwa na nini? Karibuni.
 
Rudi shule ya msingi ukasome somo la Uraia. Au la tuambie kama ulikacha shule ya msingi tukufundishe
 
Blue,Yellow,Green and Black.Tanzania tunahitaji rangi mpya za bendera,maana ya hizo rangi haipo tena.
 
Kiongozi kwa mawazo yangu naona haina maana yeyote. Ni utaratibu tu wa binadamu, kujipangia taratibu zake na kuzifuata. Kwamfano kuwa na hiyo bendera, wimbo wa taifa, nembo ya taifa n.k.
 
Back
Top Bottom