Rais Ruto: Kama Mwanaume akigombea Urais Mgombea Mwenza awe mwanamke

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
1709814541316.png

Rais Ruto amesisitiza hilo leo Alhamis 7/3/2024 kuwa ataendelea kuhakikisha sheria ya 2/3 ya jinsia imetekelezwa kikamilifu katika chama chake cha United Democratic Alliance (UDA) na katika serikali ya Kenya Kwanza kwa ujumla.

Katika uzinduzi wa Mkakati wa Baraza la Magavana Wanawake G7 jijini Nairobi, Ruto amesema serikali yake imefuata mikakati mikali ili kutimiza kiwango cha ujumuishi wa kijinsia katika Katiba na atakuwa mstari wa mbele katika kuonesha ahadi yake.

Rais Ruto amempa jukumu Mwenyekiti wa chama cha UDA Bi. Cecil Mbarire kutunga sheria mpya ambazo zitamtaka mgombea Urais wa Kiume kuwa na Mgombea mwenza wakike, na kinyume chake ikiwa Mgombea Urais ni mwanaume.

Akaongeza kuwa ni muhimu jambo hili likafanywa kwa makusudi la sivyo halitatokea kamwe, na pia jambo hili lifanywe kuwa la lazima upande wa Magavana na ngazi zote za uongozi ndani ya chama.

Rais Ruto alisema mabadiliko hayo sio sababu ana tatizo na wanaume, bali anataka kuwe na uwiano ili yeyote (wanaume na wanawake) wasiachwe nyuma.

Akaongeza wakati wa alipokuwa kwenye misukosuko ya kama Naibu Rais, wanawake wengi ndio walikuwa nyuma yake kuliko wanaume kwenye timu yake, na wakati wa uchaguzi pia ni ukweli usiopingika kuwa wanawake ndio waliompigia kura kwa idadi kubwa kuliko wanaume.

Aliwataka wanaume pia kuwa wa kwanza kuwalinda wanawake dhidi ya ukeketaji hasa katika mikoa ambayo imekithiri vitendo hivyo.

====

President William Ruto on Thursday asserted that he will remain committed to ensure that the two-thirds gender rule has been fully implemented in his United Democratic Alliance (UDA) party and in the Kenya Kwanza gov't at large.

During the launch of the Women Governors Caucus G7 Strategy in Nairobi, Ruto said that his government has pursued radical strategies to actualize the constitution's gender inclusion threshold and will lead at the front in showcasing his pledge.

He therefore tasked the UDA party chairperson Cecily Mbarire to formulate a new set of laws that will require a male presidential candidate to have a female running mate and vice versa.

"When Riggy G (DP Rigathi Gachagua) and myself agree on how things will go in the future we must also agree that going forward if a man is a candidate for president the woman must be a running mate and if a woman is a candidate then a woman is the candidate then a man should be a running mate," Ruto said amid a cheering crowd.

He added: "We must be deliberate and intentional about it otherwise it will never happen."

Ruto said that the same should also be made mandatory for Governors and all leadership positions within the party.

He expressed confidence that other party leaders will welcome the proposal to fully achieve the 2/3 gender rule.

"We will do this not because we want to do anything against men but we want to balance so that we move together," he said.

The Head of State hailed women for their reliability in actualising their mandates, narrating how he has always received unequivocal support from women since his days as Deputy President.

"When I ran into political turbulence as deputy president, more women stood by me than men in my team. And that is a fact. In the last election, more women voted for me than men," he said.

"Therefore supporting me is the easiest thing for me. Apart from the fact that in my family I have more women family members than men."

He further urged men to be the biggest champions of protecting women against Female Genital Mutilation (FGM) particularly in regions that have proven prevalence in practising the vice.

Citizen TV
 
Baada ya uongo mwingi kuhusu kushidwa kuziletea maendeleo nchi zao, marais wengi wanaume wa Afrika sasa wamekuja na uongo mwingine kuwa maendeleo ya nchi zao na watu wake yatawezekana tu kama wakati wa uchaguzi mgombea Urais akiwa mwanaume basi mgombea mwenza awe mwanamke.

Wengine wanasema Rais mwanamke ndiye atakayewaletea watu wa nchi zao maendeleo. Wamefika hata kusema wanawake wasiwapigie kura wagombea wanaume ili wawe na uhakika wa kumpata Rais mwanamke atakayeleta maendeleo ya watu wa nchi zao.

Kama siku zote na hasa hawa wa Tanganyika ni waongo, waongo, waongoooooooooooooooo. Hoja hii haina ukweli wowote.
 
Mbona habari inaelea elea tu. Toa takwimu ili uweze kujenga hoja zenye ushawishi kuhusu madai yako. Huwezi tu ku "generalize" mambo kisha ukaja na "conclusion"
 
Mbona habari inaelea elea tu. Toa takwimu ili uweze kujenga hoja zenye ushawishi kuhusu madai yako. Huwezi tu ku "generalize" mambo kisha ukaja na "conclusion"
Takwimu ni jambo jema na linasaidia kuonyesha njia. Utekelezaji wa mipango ya maendeleo ni jambo tofauti kabisa. Uongo mwingi sana ndilo donda ndugu linaloitafuna Africa. Wakiacha uongo tutapata nafuu kubwa kuelekea njia ya kuzipatia nchi zetu maendeleo ya kweli.
 
Back
Top Bottom