Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,199
- 10,929
Rais Miguel akiongoza maandamano Havana kuwaunga mkono Hamas.
Katika hali ya mabadiliko ya haraka kufuatia mashambulizi ya Hamas ya Oktoba sana huko Cuba Rais wa nchi hiyo ameongoza maandamano ya maelfu ya raia wake katika kuwaunga mkono Hamas na harakati zao za kutetea haki ya kuishi kwenye ardhi zao.
Rais Miguel Díaz-Canel aliongoza maandamano kupitia barabara kuu ya katikati ya Havana kabla ya kupinda na kupita mbele ya ubalozi wa Marekani huku yeye na wenzakewakiwa wamevaa vilemba vya nembo za Kipalestina.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Spain, Pedro Sanchez hapo juzi Novemba 22 amemtaka Waziri Mkuu mwenzake wa Israel, Netanyahu aweke akili yake sawa na kuachia taifa la Palestina liundwe.
Katika maelezo yake kwa Netanyahu alimpa mifano ya uzito wa kumaliza vikundi kama Hamas kwa njia ya vita. Akitolea mfano nchi ya Spain ilivyoshindwa kumaliza vita na vikundi vidogo kama vile Eta na Basque mpaka pale walipoamua kufanya makubaliano nao.
Maelezo hayo ya Sanchez yanaungwa mkono na ukweli kwamba mpaka kufikia kusitishwa kwa vita leo kwa siku nne Israel haikuweza kufikia lolote kati ya malengo yake ya kivita kiasi kwamba inasubiri kupatiwa mateka waliokuwa wanawatafuta lakini baada ya makubaliano na Hamas.
Netanyahu katika mazungumzo hayo na mgeni wake alimfungulia video ya mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7 akisema ni matukio mabaya sana. Hata hivyo Sanchez hakuonekana kushtushwa na video hiyo na akamwambia Netanyahu pamoja na haki ya Israel kujilinda lakini haina haki ya kuuwa watoto na akinamama namna ile iilvyo fanya kwa wapalestina wa Gaza na ukingo wa magharibi.