Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania: Wagonjwa wa COVID19 wamepungua SANA nchini

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
473
1,000
Hayo yamesemwa na Dr. Elisha Osati, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) leo Mei 27, 2020

FULL TEXT:

Leo tumekuja kuzungumza nanyi Waandishi wa Habari kuhusu tathmini ya Corona hapa nchini. Ikumbukwe tangu Corona imeingia hapa nchini Mwezi wa tatu kumekuwa na mambo mengi yakiwa yanaendelea.

Hata sisi kwa upande wetu kumekuwa na matamko lakini pia na mikutano mbalimbali kwa ajili ya kueleza wananchi na Serikali na wadau wengine na wanataaluma kiujumla.

Sisi kama Chama cha Madaktari, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha taaluma ya udaktari inatolewa kwa weledi na kufuata taaluma, kwa kushirikiana na serikali especially Wizara ya Afya kwa ajili ya kuhakikisha tunatimiza hayo.

Tukizungumzia mwenendo wa corona, tumefanya tathmini ya ugonjwa huu kwa kushirikiana na madaktari pamoja na watafiti mbalimbali kutoka hapa kwetu.


Tumebaini mambo yafuatayo juu ya mwenendo wa ugonjwa Corona:
Ugonjwa umepungua kwa kiasi kikubwa nchi kwa kuangalia vituo mbalimbali, haswa kwa vile vituo ambavyo wagonjwa walikuwa wanaweka wamepungua sana. Wale wagonjwa waliokuwa wanahitaji hewa ya Oksijeni wamepungua sana.

Mwezi wa nne tulikuwa tunapokea wagonjwa wengi na majibu ya watu wengi tuliokuwa tukiwapima zaidi ya asilimia 90 zilikuwa zinakuja na matokeo chanya kwamba wana Corona. Lakini kwa sasa hivi, yaani kwa wiki iliyopita, idadi ya sampuli zinazopelekwa na kurudi chanya ni chini ya 10% tu ya majibu ya vipimo vyote.

Lakini pia kwa ngazi ya jamii, tumeona kwa ngazi ya jamii ugonjwa umepungua kwa kiasi kikubwa sana. Nafikiri mnakumbuka kuwa tulikuwa na namba za simu kwa ajili ya kuomba msaada au kutoa taarifa, kiasi cha wanaopiga simu kimepungua sana, pia waliokuwa wanatutafuta kwa matatizo ya kukosa ladha ya chakula au harufu pia imepungua sana.

Pia idadi ya vifo imepungua sana! Kwa hiyo tukiangalia yote haya kama wataalamu, ule mzigo tuliokuwa nao kwa mwezi wa nne na wiki ya kwanza kwa mwezi wa tano hali ilikuwa ngumu sana lakini kwa sasa hali imekuwa nzuri.

Pongezi kwa Rais Magufuli na watendaji wengine
Sisi kama Madaktari tuchukue fursa hii kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa namna aliyoshughulikia tatizo kitaifa. Jambo kubwa sana aliweza kuondoa hofu kwa watu hapa nchini na kuweza kuondoa hofu kumetupa fursa ya kujifunza kuhusu ugonjwa na imetupa confidence ya kuendelea kuwahudumia wagonjwa.

Kwa hiyo tunamshukuru mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa muelekeo wa hili janga.

Lakini pia tumshukuru Waziri Mkuu ambaye alikuwa ni kiongozi wa kamati ya kitaifa ya Corona, pia na Waziri Ummy Mwalimu na Kamati zote za Wizara, wamefanya kazi nzuri na tumeshirikiana nao vizuri sana.

Pia tuwapongeze Madaktari na watumishi wote wa Sekta ya Afya. Nafkiri mnakumbuka Madaktari ktk kipindi ambacho tumekutana na wakati mgumu ni muda huu kwa kuwa ugonjwa ni mpya na hofu ilikuwa nyingi sana na baadhi ya madktari na watumishi wengine walipata ugonjwa lakini tunashukuru wote wamepona.

Wengine wamerudi kazini tunaendelea kufanya nao kazi wengine wako nyumbani wanazidi kujiuguza lakini wanaendelea vizuri lakini tunawashukuru sana. Yaani hatuna namna ya kuwashukuru madaktari na watumishi wote kwa namna ambayo tumelishughulikia hili jambo mpaka limeisha.

Tumekuwa tukitoa ushauri kwa Serikali na wadau na hata kwetu wenyewe na viongozi wa hospitali za binafsi na serikali.

Pia tuwashukuru wadau mbalimbali kwa namna tulivyoshirikiana kuleta vifaa mbalimbali nk tunawaomba tuendelee kushirikiana.


Ugonjwa bado upo, tujifunze kuishi na Corona
Lakini tutoe wito kwa serikali, wananchi wanataaluma na wadau, kwa kuwa ugonjwa unapungua, haimaanishi kuwa ugonjwa haupo, mheshimiwa Rais juzi alihutubia alisema hivyo pia. Kwa hiyo hii isutufanye tukabweteka kuona ugonjwa umeisha.

Ni kweli tunataka kurudi katika maisha kama kawaida lakini tujifunze kuishi na Corona, hivyo tusiache kufuata zile njia za kujikinga na maambukizi kama kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia sanitizer, pia kukaa miguu mitatu kutoka mtu hadi mwingine na kuvaa barakoa, especially mtu anapotoka nyumbani kwenda kwenye msongamano au kuja hospitalini.


Wito kwa wanafunzi wanaorudi shuleni
Kwa kipindi hiki ambacho wanafunzi wanarudi shuleni ni muhimu sana kufuata hatua hizo ili tusije fanya maambukizi yakawa makubwa.

Wagonjwa waombwa waendelee kwenda hospitalini kutibiwa
Jambo la pili ni kwamba tunaona wagonjwa katika hospitali zetu bado watu hawajaanza kuja hospitali vizuri. Tungependa kuwahakikishia kuwa ugonjwa umepungua kwa hiyo watu wasikae nyumbani waje hospitali waweze kuhudumiwa kwa kuwa sisi madaktari tupo tayari kuwahudumia.

Kuhusu vifaa tiba
Kuhusu upatikanaji wa vifaa kinga na vifaa tiba ni muhimu sio tu katika wakati huu wa Corona, sio tu katika kipindi cha corona, sisi tunahitaji vifaa kinga na vifaa tiba wakati wote tunaotoa huduma kwa hiyo juhudi ziendelee za Serikali na Wadau kwa ajili ya kutoa vifaa hivyo.

Lakini tuwashukuru sana wadau kwa namna walivyojitokeza kusaidia na tunachowaomba ni kwamba kwa kuwa mheshimiwa Rais John Magufuli ameshatoa agizo kuwa vifaa vinavyotolewa kwa ajili ya Corona vielekezwe Wizara ya Afya, nafikiri hii ni straight forward. Kwa hiyo vitafanyiwa process ya kupima ubora wake na Wizara itaamua kufanya distribution.


Ugonjwa haukuwa mkali kama ilivyokuwa projected
Tunashukuru pia wagonjwa wote wengi hawakupata ugonjwa mkali kama uilivyofanyiwa projection, tunashukuru hatuja fikia huko. Wagonjwa wetu wengi (hapa Tanzania) hawakuwa na homa kali sana na wale waliokuwa na ugonjwa mkali tunashukuru wamepona.

Kuhusu takwimu za ugonjwa
Sisi hatuna takwimukama general kwa sababu watu ambao wako responsible wapo, mheshimiwa Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Msemaji wa Serikali na Rais wanaweza kusema kuhusu takwimu.

Sisi tumefanya analysis ya kitaalamu kuangalia vituo vyetu vya afya vya kutolea huduma, tumeangalia wale wagonjwa wanaokuja na kuangalia jamii.

Lakini nimeeleza mwezi wa nne mwishoni na watano mwanzoni kuwa sampuli tulizokuwa tunapeleka asilimia 90 yalikuwa yanakuja majibu positive, lakini kwa sasa chini ya aslimia kumi wanakuja kama wana ugonjwa.

Lakini nafikiri takwimu sahihi zitatolewa na Wizara, takwimu zipo lakini kuzitoa ni jambo jingine.
 

Hata Sina kinyongo

Senior Member
May 16, 2020
118
500
Chama cha madaktari Nchini Tanzania kimedai kuwa maambukizi na wagonjwa wa Covid 19 yamepungua/wapungua sana hapa Nchini.

Akiongea na Idhaa ya kiswahili ya Ujerumani rais wa Chama hicho ametabanaisha kuwa visa vya wagonjwa wa Covid 19 vimepungua na hali hiyo inawapa faraja.

"Ikumbukwe hapa kwetu kwa takribani wiki tatu zilizopita wananchi waliitikia zoezi la uvaaji barakoa na pia muda wote walifuata maelekezo ya usafi wa mikono" amesema Raisi.


Mungu ibariki Tanzania na Timu ya Yanga.
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
14,109
2,000
Huu ni ujinga wa hali ya juu sana. Yaani wataalamu wa afya wanaomgelea hili siku tano baada ya wanasiasa kusema maambukizi yamepungua. Nilitegemea wataalamu watuambie kwanza kabla ya wanasiasa hawa wa hovyo...

Ni shinikizo tu la serikali linawasumbua wataalamu hawawezi kusema tofauti
 

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,049
2,000
Huu ni ujinga wa hali ya juu sana. Yaani wataalamu wa afya wanaomgelea hili siku tano baada ya wanasiasa kusema maambukizi yamepungua. Nilitegemea wataalamu watuambie kwanza kabla ya wanasiasa hawa wa hovyo...
Ni shinikizo tu la serikali linawasumbua wataalamu hawawezi kusema tofauti
Kupenda kufikiri uwezavyo, kujijibu na kuhukumu ni aina ya ujinga pia. Unakaataje wakati wamesema wao, hapo ulipo usikute hujawahi kumuona hata mgonjwa wa Covid,wala hujafiwa na ndugu,rafiki na jirani ila unaongea tu..sasa hivyo vifo mitaani viko wapi?

Hata uongee na watu mia hutamuona anaekwambia kua kafiwa na ndugu au jirani kwa Covid, sisi wengine ni watu wa masafa mikoani kila kukicha na kupita huko mitaani lakini hatuoni vifo vya Covid-19. Sijui waTanzania mmerogwa na nani, natambua tatizo lipo lakini halipo kwa kiwango kisemwacho
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
99,277
2,000
Bila kuwepo TESTING kama inavyofanyika katika Nchi nyingi duniani ili kujua idadi ya maambukizi mapya na ya vifo, hii kauli ya chama cha madaktari ni uongo wa kupindukia.

Unasemaje kwamba ugonjwa umepungua wakati hakuna TESTING kwa mwezi sasa? Kwanini hakuna TESTING wakati tumeambiwa kuna maabara mpya? Hiyo maabara imekuwa ni MUSEUM!?
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,297
2,000
Kupenda kufikiri uwezavyo,kujijibu na kuhukumu ni aina ya ujinga pia. unakaataje wakati wamesema wao,hapo ulipo usikute hujawahi kumuona hata mgonjwa wa Covid,wala hujafiwa na ndugu,rafiki na jirani ila unaongea tu..sasa hivyo vifo mitaani viko wapi?hata uongee na watu mia hutamuona anaekwambia kua kafiwa na ndugu au jirani kwa Covid,sisi wengine ni watu wa masafa mikoani kila kukicha na kupita huko mitaani lakini hatuoni vifo vya Covid-19. Sijui waTanzania mmerogwa na nani,natambua tatizo lipo lakini halipo kwa kiwango kisemwacho
Mijitu inapenda vifooo tuu
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,178
2,000
Katika miaka ya themanini na tisini tulikuwa na wimbi kubwa sana la Ukimwi na wala serikali ilikuwa haitanganzi nani kafa na nani mgonjwa. Lakini sisi huko mitaani na makazini kwetu tulikuwa tunajua nani kafa kwa ukimwi na kuna wakati tuliacha kunywa bia pale Kinondoni makaburini container kwa sababu idadi ya wafu waliokuwa wakienda kuzikwa pale kutokana na Ukimwi ilikuwa ni kubwa sana.

Kuna mwandishi mmoja amesema huko kwenye thread nyingine na nikakubaliana naye kuwa, data halisi tunazo sisi wenyewe mitaani kwetu. Tuseme tu ni jarani au mfanyakzi mwenztu yupi amekufa na Korona, na namba zitaunganika tu. Serikali inaweza kutangaza wale waliofia hospitali lakini kuna wale ambao hawakwenda hospitali. Tukisha kuwa na namba hizo bila kupikwa, ndipo tutaweza kuwa na picha halisi.

Binadamau tuna tatizo moja la kupenda kusikia vitu vinavyofurahisha nyoyo na matakwa yetu tu hata kama ni vya uwongo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom