Wizara ya Afya igeni mfano wa Wizara ya Michezo fanyeni harambee isaidie wagonjwa wasio na uwezo wa kumudu vipimo na dawa

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,271
2,024
Hakika nichukue nafasi hii kumpongeza WAZIRI MKUU Mh.MAJALIWA na Kamati nzima ya Uhamasishaji wa HARAMBEE ya kuzichangia Timu zetu za Mpira na kufanikiwa kukusanya Kiasi cha Tsh.BIL.3.7.

Pia nawapongeza Wote waliochangia Wakiongozwa na Mh RAIS wetu Mama SAMIA. Kutokana na HARAMBEE hiyo kufanikiwa naiomba WIZARA nyingie hasa WIZARA ya AFYA iandae Utaratibu kama huu wa HARAMBEE za mara kwa mara kama ulivyofanywa na WIZARA ya Michezo.

Wizara ya AFYA kufanya HARAMBEE itawasaidia Kuwalipia WAGONJWA wengi Wasio na UWEZO wa Kugharamia MATIBABU yao Ndani na Nje ya NCHI. Watanzania wengi wamekuwa wanapoteza MAISHA kwa kukosa Fedha za kugharamia Matibabu wakati Magonjwa waliyonayo yanaweza kutibika.

VIPIMO na MADAWA vimekuwa Gharama sana kiasi cha kushindwa kulipia hivyo Fedha hizo zitawekwa kwenye AKAUNTI MAALUM na kudhibitiwa.

Na UTAMADUNI huu wa Kufanya HARAMBEE kwa Upande wa Wizara ya Afya uwe wa mara kwa mara kwani Wagonjwa hawana Msimu kila siku wapo. Hofu yangu kubwa ni CHANGAMOTO ya UBADHILIFU wa FEDHA za HARAMBEE kwani Wahuni watakuwa Wanazikodolea MACHO.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom