Rais Samia Yuko wapi

Sina tatizo lolote na wewe kwa kuandika hivi, kwa sababu najuwa unaposimamia siku zote.
Ila hii tabia ya kuzungumza uongo ulio wazi, sijui waTanzania tutaiacha lini.
Unaposema "unayo haki ya kikatiba...", hiyo ni katiba gani iliyohalalisha huyo rais unayemlilia na kuimba katiba yenyewe isemavyo. Sasa tabia hii tuiite kitu gani hasa. Mtu kajitangaza mwenyewe kuwa rais, leo unataka haki yako ya kikatiba kwa mtu ambaye haitambui hiyo katiba!

Huku kuanzisha mada zisizokuwa na mwelekeo wowote zitatusaidia kitu gani?

Hivi ukisema tu 'direct' kwamba huyo anayejitangaza mwenyewe kuwa rais hajulikani alipo, kuna kitu chochote kitakachopungua?

Sitafuti ugomvi hapa, ila unafiki ni uginjwa unaotuumiza sana ndani ya taifa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…