Rais Samia umetukosea sana Watanzania, tunajihisi aibu mbele ya walimwengu

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Bandugu,

Nimepokea kwa mshtuko, mshangao na aibu nilipomsikia Rais wa JMT Dk. Samia Suluhu Hassan akiutangazia Dunia kuwa tayari amemaliza kurekodi muvi inayoitwa "Kijiji Cha Milele". Nimejihisi aibu hata kama chawa watakuja kutetea utalii na Kubidhaisha lugha ya Kiswahili duniani. None sense.

Hapa ni ushauri Samia achague kutumikia wananchi kama Mkuu wa nchi au ajiunge na wasanii wa Bongo Movie. Why?

Kuandaa movie kunahitaji muda wa mazoezi na majaribio katika locations zitakazoelekezwa na director. Msanii lazima awepo location. Movie moja inaweza kuchukua hata miezi sita na zaidi. Najiuliza Rais anapata wapi muda wa kushiriki movie na Mchina? Hivi kweli tuko serious?

Magufuli alilalamika kwamba kazi ya Urais ni ngumu maana hata muda wa kulala hupati na ukipata unakuta umelala na rundo la mafaili yanakusubiri kuyasoma na kutolea uamuzi. Rais Samia Suluhu Hassan yeye ana muda wa kucheza film kweli tuko serious?

Moja ya sifa za Marais huko duniani ni kuandika vitabu na makala kuonesha fikra, mawazo na falsafa yake. Sisi Rais anacheza movie. Ama kweli huu ndio muda wapigaji hutumia kuiba fedha za umma. Khaaa!

Nimechoka!
 
Kama wengine wanatumia muda wao kuandika na huyu anatumia muda wake kufanya documentary tofauti yao ni nini? Zote ni records. Huku ni kutafuta sababu za kulalamika bila sababu za msingi kama kawaida ya watanganyika.
 
Achana na huyo mshamba maana haieleweki kama anataka kupewa vitabu au makala za Rais .maana akipewa ataanza kulalamika kuwa makala ni ndefu sana na inawachelewesha watu kufanya kazi .
Kwa Marekani mfano huwezi kuwa Rais bila kwanza kuandika ama kitabu au vitabu au hata makala kuonesha falsafa ya utawala wako. Kwa kuwa Samia aliokota Urais basi tulitegemea kuona maandiko yake kutuonesha ana visheni ipi tuendako. Wa kwetu wengi huandika biography baada ya kuondoka.

Uchawa usikuondolee walau uwezo kidogo wa kufikiri. Mwalimu Julius Nyerere aliandika vitabu vingi sana na makala akiwa madarakani Hali iliyompa heshima duniani hadi leo. Kwa kauli hii ya Samia nimeamini docs nyingi sana anasaini bila kujua amesaini nini maana hana muda. Hata DP World walimchomekea tu mezani kurasa 50 akasaini. Kama ni documentary kwa asisubiri astaafu kwanza badala ya kushindana na kina Irene Uwoya?
 
Bandugu,
Nimepokea kwa mshtuko, mshangao na aibu nilipomsikia Rais wa JMT Dk. Samia Suluhu Hassan akiutangazia Dunia kuwa tayari amemaliza kurekodi muvi inayoitwa "Kijiji Cha Milele". Nimejihisi aibu hata kama chawa watakuja kutetea utalii na

Nimechoka!
Serikali iache kutaka kumfanya rais awe movie star.

Iweke mazingira mazuri kwa movies za Tanzania kufanya vizuri kimataifa.

Kila nikiangakia Netflix naona movies za Ki Nigeria na Kikenya kibao.

Za Tanzania sizioni.

Kwa nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom