Rais Samia: Uanaharakati, vikundi vya kigaidi na maandamano ni mfumo wa vurugu kuwasilisha sauti ya watu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,828
Rais Samia leo July 17, 2023 amefungua mkutano wa wadau wa demokrasia barani Afrika unaowahusisha viongozi wakuu wastaafu mjini Arusha. Sehemu ya hotuba yake ameongelea namna ambazo si nzuri katika kufikisha hisia za wananchi.

Rais Samia: Kushindwa kwa Serikali kuhudumia mahitaji ya msingi imeibua malalamiko kwenye sehemu ya bara la Afrika. Baadhi kudharau na kufanya baadhi ya watu kwenye jamii kupinga na kudharau mamlaka ya Serikali kwa kuanzisha mifumo ambayo inatumia vurugu kuwalisha sauti ya wananchi.

Hii inajumuisha wanaharakati, vikundi vya kigaidi na maandamano. Na hii ni sehemu baadhi ya vipengele vya demokrasia kama uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni vinatumika vibaya.

Pia, Soma=> Rais Samia akifungua Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Barani Afrika wa Viongozi wakuu wastaafu, leo Julai 17, 2023

UVCCM kuandamana nchi nzima kuunga mkono serikali, pia wamtaka msajili wa vyama vya siasa kuchukua hatua stahiki

Hayo yamefahamika wakati mwenyekiti wa UVCCM kada Mohamed Kawaida alipokuwa anaongea na viongozi wa UVCCM na kutangaza azma ya kuandamana kila kona ya nchi kuunga mkono alichoita makubaliano ya serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu bandari ....

UVCCM wataanza maandamano yao mkoani Dar es Salaam hapo tarehe 18 Julai 2023 amesema Mohamed Kawaida mwenyekiti wa UVCCM taifa na kisha kuendelea kuandamana katika mikoa mingine kuunga mkono hatua za serikali kuhusu bandari ...
 
Samia anayaogopa maandamano maana ameshaona hiyo ndio itakuwa njia ya mwisho kumzibua masikio yake, ili atusikie tukimwambia ule mkataba wa bandari ni mbovu unaomkandamiza mtanganyika na kuidhalilisha ardhi yetu, utu wetu, na mipaka yake, ameyataka mwenyewe kwa ukaidi wake.

Sasa ameona ayaweke maandamano kundi moja na vikundi vya kigaidi, hajui maandamano yapo kisheria, hiyo ni haki ya mtanganyika, kama anajua vilipo hivyo vikundi vya kigaidi aliagize jeshi la polisi likavikamate, asipoliagiza jeshi maana yake anafumbia macho vikundi vya kihalifu, hatufai.

Lakini asijaribu kutuchezea "mind games" ili kupunguza nguvu za kuzidai bandari zetu zote waTanganyika walizopewa waarabu, kwa huu mpango wake amefeli tayari, muhimu namshauri tu aliagize jeshi la polisi litoe ulinzi kwa waandamanaji hiyo siku ikifika, sasa ndio anavuna matunda ya ukaidi wake mwenyewe.
 
Si alikuwa anaigiza mwanademokrasia!

Kiko wapi sasa?
Uzalendo umeshamshinda.. kule kumpa Mbowe kesi ya ugaidi hakukuwa kwa bahati mbaya, ni yeye ndie aliagiza yote yatokee, sasa ndio tunazidi kuziona rangi zake halisi.

Hawezi kuzuia maandamano ya watanganyika watakaodai rasilimali zao, asijihami mapema kwa sababu zake nyepesi zinazovunja sheria.
 
Kama kaziba masikio sasa atasikiaje hizo sauti bila maandamano, makwenzi na kuzodolewa? Huyo kashasema hasikii kama kenge kwahiyo ni kipondo cha kichwa tu kitamfanya sauti ipenye sikioni.
 
Rais Samia leo July 17, 2023 amefungua mkutano wa wadau wa demokrasia barani Afrika unaowahusisha viongozi wakuu wastaafu. Sehemu ya hotuba yake ameongelea namna ambazo si nzuri katika kufikisha hisia za wananchi.

Rais Samia: Kushindwa kwa Serikali kuhudumia mahitaji ya msingi imeibua malalamiko kwenye sehemu ya bara la Afrika. Baadhi kudharau na kufanya baadhi ya watu kwenye jamii kupinga na kudharau mamlaka ya Serikali kwa kuanzisha mifumo ambayo inatumia vurugu kuwalisha sauti ya wananchi.

Hii inajumuisha wanaharakati, vikundi vya kigaidi na maandamano. Na hii ni sehemu baadhi ya vipengele vya demokrasia kama uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni vinatumika vibaya.

Pia, Soma=> Rais Samia akifungua Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Barani Afrika wa Viongozi wakuu wastaafu, leo Julai 17, 2023

Wadhibitiwe haraka
 
Hivi majuzi akiwa mbele ya Umma wa Watanzania, akiwa mbele ya vyombo vya habari vya Nje, na huku pembeni akiimbiwa mapambio na wakina Lucas, Faiza, na wengineyo- Kwamba amerudisha Demokrasia za Siasa na za Kiuchumi-aliutangazia umma na Dunia kuwa anakubaliana na mtazamo wa CHADEMA wa never never never again!

Kulikoni?

Mbona alikuja kumkana mtangulizi wake na Vijembe,
eb5ae8d3-fdc5-4954-a51f-6268c5b129e5-jpeg.1971057
au Namsingizia jamani?
 
Uzalendo umeshamshinda.. kule kumpa Mbowe kesi ya ugaidi hakukuwa kwa bahati mbaya, ni yeye ndie aliagiza yote yatokee, sasa ndio tunazidi kuziona rangi zake halisi.

Hawezi kuzuia maandamano ya watanganyika watakaodai rasilimali zao, asijihami mapema kwa sababu zake nyepesi zinazovunja sheria.
Watanzania tuna akili na ni wengi na tunao uwezo wa kujitokeza hadharani tofauti na watanganyika wenye ukosefu wa jeuri ya kutoka huko nje wakaonekana.

Watanganyika wengi ni mashujaa wa nyuma wa keyboard.
 
Hivi majuzi akiwa mbele ya Umma wa Watanzania, akiwa mbele ya vyombo vya habari vya Nje, na huku pembeni akiimbiwa mapambio na wakina Lucas, Faiza, na wengineyo- Kwamba amerudisha Demokrasia za Siasa na za Kiuchumi-aliutangazia umma na Dunia kuwa anakubaliana na mtazamo wa CHADEMA wa never never never again!

Kulikoni?

Mbona alikuja kumkana mtangulizi wake na Vijembe,
eb5ae8d3-fdc5-4954-a51f-6268c5b129e5-jpeg.1971057
au Namsingizia jamani?
Hicho Chuma pichani kilitawala Dunia!
 
Back
Top Bottom