Rais Samia Suluhu alazimika kufuta post yake ya Twitter aliyotoa taarifa ya kuwasili Dar. Ni baada ya malalamiko kuhusu mabando kuzidi kwa wachangiaji

Makabwela ambao wametoa malalamiko lukuki ya malipo ya bando jipya wamemlazimisha Rais Samia Suluhu kufutilia mbali post yake ya Twitter aliyoitoa ambapo alitoa taarifa rasmi ya kuwasili Dar leo.

Hii inakuwa post yake ya kwanza kuifutilia mbali tangia awe Rais rasmi wa Jamhuri ya muungano ambapo wengi wa wachangiaji wake wamemuomba kutengua uteuzi wa waziri wa teknolojia ya habari ndugu Faustine Ndugulile na mkurugenzi mkuu wa TCRA kutokana na kutokuchukulia maanani uzito wa malalamiko yao kuhusu malipo ya bando la mitandao yote ya mawasiliano nchini.

Tusubiri tuone!
Rais kashindwa kusikiliza malalamiko ya watu?

Rais hapendi uwazi?
 
Mwenzie huyu hapa analialia.


Sina shaka naye unga ukizidi maji atajitoa tu seems anapenda kupigiwa makofi tu.
 
Nashauri ati tweet mara chache sana panapo ulazima hii mambo ya kuwa informed point to point haina mantiki waendesha hio acc angalieni contents za kupost
 
Hakuna kiongozi yeyote Duniani anayeshinda mtandaoni aliyefanikiwa hakuna na aliyemshauri huyu mama kuwa mtu wa mitandaoni bhasi ajue soon kutaongozwa na mawazo ya wahuni wa Twitter naona anaenda kuungana na wakina Kigwangala
Walioitengeneza mitandao ni watu wenye akili nyingi sana na waliona mbali. Kwa rais kuandika kitu mtandaoni sio kosa kumbuka nae ni mtu wa karne ya sasa.
 
Hao ni 2% tu ya raia wote hapa nchini.

Hakuna mtu anapendwa na kuchukiwa na wote, hakuna duniani.

Kama unabisha nioneshe mmoja wapo?

Kwenye familia yako tu mitoto yako kuna baadhi haikuopendi sembuse nchi ya watu milioni 60?

Hata rais wangu Samia hawezi kuingia kwenye mtego wa kijinga kwamba eti atapendwa na kila mtu
Hayuko pale kwa nia ya kumfurahisha kila mtu. Yupo pale kutimiza yale yaliyoandikwa ndani ya ilani ya kurasa 303.

Hakuna awezaye kupendwa na kila mtu. Yesu aliwalisha watu kwa kufanya miujiza lakini miongoni mwao ndio waliokuja kumuua msalabani.
 
Makabwela ambao wametoa malalamiko lukuki ya malipo ya bando jipya wamemlazimisha Rais Samia Suluhu kufutilia mbali post yake ya Twitter aliyoitoa ambapo alitoa taarifa rasmi ya kuwasili Dar leo.

Hii inakuwa post yake ya kwanza kuifutilia mbali tangia awe Rais rasmi wa Jamhuri ya muungano ambapo wengi wa wachangiaji wake wamemuomba kutengua uteuzi wa waziri wa teknolojia ya habari ndugu Faustine Ndugulile na mkurugenzi mkuu wa TCRA kutokana na kutokuchukulia maanani uzito wa malalamiko yao kuhusu malipo ya bando la mitandao yote ya mawasiliano nchini.

Tusubiri tuone!
Aachane na mitandao ya kijamii kama anataka kufanya kazi bila kufuata miluzi ya watu...
 
Walioitengeneza mitandao ni watu wenye akili nyingi sana na waliona mbali. Kwa rais kuandika kitu mtandaoni sio kosa kumbuka nae ni mtu wa karne ya sasa.
Kitu chochote chenye addiction kina madhara hata kiwe ni kizuri namna gani pia mitandao ya viongozi ni tofauti na ww ukiona kiongozi ameTweet bhasi kuna kitu anakizungumzia ambacho kinahusu nchi au jambo muhimu ndo maana account nying za viongozi ni verified sasa ukiona mtu anatweet kuwa "NIMEFIKA DAR " hili ni tatizo pia jua hakuna kiongozi yeyte anayeshinda mitandaoni aliyefanikiwa mfano Trump,Kigwangalla,Mwigulu. Hao ni wachache tu fanya kazi ionekane ndo tunachotaka si kupost kuwa nimefika au nimefanya hv
 
Ile akaunti sijaielewa kabisa...hao wanaoiendesha wapunguze ushamba kidogo

Akaunti ya Mkuu wa Nchi huwa haipost mambo hovyo hovyo....wafuatilie akaunti za viongozi wenzake wajifunze mambo yalivyo

Au hata kwa Mtangulizi wake Hayati JPM..

May be anayeiendesha ile akaunti ya Mama yetu Raisi inawezekana mwanamke mwenzie..... kwa sabbu wanawake kwa vijipost post hawajambo wanadhani bado ni VP......

Kiufupi yule tayari ni Mkuu wa Nchi..Dunia nzima inamfuatilia 24hrs
Kuna Rais aliyekuwa ana tweet mara kwa mara kumzidi Trump ?
 
Kitu chochote chenye addiction kina madhara hata kiwe ni kizuri namna gani pia mitandao ya viongozi ni tofauti na ww ukiona kiongozi ameTweet bhasi kuna kitu anakizungumzia ambacho kinahusu nchi au jambo muhimu ndo maana account nying za viongozi ni verified sasa ukiona mtu anatweet kuwa "NIMEFIKA DAR " hili ni tatizo
Ni maamuzi yake kuandika akitakacho. Usimshushe mtu thamani kwa kitu kidogo sana.
 
Kama hawana bando waliwezaje kuona na kujibu twita yake!
Na wewe vp?kwani wanaolalamika hawana mabundle au lengo Bei zishuke?kwa maana ni kwamba bundle unaambia GB 2 ukisikiliza kawimbo kamoja tu Utube hapo hapo eti salio la bundle kimeisha kwa kweli ni mateso
 
Asipokuwa makini, na yeye atajikuta anachukiwa na wananchi walio wengi kama ilivyokua kwamtangulizi wake, aliyechagua kuwa mkaidi mwanzo mwisho.
Kwamba magu alichukiwa na wananch weng..mbona uongo ni mkubwa sana mjomba ..hiv unafaidika na nn...unalipwa au
 
Back
Top Bottom