Rais Samia: Sitangazi hadharani kiasi cha Ongezeko la Mshahara ili wafanyabiashara wasipandishe bei

Mwaka jana pesa ineongezwa lakini leo hakuna mfanyakazi anayekumbuka, wote wanataka iongezwe tena..

Hiyo ndio kusema kazi iliyofanyika mwaka jana haina maana.
Vipi gharama ya maisha ya mwaka jana na mwaka huu ziko sawa?
 
Natamani sana mishara ipunguzwe kwa makundi yafuatayo;

1. Wabunge.
2. Mawaziri
3. Majaji
4. Wakurugenzi watendaji

Haya ndio makundi yanayo lipwa vizuri zaidi, pamoja na mshahara mzuri lkn bado wanapewa nyumba, gari na ulinzi juu.

Wakurugenzi watendaji” hapa umeweka jumla sana. Ila kama wale wa halmshauri, manispaa na jiji wanalipwa hela ndogo sana. Inabidi waongezwe hata mara 2 ya wanachokipata sasa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) leo tarehe 01 Mei, 2023 mkoani Morogoro.



Rais amewasili uwanjani akiambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson pamoja na Viongozi wengine wa Kiserikali na Vyama vya wafanyakazi.

Kauli Mbiu ya mwaka huu ni Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi. Wakati ni Sasa.”

Kinachoendelea sasa ni maandamano ya vyama vya wafanyakazi wanapita mbele ya Rais na Meza kuu wakiwa na Mabango yenye jumbe mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa anazungumza;
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa amesema tangu Rais Samia aingie Madarakani, wafanyakazi 7108 mkoani humo wamepandishwa madaraja huku wengine 2030 wameajiriwa kupitia ajira mpya na kibali kingine cha kuajiri watu 3861 tayari kimeshatolewa.

View attachment 2605963
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa
Aidha, mkoa huo kwenye mwaka huu wa fedha umepanga kuanzisha ranchi mpya 4 pamoja na kufufua mashamba mengine makubwa ili kuongeza ajira kwa vijana.

Amemshukuru Rais Samia kwa uongozi mzuri na anatumaini chini ya Utawala wake Maslahi ya wafanyakazi nchini yatazidi kuboreshwa.

Katibu Mkuu wa TUCTA anazungumza;
Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi TUCTA, Heri Mkunda amesema wafanyakazi ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa jitihada anazofanya Rais Samia kwenye nyanja zote za maisha.

View attachment 2605964
Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi TUCTA, Heri Mkunda
Amesema Kauli Mbiu ya mwaka huu waliibuni kuonesha nia ya kuwawezesha wafanyakazi wapate haki zao, mikataba ya ajira na mishahara iliyo bora ili kuongeza tija na ufanisi kwenye maeneo ya kazi.

Kwa niaba ya Wafanyakazi, amemshukuru Rais Samia kwa kufanya mambo makubwa yanayowagusa. Ametoa ahadi ya kuendelea kuwa watiifu huku wakijituma kwenye maeneo ya kazi.

Mwaka jana ongezeko la Mshahara lilikuwa 23.3% likigusa wafanyakazi wa kika cha chini cha Mshahara, amesema wanaendelea kupiga magoti na kubisha hodi ili aendelee kuwafikiria.

Ameomba kitengo cha Idara ya Kazi kilicho chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kiboreshwe na kuongezewa wafanyakazi, ameishujuru Serikali kwa kuboresha afya kwa watanzania kupitia mpango bima ya afya kwa wote.

Rais Samia anazungumza;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewashukuru waandaji wote wa Maadhimisho ya mwaka huu kwa kuwezesha yafane na yaende kama yalivyopangwa.

Amesema Mei Mosi ni siku ya kutambua mchango na kutoa heshima kwa wafanyakazi kwa kazi kubwa wanayofanya ndani ya taifa. Umadhubuti wa Taifa hili upo kwa sababu ya wafanyakazi.

Pamoja na kudai mishahara bora, uadilifu na weledi kazini ndio utaleta maisha bora kwa wafanyakazi.

Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya kazi serikalini na katika sekta binafsi zipatikane ajira zenye usalama na ajira za staha kwa wote. Pia, madai yote ya mwaka jana yametekelezwa kwa zaidi ya 95%

Nafikiri ni Tanzania tu Chama cha Wafanyakazi kinampigia magoti Rais na kuomba nyongeza.

Kwa wenzetu chama kina demand nyongeza na serikali inasikiliza. Nyongeza serikali inakata Meza moja na vyama vya wafanyakazi kukubali ana ni kiasi gani wanakubaliana. Ila Bongo wanastukizwa na kupewa mbuzi kwenye gunia... Kama last year.
 
Mama kasema mambo ni moto na mambo ni faya kwa wafanyakazi. Mishahara ya nyongeza kila mwaka kwa wafanyakazi itarudishwa kama zamani, sheria za kazi na kanuni litaafanyiwa kazi na kuna chombo mahususi cha serikari cha kusimamia afya na usalama wawa wafanyakazi mahali pa kazi.

"Lakin yote hayo hatutasema hadharan ni kwa kias gan marupurupu haya tumeyaongeza maana wakisikia huko mtaani watongeza bei za bidhaa"

"Walimu pia tumewasikia na swala malipo ya ziada baada ya muda wa kazi tunalifanyia kazi, walimu na madaktari ni chama kubwa" walimu oyeee!

"mwisho kabisa tufanye kazi kwa bidii na kwa kujituma" ahsanten sana
 
Back
Top Bottom