figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Salaam Wakuu.
Kwa mjibu wa Katiba, rais ameajiriwa na Wananchi kuwatumikia. Hivyo kama Mwajiri, namtaka au namuamuru rais Samia awajengee kivuko hawa Wananchi. Ziara yake moja inatosha kuwawekea kuvuko hawa wananchi.
Nimefika Nzoka Momba, Wananchi wanavuka kama Makomandoo unaweza hisi ni mafield marshal.
Pamoja na kwamba wanalipa kodi na Tozo, bado Wananchi wa Momba Mkoani Songwe wanaendelea kuiomba Serikali kuwajengea kivuko kinachounganisha Kata mbili za Nzoka na Ipatikana kutokana na kuvunjika kwa kivuko cha awali kwa zaidi ya miaka minne sasa. Kata zote zina Viongozi wa CCM.
Wanafunzi, wajawazito na Wazee, wanapita kwa kubembea kama Kima.
Mkuu wa Mkoa na Wilaya wafukuzwe kwani hawakusaidii. Utakosaje hela ya kujenga sehemu hii kwa miaka minne?
Pia namtaka Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG akakague hela za Ujenzi zilizotumika na bado hili daraja halikujengwa. Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe, ilitumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.507,936,715.62 kwa ajili ya ujenzi lakini hili daraja halijajengwa.
Pia Milioni 100 zilizobaki kwenye Ujenzi wa madarasa(Mkopo wa Covid-19 wa Tril 1.3 au Pesa za Samia), zipelekwe kujenga hili daraja sio kurudishwa Hazina.
Natoa Amri.
Nakala kwa:
Mkuu wa Mkoa: Omary Mgumba
Mkuu wa Wilaya Momba: Fakii Lulandala
Mkurugenzi wa Wilaya ya Momba Regina Bieda