benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Akiendelea na ziara mkoani Mbeya, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini, pamoja na Wakuu wa Wilaya kuanza kujipanga kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 8,000 kwa ajili ya shule za Sekondari ambayo yatahitajika ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi watakaoanza kidato cha Kwanza mwaka 2023.
Kwa mujibu wa takwimu jumla ya wanafunzi 1,534,141 wanatarajiwa kumaliza darasa la Saba mwaka huu (2022), ambapo kati yao wanafunzi 1,257,996 wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza. Ongezeko hilo litapelekea hitaji wa vyumba vya madara 7,986 ii kuwezesha Wanafunzi wote kujiunga na kidato cha kwanza.
Bajeti ya Serikali mwaka wa fedha 2022/23 imeonesha kuwa madarasa hayo yatajengwa kwa kupitia ruzuku kutoka Serikali Kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri na fedha za washirika wa maendeleo.