Rais Samia Apeleka Bilioni 1.8 Utekelezaji wa Miundombinu ya Maendeleo Wilaya ya Ngara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
Ngara
Januari 10, 2024

TAARIFA YA KUPOKEA TZS 1,816,000,000.00 KWA AJIRI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO - Ngara.

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. NDAISABA GEORGE RUHORO anawatangazia wananchi wote kuwa, DKT SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma fedha tajwa hapo juu ili kuendelea kuboresha huduma za kijamii kwa Wananchi wa Jimbo la Ngara.

Ujio wa fedha hii ni matokeo mazuri ya kazi kubwa na nzuri inayofanywa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ngara akiwemo Mbunge ambaye ndiye anayewasemea wananchi sambamba na kuomba fedha hizi kutoka kwa Rais Samia akishirikiana na Madiwani wote wa Wilaya ya Ngara.

Ngara imekuwa Wilaya ya Mfano kwenye utekelezaji bora wa miradi ya maendeleo chini ya Usimamizi wa Kanali MATHIAS KAHABI, Mkuu wa Wilaya ya Ngara na Ndugu SOLOMON KIMILIKE, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara na fedha zilizokuja zimepokelewa na zitasimamiwa vema kabisa na viongozi hawa.

Taarifa ya fedha zilizotumwa na mgawanyo wake ni Kama ifuatavyo;

1. TZS 800,000,000 - Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Ngara iliyopo Kata ya MBUBA.
2. TZS 50,000,000 Kukamilisha jengo la OPD Zahanati ya Rulenge.
3. TZS 50,000,000 Ukamilishaji wa wodi ya Wazazi Kituo cha Afya cha Nyakisasa.
4. TZS 8,400,000 ukamilishaji wa vyoo S/M Shule shikizi Mukalela
5. TZS 10,500,000 ujenzi matundu 5 ya vyoo shule shikizi Nyamikono
6. TZS 9,100,000 ujenzi wa matundu 5 ya vyoo Shule Shikizi chamabale.
7. TZS 60,000,000 ujenzi wa Madarasa 3 shule ya Msingi Mabawe (Shule Kongwe)
8. TZS 60,000,000 ujenzi wa Madarasa 3 shule ya Msingi Ngara Mjini (Kongwe)
9. TZS 60,000,000 ujenzi wa Madarasa 3 Shule ya Msingi Kanyinya
10. TZS 128,000,000 ujenzi wa Bweni la watoto wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Murugwanza
11. TZS 200,000,000 ujenzi wa Madarasa 10 Lukole Sekondari.
12. TZS 40,000,000 ujenzi wa Madarasa 2 Rusumo Sekondari.
13. TZS 80,000,000 ujenzi wa Madarasa 4 Murusagamba Sekondari.
14. TZS 40,000,000 ujenzi wa Madarasa 2 Muyenzi Sekondari.
15. TZS 80,000,000 ujenzi wa Madarasa 4 Ngara High School
16. TZS 80,000,000 ujenzi wa Madarasa 4 kabanga sekondari.
17. TZS 20,000,000 ujenzi wa matundu 10 ya vyoo LUKOLE SEKONDARI

Fedha nyingine zimepelekwa kuboresha miundombinu ya vyoo kwenye shule za sekondari za Kabanga, Ngara High School, Muyenzi, Murusagamba, Rusumo na Lukole kwa TZS 8,000,0000.00 kila shule ya Sekondari.

Mh Ndaisaba Ruhoro ameomba fedha nyingine kwa ajili kupeleka Madawa, Vifaa Tiba, vitendanishi n.k kwenye vituo Vya kutolea huduma za AFYA VYA SERIKALI NA VILE VINAVYOMILIKIWA NA BAADHI YA MADHEHEBU YA DINI. Mhe RUHORO atatoa taarifa hivi karibuni juu ya fedha hizo Baada ya kufika na taratibu za kugawanya fedha hizo kukamilika.

Utoaji wa taarifa hii ni Mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi ya Mbunge Ruhoro kwa wanangara juu ya kupata taarifa na kushiriki katika maendeleo ya Jimbo la Ngara.

Sarah Kenneth
Kaimu Katibu wa Mbunge

WhatsApp Image 2024-01-10 at 23.23.59.jpeg
 
Back
Top Bottom