Rais Samia: Mabadiliko yametokea kwa sababu ya kutokuelewana

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Rais Samia amesema sababu nyingine ya kupangua wizara ni kwa sababu ya kutoelewana kati ya mawaziri na makatibu wakuu na manaibu waziri. Hali hiyo imeonesha kuwa kazi hazifanyiki.

Rais amesema hii ni mara ya mwisho kupangua kwa sababu ya kutokuelewana, wakati mwingine atawaondoa wote badala ya kuwapangua kama alivyofanya sasa.

Rais ameyasema hayo katika hotuba yake baada ya kuwaapisha wateule.
 
Raisi kasema kapangua kwasababu ya kutokuelewana. Je hawa watoto wa vigogo ambao wamepanguliwa wana tatizo la kujiona na nguvu kuliko maboss wao?

Mama angekua muwazi tu. Asiogope style ya jpm ilikua bora sana. Hao wanaogombana bila kuelewana sio kuhusu weledi na utendaji kazi.

Mawaziri, naibu mawaziri na makatibu wakuu hugombana kutokana na maslahi binafsi. Yeye mwenyewe aliwafungulia njia kuwaambia anajua wanapata kwenye nafasi zao. Kisha akawaambia kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake ya malisho.

Hapo kashawakosesha amani. Wenye kamba hazina malisho lazima fitna na husuda zizuke. Hapa mama katoa nafasi ya ubinafsi na ulafi kukubalika. Kwa hivyo tuseme kutoelewana kwa uhakika ni roho za kifisadi tu.

Mama anasema sasa mwisho kwamba atakua anawatema. Yaani ilitakiwa kuwatema tu wateuliwa kama hao. Warudishwe nafasi za chini badala eti kuwavumilia eti kama mama. Hapo kwenye urais wananchi wanataka kuona rais kuliko mama. Wakigombea kamba wateme tu mama.
 
Huyo Rizimoko naona anabebwa tu kwasababu ni mtoto wa master wake, kinyume na hapo nae angetakiwa apigwe chini, sioni utendaji wowote toka kwake.
Hii nchi ngumu sana!!yupo wapi waziri Lukuvi?msemo wa mchungaji msigwa kuwa akili ndogo inapoongoza akili kubwa ni vulugu tupu!? Hii panga pangu wala haina tija, na hata ukimchukua MHADZABE huko polini akapewa wizara anaongoza fresh tu!!!
 
Kwamba, hapo kwenye urais, wananchi wanataka Kumuona Rais kuliko mama😳😳

Paragraph ya mwisho ilipaswa itoe heading ya Uzi.
 
Rais Samia amesema sababu nyingine ya kupangua wizara ni kwa sababu ya kutoelewana kati ya mawaziri na makatibu wakuu na manaibu waziri. Hali hiyo imeonesha kuwa kazi hazifanyiki...
Fukuza huyo korofi.

Kwa hiyo unapomhamisha kwenda pengine amebadikika?

Mwenyewe uliwaambia wale Kwa urefu wa mfungio wao.
 
Hii nchi ngumu sana!!yupo wapi waziri Lukuvi?msemo wa mchungaji msigwa kuwa akili ndogo inapoongoza akili kubwa ni vulugu tupu!? Hii panga pangu wala haina tija, na hata ukimchukua MHADZABE huko polini akapewa wizara anaongoza fresh tu!!!
Mhadzabe atafaa sana Wizara ile ya Utalii. Kwanza yeye shida yake ni asali na nyama kidogo ya nyani. Hana habari kabisa na meno ya tembo.
 
Mama saa zingine anajiharibia mwenyewe, kwa hivyo watu walioboronga wanapanguliws tuu kwamba watanzania wengine smart waku cover nafasi wameisha kwenye jamii au??
Upuuzi.
 
Rais Samia amesema sababu nyingine ya kupangua wizara ni kwa sababu ya kutoelewana kati ya mawaziri na makatibu wakuu na manaibu waziri. Hali hiyo imeonesha kuwa kazi hazifanyiki...
Mwenye matatizo ni mteuaji, anaangalia uswahiba badala ya weledi
 
Mama saa zingine anajiharibia mwenyewe, kwa hivyo watu walioboronga wanapanguliws tuu kwamba watanzania wengine smart waku cover nafasi wameisha kwenye jamii au??
Upuuzi.
Wewe ndio una matatizo ndio maana anawang'oa Kwa kuwapiga chini na wanaobahatika hupangiwa sehemu zingine
 
Rais Samia amesema sababu nyingine ya kupangua wizara ni kwa sababu ya kutoelewana kati ya mawaziri na makatibu wakuu na manaibu waziri. Hali hiyo imeonesha kuwa kazi hazifanyiki...
Jamani, jamani, hii ni sababu kweli ya kuwa pangua? Hivi wakiachwa wote kwa pamoja taifa linapoteza nini hasa kwa kukosekana kwao?
 
Back
Top Bottom