Rais Samia: Kuuza ovyo Tanzanite kunashusha thamani yake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,385
2,000
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Madini ya Tanzanite yanapouzwa ovyo yanashusha thamani yake, akisema yanatakiwa kuuzwa kwa mpangilio maalum

Ameeleza hayo leo akizungumza na Wananchi Manyara na kuongeza, "Endapo yatauzwa kwa mpangilio na kuachiwa kidogo kidogo duniani thamani yake itapanda"

Kuhusu changamoto za Vituo vya Afya na Madarasa Wilaya Simanjiro, Rais Samia amesema Serikali inakusanya fedha na ujenzi utafanyika
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
7,459

Muulizeni huyo Miss utalii ni nani aiachie kidogo kidogo?
 
tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
13,601
2,000
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Madini ya Tanzanite yanapouzwa ovyo yanashusha thamani yake, akisema yanatakiwa kuuzwa kwa mpangilio maalum

Ameeleza hayo leo akizungumza na Wananchi Manyara na kuongeza, "Endapo yatauzwa kwa mpangilio na kuachiwa kidogo kidogo duniani thamani yake itapanda"

Kuhusu changamoto za Vituo vya Afya na Madarasa Wilaya Simanjiro, Rais Samia amesema Serikali inakusanya fedha na ujenzi utafanyika
Mama atulie na kulea wajukuu hajui lolote yupo tu,tanzanite jk aliacha gram AAA+ ikiwa 1.6m alivyoingia meko na yeye thamani ilishuka mpka laki 5 kwa AAA+...unakamata wanunuzi na wachimbaji kisha unawapa kesi,unategemea nini zaidi ya kuua soko,wanunuzi wakubwa wote waliondoka wamebaki waswahili wenye mitaji midogo.
Halafu anakuja mjinga n kusema tanzanite ikatwe hapohapo mererani wakati hakuna mtaalam wa kukata sanasana watakuharibia jiwe lako litashuka thamani
 
Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,470
2,000
SSH wewe ndio rais, sasa unangoja nani akwambie ununue Tanzanite inayochimbwa na kuihodhi BOT? Au sio wewe uliokuwa unasema BOT wachunguze jinsi ya kuruhusu Crypto currency wakati Tanzanite tu inakushinda?

BTW One crypto currency = more than 50 million shillings. Sijui mwenzetu unazo crypto ngapi? Je, huo uchunguzi unafanyika kwa pesa za walipa kodi hawa hawa wanaoshindia One dollar a day? Ama kweli Tanzania imepatikana.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom