benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,035
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa Tsh. Milioni 10 kwa kila goli ambalo Taifa Stars itafunga katika michuano ya kufuzu fainali ya michuano ya AFCON inayoendelea.
Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa imesema Rais Samia ameahidi kuanza kutoa fedha hizo kuanzia mechi ijayo ambapo Taifa Stars itarudiana na Timu ya Taifa ya Uganda (Uganda Cranes) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Ahadi hiyo inakuja wakati ambapo pia ameahidi kuipatia timu hiyo donge nono la TZS milioni 500, endapo itafanikiwa kufuzu mashindano hayo ambayo yatafanyika Januari 2024 nchini Ivory Coast.
Aidha, Rais Samia amewapongeza Wachezaji, Benchi la Ufundi, TFF na Wadau wote walioshiriki katika maandalizi ya Taifa Stars.
Pia soma: Rais Samia kununua kila goli Tsh. Milioni 5 mechi za Simba, Yanga CAF