JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Wadau nina jambo hapa tuweke siasa kando tujadili maendeleo
Baada ya huu uzi hapa chini kutolewa
Rais Samia wasaidie wananchi hawa wa Kigamboni kuna wakubwa ‘wanawapiga’ katika ardhi yao
Inaelezwa kuwa kuna kigogo mmoja pande za kule kwenye kuvuka maji kule, Kigamboni anahaha kupiga simu kwenye vyombo vya habari kwa ajili ya kuzuia habari hiyo kutoka. Tunaamini JF naye hamtakuwa sehemu ya uminywaji wa haki ambao unadaiwa kuwa unaendelea kwa wakazi hao zaidi ya 2000.
Rais Samia, wewe ni mama yetu, Rais wa Watanzania wote, matajiri na masikini, wasaidie wamama na wananchi hao kwa ujumla wao, kwa kuwa taarifa za watu wa karibu na kiongozi huyo ambaye ni mteule wako ni kuwa anapiga simu kwenye vyombo vya habari kuzuia taarifa hiyo kusambaa.
Kinachoshangaza zaidi ni kuwa kwenye video hiyo hajatajwa jina wala hakuna sehemu ambapo jina lake limetajwa lakini bado hataki Tanzania ijue kuhusu habari hiyo wakati malalamiko yapo wazi tu hata Mange Kimambi naye aliipost.
Kuna vitu havipo sawa, JF saidieni hawa raia wapate haki yao, kuna upigaji wa maana hapo unaendelea kimya kimya wadau japo sina uhakika na hilo lakini mazingira yanajionyesha hivyo.
-------------------------------------------------------------------------------------------------
Habari yenyewe ni hii ilivyokuwa mwanzoni.
Inadaiwa kuwa huu mchongo unawahusisha vigogo wa kwenye mamlaka za juu na ndiyo maana kuna danadana zinaendelea.
Taarifa za uhakika kutoka wa watu ambao wamekuwa sehemu ya waathirika wa mradi huo kwa ardhi yao kutaka kuuzwa kwa bei ya chini amedai kuwa wameshafanya vikao vingi lakini hakuna muafaka na hiyo ni kwa kuwa kuna michezo mingi michafu inaendelea nyuma ya pazia.
Inaelezwa kuna wakati walikaa kikao na viongozi wa juu tena baadhi yao ni watauliwa wa Rais Samia kuhusu mgogoro huo, wakapikwa mkwara kuwa hawatakiwi kurekodi kwa kifaa chochote mazungumzo hayo, iwe ni kwa simu au kamera ya kawaida.
Kuna wananchi zaidi ya 2000 katika madai hayo, kati yao wapo wachache ambao wameshapozwa na hivyo wamekubali kuuza kwa bei hiyo ya buku tatu kwa square mita, wakati wenzao wengi wanataka buku nane kwa square mita.
Baada ya kiongozi mmoja mkubwa kufika eneo hilo na kufanya kikao, wakaamua kuunda kamati ndogo ili kushughulika na suala hilo, lakini hao wachache nao wakapewa kazi ya kuwashawishi wenzao ili wakubali kwa kuwa kuna maslahi ya wakubwa.
Najua Serikali ya mama Samia ni sikivu na lazima itadili na hao vigogo wanaotaka kuwanyonya wananchi kwa maslahi yao binafsi ya wachache.