Rais Samia kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi AU, ETHIOPIA

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan usiku wa kuamkia leo, Jumapili Februari 18.2024 amewasili jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU), ikiwa ni saa chache tangu awaongoze waombolezaji kwenye mazishi ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa yaliyofanyika Februari 17.2024 kiijijini kwao Ngarash, wilaya ya Monduli, mkoani Arusha

Kupitia kurasa zake binafsi za mitandao ya kijamii, Rais Dkt. Samia amechapisha maelezo yafuatayo;

"Baada ya kutoka kijijini Ngarash mkoani Arusha nimewasili Addis Ababa nchini Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika" -Rais Samia

"Katika mkutano huu, pamoja na mambo mengine tutajadili kuhusu amani na usalama wa nchi zetu, na sera na majawabu kuhusu elimu na ujuzi, ikiwa ni maeneo yanayogusa maisha ya wakazi zaidi ya bilioni moja wa nchi wanachama" -Rais Samia

Katika hatua nyingine, akiwa kwenye mkutano huo Rais Dkt. Samia anatarajiwa kuzindua Sanamu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoko makao makuu ya Ofisi za AU, Addis Ababa Ethiopia.

20240218_110318.jpg
 
Back
Top Bottom