Rais Samia ashiriki mkutano wa 23 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki, leo Novemba 24, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki. Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni "Kuharakisha ufufuaji wa uchumi kupitia hatua za hali ya hewa na kuimarisha usalama wa chakula kwa ajili ya kuboresha maisha" (Theme Accelerating Economic Recovery through Climate Action and enhancing Food Security for Improved Livelihoods) katika Hoteli ya Ngurdoto - Arusha


View: https://www.youtube.com/live/oEnJHnZUVIg?si=cQkGvwX94c0gMXdT
IMG_9172.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 24 Novemba, 2023.

IMG_9173.jpeg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Somalia, Mhe. Hassan Sheikh Mohamud, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngurdoto Mkoani Arusha, tarehe 24 Novemba, 2023.

IMG_9174.jpeg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngurdoto Mkoani Arusha tarehe 24 Novemba, 2023.

IMG_9175.jpeg
Rais wa Kenya Mhe. Dkt. William Ruto, akishiriki Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngurdoto Mkoani Arusha, tarehe 24 Novemba, 2023.

IMG_9176.jpeg
Waziri Mkuu wa Rwanda Mhe. Dr. Edouard Ngirente, akishiriki Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngurdoto Mkoani Arusha, tarehe 24 Novemba, 2023.
 
Back
Top Bottom