Rais Samia: Kiswahili ndiyo Lugha ya kutuunganisha Afrika, Tanzania tuko tayari kutoa Walimu na vifaa vya kufundishia kuja Comoro

Rais Samia: Kiswahili ndiyo Lugha ya kutuunganisha Afrika, Tanzania tuko tayari kutoa Walimu na vifaa vya kufundishia kuja Comoro

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Rais Samia amesema Kiswahili kina uwezo wa kuwaunganisha Waafrika na kupendekeza kitumike kama lugha ya mawasiliano, elimu na biashara katika nchi za Afrika, ikiwemo Comoro.

"Lugha pekee ya Kiafrika inayoweza kutuunganisha au kuunganisha watu wetu ni kiswahili, hivyo ilikujenga umoja nitumie fursa hii kupendekeza kwamba Kiswahili lugha ya mawasiliano, elimu na biashara kati yetu, ifundishwe mashuleni na kutambulika rasmi hapa Comoro."

Amesema Tanzania iko tayari kusaidia kwa kutoa walimu na vifaa vya kufundishia. Aidha, amesisitiza kuwa Kiswahili ni urithi wa pamoja na daraja la maendeleo baina ya mataifa ya Afrika.

"Tanzania iko tayari kusaidia kutoa walimu na vifaa vya kufundishia, tukumbuke kwamba Kiswahili ni urithi wetu wa pamoja na ni daraja la maendeleo baina yetu."
 
Kule kwa yule Dogo wa Bukinabe yeye yuko bize na ujenzi wa sgr kuunganisha nchi tatu, sisi sijui tuko wapi, ohh kumbe na sisi tunapeleka sgr Burundi na rwanda, lazima uchumi upande kuliko US
 
Back
Top Bottom