Rais Samia kagusa Watumishi kwa Mikopo ya Elimu nchini kuanzia Vyuo vya kawaida, Kati na Vyuo Vikuu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kurahisisha ugumu wa maisha Kwa watumishi.

Mnamo tarehe 14.3.2023 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ikishirikiana na benki ya NMB wameanzisha mfuko uitwao Elimu Loan. Mfuko huu utatoa mikopo kwa riba ya 9%, hii itakuwa ni maalum Kwa watumishi ambao mishahara yao inapitia benki hiyo.

Hapa mtumishi anaweza akapata mkopo kujiendeleza yeye, mweza wake au mtoto wake. Hii itanzia vyuo vya kawaida vinavyotoa elimu ya cheti, stashahada n.k.

Haya yote ni mapenzi aliyonayo Mheshimiwa Rais kwa watumishi wake na familia zao iliwapate elimu yenye riba nafuu.

Asante Mheshimiwa Rais wetu watumishi wanakupenda wanakushukuru. Nimpongeze Waziri wa Elimu Mhe. Prof. Mkenda, Naibu Waziri Mhe. QS Kipanga na Menejimenti ya Wizara ya Elimu kwa ubunifu huu ambao unaenda kukomboa watumishi.

WhatsApp Image 2023-03-16 at 20.54.27.jpeg
 
Watumishi wa umma wana raha na bahati kweli, hongera na pongezi kwa rais, sisi wafanyabiashara uchwara tunaumia kwelikweli, hatuna jinsi, hatuna tumaini, linapofanywa jambo tunaomba liwe linaangalia kote kote! Au pande zote!
 
Back
Top Bottom