Rais Samia, imulike Bandari ya Dar nchi inahujumiwa, kaweke Kambi pale Bandarini

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,598
3,644
Meli za kutoka Dubai kuja DSM huchukua siku 14, Mzigo ukifika Dar Es Salaam bandarini utakaa siku hata 20-28 ukisubiri kupakuliwa.

Meli ikitoka UK au China itatumia siku 28-30 kufika Dar, Mzigo ukifika hapo Bandarini unachukua siku 20-28 zingine kupakuliwa.

Gharama za Usafiri imebidi SHIPLINERS waziongeze kufidia muda mrefu wa kusubiri hapo Bandarini.

Sasa hivi Wafanyabiashara kutoka CONGO DR, RWANDA, MALAWI, ZAMBIA, UGANDA wameanza kukimbilia Bandari ya Mombasa kupitisha mizigo yao.

Mheshimiwa Rais Samia, ukicheka na nyani utavuna Mabua., wananchi vitu vitazidi kupanda bei bila sababu yoyote ya maana.

Nimekuwekea na VIDEO uisikilize kama ushahidi mwingine.

KAZI IENDELEE
 
Wewe ni kama umechanganyikiwa tu au una utapiamlo wa akili.

Unahitaji PhD kujua kuwa Rais ambae anahamasisha ufisadi katika Serikali yake hawezi tena wakati huohuo kupambana na ufisadi huo?

Yaani unataka Rais ahamasishe ufisadi na kupambana na ufisadi huo kwa wakati mmoja?WTF?!
 
Meli za kutoka Dubai kuja DSM huchukua siku 14, Mzigo ukifika Dar Es Salaam bandarini utakaa siku hata 20-28 ukisubiri kupakuliwa.

Meli ikitoka UK au China itatumia siku 28-30 kufika Dar, Mzigo ukifika hapo Bandarini unachukua siku 20-28 zingine kupakuliwa.

Gharama za Usafiri imebidi SHIPLINERS waziongeze kufidia muda mrefu wa kusubiri hapo Bandarini.

Sasa hivi Wafanyabiashara kutoka CONGO DR, RWANDA, MALAWI, ZAMBIA, UGANDA wameanza kukimbilia Bandari ya Mombasa kupitisha mizigo yao.

Mheshimiwa Rais Samia, ukicheka na nyani utavuna Mabua., wananchi vitu vitazidi kupanda bei bila sababu yoyote ya maana.

Nimekuwekea na VIDEO uisikilize kama ushahidi mwingine.
KAZI IENDELEE
Sasa hivi inaonekana vitengo vingi vya Serekali, Watumishi wanajifanyia wanavyotaka wao! Hawamuogopi Mama kabisa!

Tena kile kitendo cha yule Mama mmoja aliyejaribu kujitokeza mbele ya Raisi siku ile ya Sheria, na Rais akamkaataa kiaina basi ile ndiyo ikazidi kuwapa kichwa baadhi ya Watumishi wabadhirifu kufanya yao kwa kutumia Mwanvuli wa utumishi!! Nchi hii ngumu sana!!
 
Mkuu kwa Bandari nadhani hata angekutawala nani! Pale ni pagumu.
Kama kwa Mwendazake ambaye alikuwa mkali na akamweka mtu wa karibu yake aliyekuwa mkali lakini upigaji ulikuwa palepale sembuse Mama?
Hajapatikana kiongozi anayetumia akili tu. Hakuna kitu kinachoshindikana pale. Magufuli alikuwa anaongoza kwa style za zamani sana. Ni lazima angeshindwa. Samia yeye ni kama Kikwete. Bora liende. Nakuapia akipatikana kiongozi mzuri akija na mikakati ya kisayansi pale kila kitu kinanyooka.
 
Sasa hivi inaonekana vitengo vingi vya Serekali, Watumishi wanajifanyia wanavyotaka wao! Hawamuogopi Mama kabisa! Tena kile kitendo cha yule Mama mmoja aliyejaribu kujitokeza mbele ya Raisi siku ile ya Sheria, na Rais akamkaataa kiaina basi ile ndiyo ikazidi kuwapa kichwa baadhi ya Watumishi wabadhirifu kufanya yao kwa kutumia Mwanvuli wa utumishi!! Nchi hii ngumu sana!!
Haya nilitegema kabisa. Unajua Magufuli alikuwa mkali lakini hakuwa anatumia elimu na sayansi kwenye kuongoza. Matokeo yake ni kuwa watu walikuwa wanamwogopa mtu mmoja na siyo kuwajibika kwa sababu ya mfumo ulio mzuri. Kiongozi wa namna hii akiondoka ni lazima anaacha ombwe kubwa la uongozi, na watu wanaona kama wamepewa nafasi ya kupumua.
 
Samia hata akijitahidi kuonesha hataki utani hafananii na kiongozi alie serious, na vile nina wasiwasi nae, anaweza kwenda huko bandarini kukagua halafu wajanja bado wakaiba akiwepo, huyu Rais wetu kwakweli sijui namuonaje...
Just thinking aloud: unaweza kuwa mpango wa kuaminisha watu kuwa bandari ya Dar imeelemewa hivyo solution ni kujengwa bandari ya Bagamoyo. Tutafakari: Thread kama hizi zinazoweza kufuatiliwa na matamko kutoka kwa viongozi kuwa ''hata kwenye mitandao kelele zinapigwa kuwa bandari ya Dar imeshindwa kuhimili msongamano hivyo bila bandari ya Bagamoyo ni bure''
 
Back
Top Bottom