Mbunge Juliana Shonza Atolea Ufafanuzi Kuhusu Uwekezaji wa Bandari na Kampuni ya DP World

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
"Nataka tuwekane sawa maana tayari watu wameanza kupotosha na kazi ya Serikali ni kuelimisha wananchi, mjadala wa bandari umekuwa ni mkubwa sana kuliko Mijadala mingine yote na hii ni kwasababu kwa mara ya kwanza watanzania wameshuhudia mkataba mkubwa kama wa bandari ukipelekwa Bungeni" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Mkataba wa bandari siyo wa kwanza, Serikali imeshasaini Mikataba mingi lakini mkataba wa bandari ndiyo wa kwanza kupelekwa Bungeni. Huko nyuma Mikataba ilikuwa inasainiwa na Serikali na Mawaziri lakini kwasababu Rais Samia alisema atahakikisha Watanzania wanakuwa na Uhuru wa kujieleza atahakikisha anakuza Demokrasia ya wananchi kuhoji, kujieleza na kukosoa Serikali pale wanapoona Serikali haijafanya vizuri" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Sasa hivi bandari ya Dar es Salaam imetoa ajira 28,000 tu lakini mwekezaji akija zitaongezeka 71,000. Watu wanaogopa kununua magari maana anajua bandari litakaa siku 5 unasubiri mzigo wako lakini magari yakifika kuchukua mzigo na kuondoka ajira zitaongezeka maana magari yatakuwa mengi na vijana wengi watapata ajira" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Uwekezaji wa bandari utasaidia kukuza sekta ya usafirishaji, leo hii nchi yetu tunajenga Reli kubwa ya SGR na huku Kusini tunayo Reli ya TAZARA. Hizi Reli tunajenga siyo mapambo ya kupamba nchi lakini ili tusafirishe mizigo kwa wingi" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Serikali inajenga barabara lakini zinaharibika kila siku kwasababu mizigo ni mingi, tunajenga Reli tuwe na bandari kavu, hapa Songwe tumeanza kuomba Serikali itupatie bandari Kavu pale Pemba na Reli yetu ya TAZARA iboreshwe ili mizigo isafirishwe kwa wingi" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Wameenda mbali zaidi wakasena Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi wameenda wamehongwa, hakuna aliyehongwa. Sisi tumeenda India 🇮🇳 na Dubai tumelipwa na Bunge kwa stahiki za kibunge amelipa Spika Dkt. Tulia Ackson, hakuna Mbunge aliyepokea fedha za Mwarabu" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Sisi wabunge tulivyoenda Dubai tulisema tukamuambia Waziri Mbarawa jambo hili ninyi kama Serikali ucheleweshaji na mkwamo unatokana na nini? Kwasababu kama Tanzania 🇹🇿 tumechelewa sana kupata wawekezaji wakubwa kama DP World kwenye bandari zetu kwa mambo ambayo tumeyaona" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Mimi niwatoeni hofu, pamoja na hofu ambazo watanzania mmekuwa nazo, hofu hizi zimefanya Serikali imekuwa makini. Sisi tutawapa kwanza miaka ya matazamio maana kufunga ile mitambo mpaka kukamilika siyo suala la mwaka mmoja linaweza kuchukua miaka kadhaa wafunge mitambo ambayo wametuahidi, tunaweza kuwapa miaka 10 au 20 tuwaangalie kwanza" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Sasa hivi mapato ya bandarini tunaingiza Trilioni 7, DP World wakishafunga mitambo na kuanza kazi tutaingiza Trilioni 27. Katika miaka tutakayowapa wakifanya vizuri tutaendelea kuwaongeza miaka lakini siyo miaka 100" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Nipo hapa kuwapa ufafanuzi, Ndugu zangu hakuna bandari iliyouzwa, hakuna Rais wala Chama anayeweza kuuza bandari ya watanzania. Tunapozungumzia PPP, Rais anaposhawishi wawekezaji Tanzania haimaanishi kuuza, kama ni kuuzwa Nchi yote tungekuwa tumeshauzwa maana wawekezaji wapo kila kona Tanzania" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Kilichofanyika ni sisi kuingia makubaliano na mashirikiano, mkataba wa Mashirikiano na bandari bado, tulichopitisha Bungeni ni makubaliano ya Mashirikiano kati ya Tanzania na Dubai kwamba tutashirikiana kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na kiutamaduni " - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Leo tunasema Tanzania 🇹🇿 na China 🇨🇳 ni marafiki, kwasababu walisaini Mikataba ya makubaliano ndiyo inafanya kazi mpaka leo. Wabunge tumepitisha pale Bungeni ni makubaliano ya Mashirikiano ya kiuchumi na kisiasa kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai" -Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Kwa kuwa makubaliano tumeshayakamilisha kinachofuata kuna Mikataba 4 ndiyo itasema kuwa Tanzania 🇹🇿 na Dubai (TPA & DP World) kwamba watashirikiana kwenye mambo gani na DP World itaweka kiasi gani na Tanzania tutanufaika kiasi gani" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Wanasema tumewapa bandari kwa Miaka 100, nashukuru sana maana wapinzani wameanza kupishana. Lissu anasema kwenye makubaliano hakuna mahali ambako kumeonyesha kuwa tumetoa bandari kwa miaka 100. Wanasema njia ya mwongo ni fupi" Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Hakuna makubaliano ya kutoa bandari kwa miaka 100, mambo ya ukomo kwamba tutawapa bandari kwa miaka mingapi hayatasainiwa na Serikali ya Tanzania na Dubai, hapana! Itakuwa ni kati ya DP World na TPA watasaini na kukubaliana ukomo utakuwa ni wa miaka mingapi" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Haiwezekani, Chama Cha Mapinduzi siyo wajinga, yaani mwekezaji anakuja tunampa miaka 100, mwekezaji ndiyo anafika anapewa miaka 100? Rais Samia na Mwenyekiti wa CCM Taifa ametuhakikishia, Serikali haitaingia makubaliano ya kuwapa miaka 100. Kampuni inayokuja kuwekeza katika bandari ni DP World" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Serikali iliona vyema wabunge waende wajiridhishe kwasababu Rais Samia anataka mambo ya uwazi, anataka Mikataba isaidiwe Bungeni, akasema baadhi ya wabunge waende na mimi nilichaguliwa na Spika wa Bunge nikaenda India 🇮🇳 na wenzangu wakaenda kwenye nchi zingine ikiwepo Dubai" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe.

"Ukienda India 🇮🇳, DP World wamepewa eneo kubwa kama Wilaya ya Mbozi ili wawekeze na India eneo kubwa ni Jangwa. Tulitembea eneo moja baada ya jingine. DP World wamejenga Reli ya kwao, Treni za kwao, Mitambo ya kuzalisha Umeme ya kwao na Mitambo ya kupakia na kushusha mizigo Bandarini ya kwao. Shehena zinashushwa hapa Tanzania kwa siku tano DP World India wanashusha kwa masaa tu" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Niwaombe msikubali kudanganywa na kurubuniwa, Serikali ipo kazini na lengo lake ni kufanya uwekezaji" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

MAFANIKIO AMBAYO TANZANIA ITAPATA KWENYE UWEKEZAJI WA BANDARI

1. Sasa hivi bandari ya Dar es Salaam Serikali inakusanya Trilioni 7 lakini tukileta mwekezaji tutapata Trilioni 27

2. Sasa hivi bandari ya Dar es Salaam inapokea Meli 1569 lakini uwekezaji ukifanyika pale zitaingia Meli 2950 maana yake mapato yataongezeka

"Nani alikuwa anajua kuwa kwa miaka zaidi ya 20 bandari ya Dar es Salaam ilikuwa inaendeshwa na (Tanzania International Container Terminal Services (TICTS), na yenyewe ni Kampuni, siyo Tanzania tulikuwa tunaendesha bandari. Suala la kuweka mwekezaji kwenye bandari siyo suala jipya" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Sasa hivi nchi nyingi zimeacha kupitisha mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam kwasababu kuna ubabaishaji na ucheleweshaji wa mizigo. Ndiyo maana watu wanaingia kwenye bandari ya Mombasa na Beila. Sisi kama nchi tunapoteza mapato" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Sisi Sera yetu ni ya PPP (Public Private Partnership) yaani Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi. Serikali haiwezi ikafanya yenyewe ni lazima tushirikishe Sekta Binafsi hususani kwenye Miradi na Mashirika makubwa yenye sura ya kibiashara" - Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe.

 
Back
Top Bottom