Bandari ya Dar es Salaam ina changamoto za Mafanikio

fimbo ya mpera

Senior Member
Oct 1, 2014
101
79
BANDARI YA DSM NA CHANGAMOTO ZA MAFANIKIO
  • Ni baada ya ukamilishaji wa mradi wa DMGP, uimarishaji wa mifumo na utekelezaji wa maelekezo na matamanio ya Rais Dkt. Samia katika mapinduzi ya Bandari
  • Sasa meli zinamiminika kila siku, wateja wameongezeka, mapato juu, mfungamano wa ajira umeimarika
  • Imevutia uwekezaji wa makampuni makubwa ya kimataifa ikiwemo DP WORLD, COSCO, APM, na nyinginezo
Na. Shaibu Sufiani
Unaposikia Meli zimekaa foleni zinasubiri kuingia bandari ya Dar es salaam usilalamike, shangilia kwani huo ni Uchumi wa Taifa unaimarika

Unapopita kandoni mwa Bahari ya hindi ukaona meli 10 au zaidi zimepanga foleni zinasubiri kuingia mshukuru Mungu mwambie Alhamdullilah uwekezaji wa maboresho ya bandari ya Dar es salaam umelipa na sasa wateja wengi wameongezeka maradufu

IKO HIVI
Kama ambavyo wamiliki wa nyumba za kulala wageni wanavyojisikia pale vyumba vinapojaa na huku wateja wakiendelea kuulizia vyumba, au washabiki wa mpira wanapofurika uwanja wa mpira kushangilia timu yao hadi kukosa viti, ama waumini wa dini wanapokwenda katika nyumba za ibada na kukuta nafasi zimejaa na ili wahudumiwe ni lazima kwanza wahudumiwe wenzao wenzao ndipo wao pia wahudumiwe,

Hivyo ndivyo ilivyo Babdari ya Dar es salaam kwa sasa, kwa miezi kadhaa mfululizo kuanzia mwezi wa 10 hadi hii Januri, MAGATI yote 12 ya Bandari hiyo kila siku kila saa yanakuwa yamejaa meli zikishusha na kupakia aina mbambaku za shehena kama vile Magari, Mizigo mchanganyiko, mbolea, makasha(Contena), Mafuta nakadharika, huku idadi kubwa ya meli ikiendelea kusubiri wenzao wamalize kushusha mizigo ili wao pia waingia

Inawezekana mtu wa kawaida akaona ni makusudi, au akaona kuna uzembe au kuna njama au namna yoyote navyoweza kuhisi yeye, lakini ukweli ni kwamba hakuna uwekezaji usiokuwa na matunda Chanya

Uwekezaji wa Tanzania katika uboreshaji wa Badari ya Dar kupitia mradi wa DMGP ulikuwa na lengo mahsusi kuhusiana na kuboresha miundombinu ili bandari iweze kuleta tija zaidi kwa Taifa katika kutoa huduma za kibandari

Fuatana nami hapa ili kufahamu kila kitu kuhusiana na uwekezaji huo mkubwa kuwahi kufanyika nchini

HALI YA BANDARI ZETU ZIKOJE
DAR PORT A-Z_page-0003.jpg

Tunaarifiwa kuwa kabla ya mwaka 2015 hali ya bandari zetu hasa bandari tegemeo ya Dar es salaam haikuwa na uwezo mkubwa wa kiushindani ambapo meli zilizokuwa zinakuja ni ndogo kwa sababu ya kina huku Meli za Magari zikiwa zinahudumiwa katika eneo la mizigo mchanganyiko (General Cargo), na hazikuwa nyingi, ambapo pia hakukuwa na mpangilio wa maeneo ya kufanyia kazi kulingana na aina za mizigo huku Vifaai vya kuhudumia meli vikiwa duni, Magati yalikuwa na kina kifupi (chini ya mita 9) kiasi cha makusanyo ya mapato kutokuwa makubwa kutokana na uchache wa shehena iliyokuwa inahudumiwa kulingana na soko, Kwa ujumla UFANISI ulikuwa DUNI,

NINI KILIFANYIKA
Kutokana nachangamoto hizo, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini (TPA) iliamua kutafuta fedha ili kufanya maboresho ya Bandari (DMGP-mpango ulioanza kutafuta fedha miaka ya 2011 hadi 2016 uliposainiwa mkataba wa maboresho ya bandari)

DMGP NI NINI

Dar es Salaam Maritime Gateway Project (Mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es salaam)
Uchambuzi, upembuzi na utafiti 2010 kwa serikali kutafuta pesa hadi mkataba uliposainiwa na mradi kuanza kazi 2016/2017

DAR PORT A-Z_page-0008.jpg

MAENEO YA MRADI WA MABORESHO YA BANDARI YA DSM

UJENZI WA MAGATI

- Gati jipya la Magari (RO-RO) na Yard yake limejengwa ukubwa wa Gati ni mita 300 Ukubwa wa YARD ni mita za mraba 72,000 lenye uwezo wa kutunza magari zaidi ya 6000 kwa wakati mmoja

2.UIMARISHWAJI GATI ZILIZOKUWEPO
Katika magati yaliyokuwepo,
Magati 7 yameimarishwa, Gati namba 1 hadi 7 ziliimarishwa kwa kuongezewa kingo ya urefu wa mita 15 kuelekea baharini, Kumewekwa vikingio vya meli vya kisasa (Fenda), Katika kila Gati zilizoimarishwa maeneo ya kuwekea shehena yameboreshwa, Mifumo ya kuzimia moto,Hydraut,Bankering na taa(Tower lights zimewekwa kuwezesha huduma kutolewa sa 24

NB; gati namba 5 hadi namba 7 zimeimarishiwa yadi yake ya kutunza shehena za makasha zinazoweza kutunza makasha zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja

3 . UONGEZAJI WA KINA – DRAFTING
Kina cha Bahari kilikuwa kidogo kiasi cha meli kubwa au zilizobeba mzigo mkubwa kushindwa kuingia, hivyo mradi ulifanikisha:-
  • Uchimbaji wa kina cha Bahari umefanyika kufikia mita 14.5 kutoka chini ya mita 9 za awali kwenye maeneo tofauti tofauti,
  • Mwanzoni meli kubwa zenye tani kuanzia 30,000 zilibidi kwanza zikapunguze mzigo gati namba 7 ndio ziweze Kwenda gati nyinginezo
4. MLANGO WA KUGEUZIA MELI
Aidha eneo la kuingilia meli (Entrance channel) halikuwa kubwa hivyo kuleta ugumu wa upitishaji wa meli kuingia na kutoka bandarini ndipo mradi ukafanikisha maboresho pia ya upanuzi wa mlango wa kuingiza meli na Kuboresha eneo la kugeuza meli – Turning Base

MATOKEO YA MABORESHO
Kukamilika kwa maboresho haya kumeleta matokoe makubwa ambayo kwa kiasi kingine matokeo hayo yanageuka kuwa changamoto. Hata hivyo changamoto hizi za kimafanikio hazipaswi kuwafanya wadau wa maendeleo na wadau watumiaji wa bandari kurudi nyuma na badala yake kusonga mbele kutafuta suluhu bora zaidi katika kufanikisha.
DAR PORT A-Z_page-0013.jpg

Miongoni mwa matokeo ya moja kwa moja ya maboresho ya mradi wa DMGP ni pamoja na

KUONGEZEKA KWA SHEHENA

Tunaarifiwa kuwa shehena zinazoshuka Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka kutoka chini ta Tani milioni 13 mwaka 2016 hadi zaidi ya tani milioni 21 kwa mwaka 2022/23

Shehena za Shehena za Makasha zimepanda hdi kufikia wastani wa makasha 90,000 kwa mwezi tofauti na awali

Huku Shehena za magari zimeongezeka hadi kufikia wastani wa gari 200,000 kwa mwaka

DAR PORT A-Z_page-0018.jpg

KUONGEZEKA KWA MAPATO TPA NA TRA
Taarifa zinaonyesha kuwa Makusanyo ya Bandari (Port Charges), yameongezeka hadi kufikia zaidi ya bilioni 106 kila mwezi sawa na wastani wa zaidi ya Trilioni 1.2 kwa mwaka

Vile vile Makusanyo ya Kodi yanayokusanywa na TRA kama forodha kupitia Bandarini yamepanda kufikia 40% ya makusanyo yote ya kila mwezi ya TRA

Maana yake nini, maana yake ni kwamba kwa kadri meli zinavyozidi kuwa nyingi, ndivyo makusanyo yanazidi kuongezeka

KUONGEZEKA KWA IDADI YA MELI
Idadi ya meli zinazoingia Bandarini Dar zimeongezeka maradufu kufikia wastani wa meli 90 kwa mwezi kutoka chini ya meli 60 huko nyuma ambapo kuna nyakati zimewahi kufika zaidi meli 100 katika kipindi cha mwezi mmoja

ONGEZEKO LA WATUMIAJI WA BANDARI
Maboresho pia yamepelekea kuongezeka kwa watumiaji wapya wa bandari mbapo nchi kama Zimbawe zimeongeza kuitumia bandari ya DSM hasa katika usafirishaji wa Magari sambamba na kampuni kadhaa kubwa za meli kuanzisha safari zake kuja Dar es salaam

ONGEZEKO LA AJIRA/FURSA
Maboresho yameongeza mnyororo wa thamani ambapo katika ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ambapo inakadiriwa zaidi yamakampuni 8000 yanatoa huduma mbalimbali bandarini, Maelfu ya madereva wa malori wamepata ajira, wenye malori nao wameongezeka na wameongeza vipato

Aidha wauzaji bidhaa na huduma kama mama lishe, migahawa, petrol stations, wauza vipuri, wazabuni na wengine wengi wamepata ajira katika bandari ya DSM.

Ni kwa sababu ya maboresho haya ndipo leo tunasikia kuna meli 36 zipo nje zinasubiri kuingia zikingojea meli zilizotangulia katika Gati 12 zilizopo hivi sasa zimalize kuhudumiwa nazo ziingie.

Ni vyema na haki kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna bora anavyoitazama sekta ya uchukuzi hasa eneo la bandari katika jicho pan ana bora ambapo hakuna namna hivi sasa uwekezaji mkubwa wa upanuzi ama uongezaji wa magati unahitajika.
DAR PORT A-Z_page-0001.jpg

DAR PORT A-Z_page-0022.jpg

Hesabu ya kawaida inaonyesha kuwa kama bandari yote ya Dar ina jumla ya magati 12 (Ukijumlisha na magati ya kushushia mafuta), nak ama kwa wakati mmoja meli zinazoingia nchini kutaka kuhudumiwa ni zaidi ya meli 40, hivyo kwa kila wakati lazima kuwepo na meli zaidi ya 20 zikisubiri wenzake wamalize,

Hii inatokana na ukweli kuwa meli moja ili imalize kuhudumiwa kwa kushuisha na kupandisha mizigo melini huchukua wastani wa siku moja hadi tano kutegemea na aina ya shehena iliyobeba

Tuendelee kuelimishana na kufahamishana juu ya umuhimu wa uwekezaji mkubwa unaohitajika kufanyika katika Bandari zetu huku tukirejea maneno yanayosema Kuongezeka kwa Meli nchini sio dhambi ni neema.

Shaibu Sufiani

Tuwasiliane :- shaibusufiani@gmail.com
 
Ukisoma hapa

Dar es Salaam Maritime Gateway Project (Mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es salaam) Uchambuzi, upembuzi na utafiti 2010 kwa serikali kutafuta pesa hadi mkataba uliposainiwa na mradi kuanza kazi 2016/2017

Mipango iliwekwa wakati wa JK na ilianza kutekelezwa wakati wa Magu

Yeye mama alichotuletea hapo bandarini ni DP world ambao mpaka sasa hatujui watatuletea faida au hasara.
 
Hu Uzi ukiusoma kwa umakini sidhani kama utasikiliza kelele za wapotoshaji kuhusu bandari Dar. Nyumbu kwenye huu Uzi watapita kama upepo
 
Kwa hiyo faida au hasara inapimwa kwa time interval gani baada ya kuingiwa kwa mkataba na utekelezaji wake , wakuu ebu mtusaidie hapa maana sio unalala tu huku jf alafu kumbe upo shalo
 
fimbo ya mpera ,

Kazi ya Bandari ni kupakia na kupakua mizigo kwenye meli.

Kama kuna MSONGAMANO wa meli maana yake bandari haina vifaa vya kutosha, au ina wafanyakazi wapambe.

Bandari kama watoa huduma wanatakiwa wawafikirie WATEJA wao. Kama kuna msongamano bandarini sidhani kama wateja watakuwa wanafurahishwa na hali hiyo.

Makala inayosifia na kushangilia MSONGAMANO ktk bandari yetu sio ya kizalendo na haiko kwa maslahi ya taifa letu.

Cc Nguruvi3
 
Hu Uzi ukiusoma kwa umakini sidhani kama utasikiliza kelele za wapotoshaji kuhusu bandari Dar. Nyumbu kwenye huu Uzi watapita kama upepo
 
Ukisoma hapa

Dar es Salaam Maritime Gateway Project (Mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es salaam) Uchambuzi, upembuzi na utafiti 2010 kwa serikali kutafuta pesa hadi mkataba uliposainiwa na mradi kuanza kazi 2016/2017

Mipango iliwekwa wakati wa JK na ilianza kutekelezwa wakati wa Magu

Yeye mama alichotuletea hapo bandarini ni DP world ambao mpaka sasa hatujui watatuletea faida au hasara.
Jenga hoja yako sawa sawa
 
fimbo ya mpera ,

Kazi ya Bandari ni kupakia na kupakua mizigo kwenye meli.

Kama kuna MSONGAMANO wa meli maana yake bandari haina vifaa vya kutosha, au ina wafanyakazi wapambe.

Bandari kama watoa huduma wanatakiwa wawafikirie WATEJA wao. Kama kuna msongamano bandarini sidhani kama wateja watakuwa wanafurahishwa na hali hiyo.

Makala inayosifia na kushangilia MSONGAMANO ktk bandari yetu sio ya kizalendo na haiko kwa maslahi ya taifa letu.

Cc Nguruvi3
Makala haijaonyesha Bandari kuacha kufanya hiyo shughuli mbona?. Au mimi sijaelewa
 
BANDARI YA DSM NA CHANGAMOTO ZA MAFANIKIO
  • Ni baada ya ukamilishaji wa mradi wa DMGP, uimarishaji wa mifumo na utekelezaji wa maelekezo na matamanio ya Rais Dkt. Samia katika mapinduzi ya Bandari
  • Sasa meli zinamiminika kila siku, wateja wameongezeka, mapato juu, mfungamano wa ajira umeimarika
  • Imevut
Baada ya maboresho hayo yalio asisiwa na watanzania na kutekelezwa na watanzania , je kweli hatua inayo fuata haiwezi kufanywa na watanzania Hadi hizo kampuni zifanye hiyo kazi, au ndio kuwezeshana kununua nyumba dubai na masaki za matrillioni ya madafu
 
..makala imesema kuna MSONGAMANO bandarini.

..maana yake upakuaji na upakiaji wa mizigo haufanyiki kwa wakati na kwa ufanisi.

..binafsi sijawahi kusikia MTEJA anayefurahia msongamano na ucheleweshaji wa huduma.

..Makala kama hizi haziko kwa maslahi ya bandari yetu, na si za kizalendo.
 
Ukisoma hapa

Dar es Salaam Maritime Gateway Project (Mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es salaam) Uchambuzi, upembuzi na utafiti 2010 kwa serikali kutafuta pesa hadi mkataba uliposainiwa na mradi kuanza kazi 2016/2017

Mipango iliwekwa wakati wa JK na ilianza kutekelezwa wakati wa Magu

Yeye mama alichotuletea hapo bandarini ni DP world ambao mpaka sasa hatujui watatuletea faida au hasara.
Lugha nyepesi kutumika na kueleweka ni kuwa Bandari yetu imefanikiwa kukuwa na kwa mantiki hiyo ni lazima uwekezaji uongezeke
 
Back
Top Bottom