Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,986
- 144,313
Muda mfupi uliopita kupitia kipindi cha "Ijue BOT" kinachorushwa na Azam tv, nimemsikia Afisa Mwandamizi wa BOT, Bwana Deogratias Mnyamani akitoa maelezo kuhusu Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake ya mwaka 2019. Katika maelezo yake akihojwa na Mtangazi wa kipindi hicho, Bwana Mnyamani ameeleza mambo kadhaa ambayo naamini watu wengi hawayajui kuanzia watoa huduma mpaka walaji.
Kwa mfano, Bwana Mnyamani amesema kutoa kadi ya benki kwa mtoa huduma kama dhamana ni kosa kwa mkopeshaji na mkopaji. Swali ni je, watu wangapi wanafahamu hivi? Baadhi ya watoa huduma(Wakopeshaji) wanaweza kuwa wanajua, ila Walaji kwa maana ya Wakopijaji, wanajua kutoa kadi ni kosa kisheria?
Vile vile, Afisa huyu ameeleza adhabu kwa wanaofanya biashara ya kukopesha bila kuwa na leseni ambapo amesema adhabu ni faini kati ya shilingi milioni 20 mpaka milioni 100 au kifungo cha miaka 2 mpaka 5 jela au vyote kwa pamoja. Swali ni je, watu wanaofanya hii biashara kienyeji wanafahamu kuhusu adhabu hizi?
Kwa kifupi, Bwana Deogratias kaongea mengi kuhusu hii sheria na kanuni zake na amesema walikuwa kwenye kipindi cha kutoa elimu kuhusu hii sheria na kanuni zake na sasa wanajipanga kuanza kuisimamia.
Ukweli ni kwamba, watu wengi wanafahamu uwepo wa hii sheria, lakini kama ilivyo kwa sheria zingine, wengi hawajui nini kimo katika hii sheria na kanuni zake na zaidi watu wengi wanaona hii sheria ipo tu lakini serikali haiisimamii na ndio maana inapuuzwa sana humu mitaani kwa watu kufanya hii biashara pasipo kuwa na leseni, huku wenye leseni, wakiifanya kwa kupuuza hii sheria ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019.
Hivyo, wakati serikali kupitia BOT wakijipanga kuanza kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa sheria hii kama alivyosema Afisa huyu wa BOT, nashauri BOT watoe matangaza kabla ya taarifa ya habari kwenye television na redio ili watu watambue kuwa ile "grace period" imepita na sasa utekelezaji unaanza. Mbali na kutoa matangaza kwenye vyombo vya habari, pia watumie mitandao ya kijamii kueleza umma kuhusu hii sheria na kukumbusha umma kuwa sasa usimamizi na utekelezaji wa hii sheria kwa vitendo uko mbiona kuanza.
Pia, kwenye matangazo haya, watamke adhabu anazoweza kupata mtu kwa kuvunja hii sheria na kanuni zake. Hii itasaidia ku-create awareness kwa umma na kufanya watu waone serikali sasa iko serious kuhusu hii sheria na itsaidia sana kupunguza manyanyaso wanayopata wananchi hasa kutoka kwa wale wanaofanya hii biashara pasiokuwa na leseni, na wale wenye leseni kuzingatia mashariti ya leseni walizopewa.