Nani mwenye ushahidi au mfano wa BOT kuchukua hatua kwa watu binafsi na Taasisi zinazoto mkopo bila kuzingatia sheria ya huduma ndogo xa fedha?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,018
144,377
HIili swala la mikopo uumiza mitaani na na kwa njia ya online, limegeuka kilio na maumivu kwa watu wengi na ushahidi ni kuongezeka kwa nyuzi(thread) kuhusu mikopo umiza hapa hspa JamiiForums.

Malalamiko haya hayajaanza leo, jana wala juzi, bali ni ya muda mrefu na bahati nzuri serikali ikaja na sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019 ambapo Benki Kuu ya Tanzania(BOT) ndio wenye jukumu la kusimamia hiyo sheria na pia kutoa elimu kwa umma kama sikosei.

Hata hivyo, mikopo hii inayotolewa kinyume na sheria, imeendelea kutolewa na watu binafsi na baadhi ya. Taasisi kama vile hii sheria haipo kabisa na hii inatupa ujumbe kuwa waliopewa dhamana ya kusimamia hii sheria wameamua kuzembea au kazi imewashinda.

Leo hii naomba kuuliza ni nani humu amewahi kuona. au kusikia. BOT wamechukua hatua kwa watu au taasidi zinazofanya hii biashara pasipo kufuata sheria.

BOT, mbali na kutumia vipind vya television kuelezea kuhusu hii sheria na kutoa press release kwenye website yao kuonya kuhusu kufanya biashara ya kukopesha pasipo kuwa na leseni, nini kingine wanafanya kusimamia hii sheria?

Au BOT mna masilhahi na wavunja sherial?

Mfano wa nyuzi (thread) za malalamiko za hivi karibuni ni hizi:

Mimi sijawahi kuona wala kuambiwa kua flani kachukuliwa hatua kwasababu ya ukopeshaji pesa,kisa hakua anafuata sheria na taratibu zilizowekwa,badala yake naona watu wanaanzisha tu ofisi.
Hadi mkuu umeleta uzi leo,ujue kuna wadada na wamama siku ya leo,wapo kuzisaka pesa za kausha damu,wakalipe mikopo.
Njia wanazotumia kutafuta pesa ili wakalipe mikopo,nyingine ni halali na nyingine si halali,hivyo kuleta matatizo kwenye jamii kwa wale ambao huzitafuta kivyovyote bila ya uhalali.
 
Natamani nimshauri Raisi avunje kabisa uongizi wa BOT na wengine wanaopaswa kusimamia hii sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019.

Hawa watu sijui kazi yao ni kupiga suti na kukaa kwenye viyoyozi maofisini tu?
 
Malalamiko haya hayajaanza leo, jana wala juzi, bali ni ya muda mrefu na bahati nzuri serikali ikaja na sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019
Mkuu hao jamaa wanakopesha kwa masharti nafuu ila riba zao ndio nimeambiwa ni KUBWA. Watu wanaenda kukopa huko kwa hiari ili wapate fedha kwa wakati. So gharama wanayoingia ni kwa ajili ya KUPATA FEDHA KWA HARAKA. ambapo kwenye taasisi zilizosajiliwa huwezi kupata kwa haraka.

Walalamikaji wengi ni wale WASIOLIPA, wanatafuta Huruma ya Jamii ili wasilipe. Na hao huwa wanalalamikia hata BANK,SONGESHA, NIWEZESHE, VICCOBA na pia ndio wale ambao hata wakikopeshwa na Ndugu zao basi UNDUGU unaisha. hawataki kukubali matokeo ya Maamuzi waliyofanya(UWAJIBIKAJI).

BOT sijawai sikia wamewashughulikia hao Kausha damu. Na sheria kama inawataka kufanya hivyo basi WAWAJIBIKE.
 
Mimi nafikili kukopesha sio tatizo, isipokua serkali isimamie viwango vya riba kutokana na muda mkopo unaotolewa.
BOT waunde kamati, wachunguze vikampuni vyoote vinatoa mikopo kama vimekidhi vigezo na pia wafuatilie riba wanazowatoza wateja wao kutoka na muda wa huo mkopo kwenye marejesho ya mteja wao.
Mimi naamini wana viwango vyao vya riba kisheria, hivyo ni kuwakagua kwa kuangalia asilimia wanazo watoza wateja wao na wateja pia waeleimishwe kwamba wasikubali kupokea mkopo kama riba itazidi asilimia fulani, au mteja atoe taarifa iwapo ataona anatozwa asilimia nyingi tofauti na sheria inavyotaka.
 
Mkuu hao jamaa wanakopesha kwa masharti nafuu ila riba zao ndio nimeambiwa ni KUBWA. Watu wanaenda kukopa huko kwa hiari ili wapate fedha kwa wakati. So gharama wanayoingia ni kwa ajili ya KUPATA FEDHA KWA HARAKA. ambapo kwenye taasisi zilizosajiliwa huwezi kupata kwa haraka.

Malalamiko mengi unayosema watu wanalalamika, ukiyatazama ni ya wale WAKOPESHWAJI(WALIOKOPWA).

Inshort, Walalamikaji wengi ni wale WASIOLIPA, wanatafuta Huruma ya Jamii ili wasilipe. Na hao huwa wanalalamikia hata BANK,SONGESHA na pia ndio wale ambao hata wakikopeshwa na Ndugu zao basi UNDUGU unaisha, hawataki kulipa.

BOT sijawai sikia wamewashughulikia hao Kausha damu. Na sheria kama inawataka kufanya hivyo basi WAWAJIBIKE.
Soma hizo thread hapo juu kwenye huu uzi labda utaelewa concern yangu.
 
Mimi nafikili kukopesha sio tatizo, isipokua serkali isimamie viwango vya riba kutokana na muda mkopo unaotolewa.
BOT waunde kamati, wachunguze vikampuni vyoote vinatoa mikopo kama vimekidhi vigezo na pia wafuatilie riba wanazowatoza wateja wao kutoka na muda wa huo mkopo kwenye marejesho ya mteja wao.
Mimi naamini wana viwango vyao vya riba kisheria, hivyo ni kuwakagua kwa kuangalia asilimia wanazo watoza wateja wao na wateja pia waeleimishwe kwamba wasikubali kupokea mkopo kama riba itazidi asilimia fulani, au mteja atoe taarifa iwapo ataona anatozwa asilimia nyingi tofauti na sheria inavyotaka.
Labda tumuombe Makonda aingilie kati maana ndio anasikilizwa nchi nzima kwa sasa. Anachoongea nchi nzima wanakijadili.

Tumuombe Makonda amvae Waziri wa Fedha na viongozi wa BOT na bila shaka kilio kitafika kwa Raisi na hatua zitachukuliwa maana hii nchi sasa ndio inavyoenda.
 
Yaani ukiwaona ni watu walaini sana ni kama hawaishi pamoja nasi,wana siri gani mpaka watengwe kwenye makazi yetu? Sijawahi waona wakija kwenye viwanja vyetu kujenga zaidu ya kusikia kota za benk.
 
Natamani nimshauri Raisi avunje kabisa uongizi wa BOT na wengine wanaopaswa kusimamia hii sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019.

Hawa watu sijui kazi yao ni kupiga suti na kukaa kwenye viyoyozi maofisini tu?
Kuvunja BOT kunaweza kukubekifaya wewe mvunjaji, nafasi kuu haiendi kwa mtu yeyote eti mradi ni mtanzania, lazima awe wa karibu.
 
Labda tumuombe Makonda aingilie kati maana ndio anasikilizwa nchi nzima kwa sasa.

Tumuombe Makonda amvae Waziri wa Fedha na viongozi wa BOT na bila shaka kilio kitafika kwa Raisi na hatua zitachukuliwa maana hii nchi sasa ndio inavyoenda.
Kweli..mkuu.
mimi natamani watu waelimishwe kuhusu viwango vya riba. Yaani iwe hata ukimkopa lafikiako uwe unajua kabisa kua nikikopa laki moja, basi riba yake isizidi sh.elf5 kwa mwezi.kutokana na asilimia inayopangwa na serkali kisheria. Naamini watu hawata umizwa hivyo.
Usikute kunawatu wanakopa laki wanaambiwa warudishe laki na elf40 na wanakubari kwasababu tu kakwama.
 
Back
Top Bottom