Rais Samia: Chuo cha Diplomasia sasa kitaitwa Chuo cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988

IMG-20230930-WA0294.jpg

View: https://www.youtube.com/watch?v=Y8ALXkIaiow

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa shughuli ya Uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Dkt. Salim Ahmed Salim, leo Septemba 30, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Maktaba hiyo ya Dk. Salim ambaye ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa aliyekuwa Katibu Mkuu wa nane wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) Mwaka 1989 hadi 2001 itajumuisha video, picha, hotuba na machapisho.

Lengo la kuanzishwa kwa maktaba hiyo, ni kutoa uelewa zaidi wa safari na mchango wa Dkt. Salim ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu na katika kuitumikia jamii.

Dkt. Salim amewahi kuwa Balozi wa Misri nafasi ambayo aliitumikia kwa muda wa mwaka mmoja kati ya Mwaka 1964 na 1965 kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini India.
photo_2023-09-30_08-55-02.jpg

Endelea kufuatilia kupata updates ya kinachoendelea ukumbini...

17204068_0-82-1600-901.jpeg

Dk Salim Ahmed Salim (kulia) akiwa na Joseph Sinde Warioba aliyewahi pia kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. (Picha: Maktaba ya Salim Ahmed Salim).

17204090_0-0-2297-1536.jpeg

Dk Salim Ahmed Salim (kushoto) akiwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
(Picha: Maktaba ya Salim Ahmed Salim).

Wageni wengine ambao wameshawasili ukumbi ni Rais Mstaafu Jayaka Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Ahmed Salim Mtoto wa Dkt. Salim na Mwakilishi wa Familia naye ni mmoja wa watakaoshiriki kwa ukaribu katika tukio hili.

Waziri January Makamba
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ametoa utambulisho wa wageni maalum waliopo katika shughuli hii na usema:

“Wizara ya Mambo ya Nje tunatambua mchango wa Dkt. Salim ni mkubwa na tunathamini sana, ameshiriki kwenye mambo mengi ndani na nje ya Nchi.

“Tunaamini Tovuti hii itakuwa hazina kubwa kwa kizazi cha sasa na cha baadaye. Kuhifadhi kumbukumbu ni jambo la muhimu na tunajifunzanidhamu ya kurekodi historia.

"Kuna barua ambayo nilimuandikia Dkt. Salim miaka 20 iliyopita nikiwa bado nina nywele, sikutegemea kama atahifadhi barua hiyo, inaonesha jinsi alivyokuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu."
IMG-20230930-WA0310.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Ahmed Salim mtoto wa kiume wa Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim, wakifuatilia kwa makini video fupi ya kumbukumbu mbalimbali (hazionekani pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.

IMG-20230930-WA0304.jpg

IMG-20230930-WA0308.jpg

Sehemu ya wanafamilia ya Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za kiongozi huyo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.

Mjadala
Mazungumzo kuhusu Dkt. Salim Ahmed Salim kulingana na nyadhifa mbalimbali alizozitumikia yatafanyika kwa kuongozwa na Moderator Saida Yhya-Othuman:
IMG-20230930-WA0309.jpg

Mwezeshaji wa mjadala juu ya kumbukumbu ya Dkt. Salim Ahmed Salim, Profesa Saida Yahya Othman akiongoza mjadala uliochangiwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Joseph Warioba, Balozi Christopher Liundi na Balozi Amina Salum Ali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.

Nafasi: Uwaziri Mkuu
Mzungumzaji: Joseph Warioba (Waziri Mkuu Mstaafu)

Nilimfahamu Dkt. Salim Mwaka 1964 alipokuwa Balozi wetu pale Cairo, baadaye tulifanya kazi pamoja na mwelekeo wetu ulikuwa ukifanana.

Dkt. Salim ni Mtanzania, ikitokea changamoto ya Pemba na Unguja atalitazama kwa Utaifa, hivyohivyo ikitokea kwa Bara na Visiwani.

Anapenda sana kusoma na kujifunza, akiwa na uhakika wa jambo atasema kwa ufasaha bila kumfikiria mtu.

Mwalimu Nyerere alipomteua Dkt. Salimu kuna watu walipinga, waliami amekaa nje muda mrefu hivyo hatakuwa anajua changamoto za Watanzania, lakini aliwashangaza kwa kuwa na utendaji mzuri.

Nafasi: Mwanasiasa na Pan Africanist
Mzungumzaji: Christopher Liundi (Balozi Mstaafu)

“Dkt. Salim kawaida yake tulipokuwa tukienda naye kwenye mikutano alikuwa na nguvu sana, aliandaa notes zake mwenyewe wakati wa mkutano na alishirikiana na watu wengi.

Alikuwa na uwezo wa Lugha, alipokuwa katika majadiliano alijiona kama Samaki ndani ya maji, niwasisitize ukipata nafasi ya kujifunza lugha jifunze.

Dkt. Salim alipigania Wanawake waingie katika mazungumzo ya migogoro tulipokuwa Darfur (Sudan)

Vijana waitumie Tovuti ya Dkt. Salim itakuwa na faida kubwa kwao, iwe sehemu ya urithi wa Bara la Afrika, pia nitoe ushauri kwa Serikali kwa kuwa kuna taarifa nyingi zipo kwenye Vyombo vya Habari basi iwezekane kukusanywa kwa ajili ya kutumika kwenye makavazi ili ifaidishe watu wengi.

Nafasi: Mshauri
Mzungumzaji: Balozi Amina Salum Ali

Mungu amempa Dkt. Salim kipaji cha uvumilivu na kuna masomo mengi kutoka kwake, hata alpochafuliwa hakutaka kujiingiza kwenye siasa za chuki na visasi.

Hakutaka kususa na alishiriki kwenye matukio yote ya Kitaifa, alijitoa.

Viongozi wa Kiafrika wengi tuna nyongo lakini kwake ni tofauti, hata mkikwazana anaweza kujitoa kwako.

Ukaribisho wa Rais
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene anamkaribisha Rais Samia kuzungumza.
IMG-20230930-WA0301.jpg

IMG-20230930-WA0303.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.

Rais Samia
Tovuti hii inatoa fursa kwa watu mbalimbali na inaonesha historia ya Bara la Afrika, nimeipitia na kubaini kuwa kwa mara ya kwanza tutakuwa na tovuti ya kipekee inayoakisi taarifa za Dkt. Salim.

Mfano nimesikiliza kwa umakini mahojiano aliyoyafanya Septemba 16, 1989 kwenye Chuo cha Diplomasia Dar es Salamaa ikiwa ni siku tatu kabla ya kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU.

Pia nimepitia barua na mawasiliano ya kimaandishi yaliyoonesha nafasi yake ya kushauri na kuimarisha jitihada za ukombozi.

Anatufundisha juu ya uadilifu, unyenyekevu na uzalendo, kwa mradi ulivyo inaonekana Dkt. Salim alijipanga mapema.

Niwapongezea Familia kwa jambo mlilolianza, nimefarijika kusikia kuwa Tovuti hii itakuwa endelevu na itakuwa inaongezewa taarifa, pia itafikiwa bila gharama.

Katika nyanja ya Kidiplomasia aliwakilisha vizuri Taifa letu akiwa katika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa Balozi.

Nakumbuka wakati anatangazwa kuwa Waziri Mkuu Wa Tanzania, Mwaka 1984 Nchi ilikuwa na changamoto ya uchumi, kuaminiwa na kupewa nafasi nyeti kama ya Waziri Mkuu katika kipindi kigumu ilionesha uimara wake katika kuchapa kazi.

Alitazama changamoto kama fursa, kupitia Wizara ya Ulinzi aliweka mkazo katika kuitumikia Nchi, jitihada hizo ziliongeza bidii katika kulitumikia Taifa letu.

Mliofuatilia uongozi wake OAU mtakubaliana na mimi mchango wake alioutoa, niwasii viongozi wenzangu kuwa Tovuti tunayozindua leo ina manufaa katika historia.

Tusichome kumbukumbu zinaweza kutusaidia.

Dkt. Salim alikuwa akithamini muda, akikuita ofisini ukichelewa dakika 5, ukifika anaanza kukupa elimu ya umuhimu wa muda.

Kutokana na Mchango wake katika Diplomasia, kile Chuo cha Diplomasia sasa rasmi kitafahamika kwa jina la Dkt. Salim Ahmed Salim.
IMG-20230930-WA0292.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa shughuli ya Uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Dkt. Salim Ahmed Salim, leo Septemba 30, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Maktaba hiyo ya Dk. Salim ambaye ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa aliyekuwa Katibu Mkuu wa nane wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) Mwaka 1989 hadi 2001 itajumuisha video, picha, hotuba na machapisho.

Lengo la kuanzishwa kwa maktaba hiyo, ni kutoa uelewa zaidi wa safari na mchango wa Dkt. Salim ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu na katika kuitumikia jamii.

Dkt. Salim amewahi kuwa Balozi wa Misri nafasi ambayo aliitumikia kwa muda wa mwaka mmoja kati ya mwaka 1964 na 1965 kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini India.
View attachment 2766971
Endelea kufuatilia kupata updates ya kinachoendelea ukumbini...

View attachment 2766974
Dk Salim Ahmed Salim (kulia) akiwa na Joseph Sinde Warioba aliyewahi pia kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. (Picha: Maktaba ya Salim Ahmed Salim).

View attachment 2766975
Dk Salim Ahmed Salim (kushoto) akiwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
(Picha: Maktaba ya Salim Ahmed Salim).

Rais Samia anatarajiwa kuwasili saa tano asubuhi.
Petty issues. It is a pity! Rais anashughulika na ujinga/mambo madogo madogo badala ya mambo ya kuliokoa taifa
 
Huyo mzee alikuwa Genius.

Forehead (Paji lake la uso) ni kubwa , na hiyo ni ishara ya watu ambao wako gifted kiakili.
Hata Mwalimu Nyerere alikuwa na Forehead kubwa.

Siku nyingine Vetting ya viongozi ihusishe kupima circumference ya kichwa, na Urefu wa makomwe yao. Wenye makitu hayo makubwa hao ndo watu wenye akili!

Siyo unaleta viongozi wana vibichwa vidogo kama limau, hatuwezi kuwa na fikra za kusonga mbele
 
Huyo mzee alikuwa Genius.

Forehead (Paji lake la uso) ni kubwa , na hiyo ni ishara ya watu ambao wako gifted kiakili.
Hata Mwalimu Nyerere alikuwa na Forehead kubwa.

Siku nyingine Vetting ya viongozi ihusishe kupima circumference ya kichwa, na Urefu wa makomwe yao. Wenye makitu hayo makubwa hao ndo watu wenye akili!

Siyo unaleta kiongozi ana kichwa kidogo kama limau, hamna kitu hapo!
Kwa hiyo 2030 twende na Nape? 😄😄😄
 
Hapo umechemsha. Nyerere hakuwa na paji la uso pana japo alikuwa smart kichwani. Kwasisi tuliokuwa tunakutana naye karibu tunajua. Tafuta theory nyingine kuhalalisha hoja yako
 
, punguza majungu chief.
 
Hapo umechemsha. Nyerere hakuwa na paji la uso pana japo alikuwa smart kichwani. Kwasisi tuliokuwa tunakutana naye karibu tunajua. Tafuta theory nyingine kuhalalisha hoja yako
nazungumzia paji la uso kubwa!.

Kuna ukubwa katika upana na pia kuna ukubwa katika urefu.

Nenda kaangalie paji la Uso la Nyerere kwenye picha, utaona ni refu kuliko wenzake wengi anaokuwa nao katika picha moja.

Pia volume/ujazo wa kichwa cha Nyerere ilikuwa ni kubwa sana, kaangalie picha zake
 
Angalia paji la Uso la Salim Ahmed Salim alipokuwa kijana, uone lilivyo kubwa. Angalia urefu wake kuanzia nywele za utosini hadi kwenye macho, uone lilivyo refu. Hiyo ni Sign ya Ubongo mkubwa a.k.a Akili nyingi.

Ndiyo maana huyu mzee katika ujana wake aliweza kuachieve mambo makubwa ambayo ni un-imaginable kwa vijana wa leo.

Huyu mzee Almanusra aukwae ukatibu mkuu wa UN mwanzoni mwa miaka ya 1980 kama siyo figisu za Marekani.

Wakati huo huyu mzee alikuwa in his early 40's tu.
Screenshot_20230930-160647.jpg
 
Back
Top Bottom