Rais Samia: Chuo cha Diplomasia sasa kitaitwa Chuo cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Angalia paji la Uso la Salim Ahmed Salim alipokuwa kijana, uone lilivyo kubwa. Angalia urefu wake kuanzia nywele za utosini hadi kwenye macho, uone lilivyo refu. Hiyo ni Sign ya Ubongo mkubwa a.k.a Akili nyingi.

Ndiyo maana huyu mzee katika ujana wake aliweza kuachieve mambo makubwa ambayo ni un-imaginable kwa vijana wa leo.

Huyu mzee Almanusra aukwae ukatibu mkuu wa UN mwanzoni mwa miaka ya 1980 kama siyo figisu za Marekani.

Wakati huo huyu mzee alikuwa in his early 40's tu.
View attachment 2767166
Unasifia upumbavu alifanya nn cha maana tunataka kuona matokeo sio history sijui upuuz gan mjinga ww
 
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa shughuli ya Uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Dkt. Salim Ahmed Salim, leo Septemba 30, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Maktaba hiyo ya Dk. Salim ambaye ni Mwanadiplomasia wa Kimataifa aliyekuwa Katibu Mkuu wa nane wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) Mwaka 1989 hadi 2001 itajumuisha video, picha, hotuba na machapisho.

Lengo la kuanzishwa kwa maktaba hiyo, ni kutoa uelewa zaidi wa safari na mchango wa Dkt. Salim ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu na katika kuitumikia jamii.

Dkt. Salim amewahi kuwa Balozi wa Misri nafasi ambayo aliitumikia kwa muda wa mwaka mmoja kati ya mwaka 1964 na 1965 kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini India.
View attachment 2766971
Endelea kufuatilia kupata updates ya kinachoendelea ukumbini...

View attachment 2766974
Dk Salim Ahmed Salim (kulia) akiwa na Joseph Sinde Warioba aliyewahi pia kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. (Picha: Maktaba ya Salim Ahmed Salim).

View attachment 2766975
Dk Salim Ahmed Salim (kushoto) akiwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
(Picha: Maktaba ya Salim Ahmed Salim).

Wageni wengine ambao wameshawasili ukumbi ni Rais Mstaafu Jayaka Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Ahmed Salim Mtoto wa Dkt. Salim na Mwakilishi wa Familia naye ni mmoja wa watakaoshiriki kwa ukaribu katika tukio hili.

Mazungumzo kuhusu Dkt. Salim Ahmed Salim kulingana na nyadhifa mbalimbali alizozitumikia yatafanyika kwa kuongozwa na Moderator Saida Yhya-Othuman:

Nafasi: Uwaziri Mkuu
Mzungumzaji: Joseph Warioba (Waziri Mkuu Mstaafu)

Nafasi: Mwanasiasa na Pan Africanist
Mzungumzaji: Christopher Liundi (Balozi Mstaafu)

Nafasi: Mshauri
Mzungumzaji: Balozi Amina Salum Ali

Inatusaidia nini ndio maana alidumu kwa muda mfupi sana kwenye nafasi ya waziri mkuu baada ya shujaa Edward Sokoine Moringe kufariki mwaka tare 12 Aprili 1984 hukoWami Dkawa Morogoro kwa ajali ya gari iliyosababishwa na dereva wa kutoka kambi ya wapigania uhuru wa Afrika kusini aitwaye 'DUBE'
 
Huyo mzee alikuwa Genius.

Forehead (Paji lake la uso) ni kubwa , na hiyo ni ishara ya watu ambao wako gifted kiakili.
Hata Mwalimu Nyerere alikuwa na Forehead kubwa.

Siku nyingine Vetting ya viongozi ihusishe kupima circumference ya kichwa, na Urefu wa makomwe yao. Wenye makitu hayo makubwa hao ndo watu wenye akili!

Siyo unaleta viongozi wana vibichwa vidogo kama limau, hatuwezi kuwa na fikra za kusonga mbele
😆😆😆
 
nazungumzia paji la uso kubwa!.

Kuna ukubwa katika upana na pia kuna ukubwa katika urefu.

Nenda kaangalie paji la Uso la Nyerere kwenye picha, utaona ni refu kuliko wenzake wengi anaokuwa nao katika picha moja.

Pia volume/ujazo wa kichwa cha Nyerere ilikuwa ni kubwa sana, kaangalie picha zake
Kaka watu wengine sisi usituambie tukaangalie picha yake bali tulibahatika kuwa naye karibu. Anyway ninachopingana na wewe ni hiyo nadharia ya ukubwa wa paji la uso na mtu kuwa Genius. Yaani nyie ndio wale mtu anapopata nafasi na kufanikiwa basi mtampa kila sifa. Kiukweli Nyerere alifanikiwa sana hasa katika uadilifu na kuunganisha watu. Lakini ninaamini kufanya kwake vizuri HAIHUSIANI NA PAJI LA USO na SIO KWAMBA YEYE ALIKUWA GENIUS SANA.

Pia tushukuru Nyerere hakuwa MCHAGA au KUTOKA NG'AMBO YA PILI
 
Huyo mzee alikuwa Genius.

Forehead (Paji lake la uso) ni kubwa , na hiyo ni ishara ya watu ambao wako gifted kiakili.
Hata Mwalimu Nyerere alikuwa na Forehead kubwa.

Siku nyingine Vetting ya viongozi ihusishe kupima circumference ya kichwa, na Urefu wa makomwe yao. Wenye makitu hayo makubwa hao ndo watu wenye akili!

Siyo unaleta viongozi wana vibichwa vidogo kama limau, hatuwezi kuwa na fikra za kusonga mbele
😂😂😂😂😂😂
 
Unasifia upumbavu alifanya nn cha maana tunataka kuona matokeo sio history sijui upuuz gan mjinga ww

Ndio ukasome nyaraka zake. Kwa kifupi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na baadae Kawa Katibu Mkuu wa AU miaka hiyo ikijulikana Kama OAU. Ilibaki kidogo awe Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kama sio ujinga wa Marekani kumuwekea VETO.
 
Inatusaidia nini ndio maana alidumu kwa muda mfupi sana kwenye nafasi ya waziri mkuu baada ya shujaa Edward Sokoine Moringe kufariki mwaka tare 12 Aprili 1984 hukoWami Dkawa Morogoro kwa ajali ya gari iliyosababishwa na dereva wa kutoka kambi ya wapigania uhuru wa Afrika kusini aitwaye 'DUBE'

Unajua kwanini alikaa muda mfupi?
 
Back
Top Bottom