ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,109
- 49,817
Legacy ni ipi katuachia yule bwana?
View: https://twitter.com/CyrilRamaphosa/status/1708497215356858878?t=8Txy9u4MgcWKiiiolvWvuQ&s=19
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema tovuti ya Dk. Salim Ahmed Salim, ni hazina kubwa kwa taifa kwani ina manufaa kwa wale wote wanaotaka kujifunza, masuala ya kidiplomasia na uongozi.
Dk. Samia ameyasema hayo leo Septemba 30, 2023 katika uzinduzi wa tovuti ya kwanza ya hifadhi ya nyaraka ya Kiongozi kwa njia ya kidigitali inayotambulika "The Salim Ahmed Salim Digital Archive" www.salimahmedsalim.com katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
"Nimefarijika sana kusikia tovuti hii itakuwa endelevu na itakuwa ikiboreshwa mara kwa mara,"
Aidha, Dk. Samia amesema kupitia ushirikiano wa serikali na familia ya Dk. Salim, tovuti hii itamuwezesha kila mmoja kuifikia bila gharama yeyote.
"Tunapomzungumzia Dk. Salim Ahmed Salim, ni ukweli usiopingika kwamba huyu ni Mtanzania mahiri,
"Katika nyanja ya kidiplomasia Dk. Salim alituwakilisha katika nchi mbalimbali ikiwemo Misri, India, China.
"Dk.Salim alichapa kazi kwa moyo wake wote hivyo kudhihirisha uadilifu na uchapakazi," Dk. Samia amenukuliwa.
Imeandaliwa na Ismaily Kawambwa na Samwel Swai
Habari Leo
View: https://www.instagram.com/p/Cx0WzbpI21R/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==