Rais Samia boresha kila kitu tutakusahau, ila ukimaliza mchakato wa Katiba tutakukumbuka milele

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
5,277
7,984
J K Nyerere alikuwa Pan Africanist na hicho ndicho kilicho mpamanua dhidi ya wenzie kama akina Jomo Kenyatta au Milton Obotte. Miaka yote alifikiria kuunga mkono mapambano ya nchi zinazopigana na wakoloni.

Mwinyi alikuwa mwana Diplomasia mliberali na ndiyo maana akafungua milango ya uchumi wa soko huria miaka ya 1985-95 na kujipatia jina la Ruksa. Uanzishaji wa Madaladala na uuzwaji wa mitumba uliopo mpaka leo ni moja kati ya maamuzi yake bora kabisa.

Mkapa alikuwa Mwandishi na Mwana Diplomasia mbobezi na muumini wa uchumi wa sekta binafsi. Alijipambanua kwa ile sera ya "Uwazi na Ukweli" na tukaona magazeti na vituo vya TV na Radio binafsi vikishamiri. Na tukashudia na kasi kubwa ya kuuzwa kwa mashirika ya umma (privatisation). Ni baba wa mapinduzi ya uchumi huu wa kisasa tulionao.

Kikwette alikuwa Mwanasiasa aliyegeuka Mwana Diplomasia. Alibebwa na kauli ya "Maisha Bora kwa Watu Kila Mtanzania". Na kwa kusema ukweli alijitahidi kuwa kila mtu aweze kupata riziki kutokana na mazingira aliyopo. Tutamkumbuka kwa kupanua Uhuru wa maoni, demokrasia na usuluhishi wa migigoro kwa majadiliano.

Magufuli alikuwa ni Mkemia aliyejihuisha kuwa mhandisi wa miundombinu. Kwa miaka aliyohudumu kama Waziri kwenye Awamu ya Mkapa na Kikwette alijenga barabara barabara na madaraja mengi kuliko kiongozi yeyote. Hiyo ndiyo ilimpambanua na kuwa Rais wa miundombinu katika kipindi chake cha u-Rais kwa kauli yake ya "Hapa Kazi Tu". Aliona miundombinu ndiyo itakuwa chachu ya kujenga uchumi. Lakini kipindi chake kifupi kimeacha majeraha mengi kwenye haki za kiraia, Utawala bora, ukandamizaji demokrasia, utekwaji wa WAKOSOAJI, uwapo wa kikundi cha WASIOJULIKANA, dhuluma kwa wafanyabiashara kupitia TASK FORCE na mengine mengi.

Aidha ile kauli ya Baba wa Taifa mwaka 1982 kuwa "Katiba hii imenipa Madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu", ilijidhihirisha kipindi cha Magufuli.

Kimsingi kila Rais au kiongozi falsafa yake hujengwa na kile alichokifanya sana au kile kilichomjengea umaarufu.

Je Rais Samia Ni Nani?
Rais Samia ni Public Administrator ambaye amehudumu kama Waziri wa Mazingira na Muungano kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais kipindi cha Jakaya Kikwette.

Lakini hicho siyo kilichomjenga kuweza kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye Makamu wa Rais wa Tanzania kwenye awamu ya Magufuli.

Mwaka 2014 SSH alichaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge Maalum la Katiba (BMLK) chini ya Samuel Sitta (RIP). Hii kazi aliyoifanya kama Naibu Spika wa BMLK ndiyo imemjengea haiba aliyonayo.

SSH anaamini katika kufanya mambo kwa kufuata katiba, anaamini katika Utawala wa Sheria. SSH anataka kila Mtanzania atendewe haki, hapendi dhuluma kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa Taifa. Ana amini katika Uhuru wa vyombo vya habari na ukosoaji chanya. Ana amini katika ushirikiano wa kimataifa utakuza uchumi kupitia uwekezaji.

Kwa maoni yangu yote anayofanya Rais SSH ni mazuri lakini yasipowekwa kwenye MUSTAKABALI SAHIHI yatapotea.

Kitu pekee kitakacho yafanya mambo anayosimamia yabakie kuwa ya kudumu ni KUMALIZIA mchakato wa KATIBA, kile ambacho ndiyo kinajenga haiba yake.

Kwenye Ilani ya CCM ya 2015, kulikuwa na ajenda ya kumalizia mchakato wa KATIBA. Kwa hiyo CCM kama Chama kinataka Katiba mpya ya wananchi.

Bahati mbaya mtangulizi wake Magufuli hakunona kama ni KIPAUMBELE kwa kuwa haiba yake ilijengwa na miundombinu.

JK hakumaliza mchakato wa KATIBA mpya kwa sababu alikuwa DHAIFU (Hili tusibishane, kwa kuwa hata JJ Mnyika aliwahi kutamka Bungeni).

Nini Afanye Samia?
Anaweza kuwapata wataalamu wa Sheria na Katiba ambao siyo ndumila kuwili (kama Polepole + Kabudi) wakazi huisha Rasimu zile 2 ya Warioba na ya Sitta/ Chenge). Wakaangalia katika vipengele vinavyokinzana ni vipi vina masilahi mapana ya Taifa letu la Tanzania. Kisha wakaipeleka kwenye hatua ya REFERANDUM

Namsihi Rais SSH kama anapita humu JF au wasaidizi wake wamwambie kuwa Yeye ni Tunda la BMLK, na Tanzania itamkumbuka milele na milele kama atatuachia KATIBA mpya ya wananchi.

Atakumbukwa kwenye UKURASA mmoja na J K Nyerere hata kama atakaa kipindi kimoja cha miaka 5.

Afrika Kusini na Kenya wanafaidi matunda ya Katiba ya Wananchi. Kule tumeona namna Institutions zilivyo STRONG kuliko PERSONALITIES. Magufuli alikuwa VERY STRONG person akazizidi na Institutions zetu zote za Mahakama, Bunge, Polisi, Magereza, nk

Tanzania HATUTAKI VIINGOZI WENYE NGUVU tena Ila tunataka TAASISI ZENYE NGUVU
 
CCM hawataki KATIBA.
SI mama wala wajumbe, wana damu mikononi mwao, wanaogopa tume mbalimbali zilishatoa majibu hasa mauaji ya zanzibar, kifo cha akwilina , mtwara, kibiti na mizoga ya koko beach, hawawezi kubali.
Uzuri Mwenda zake aliitumia kuwapiga, kama wana akili watataka imaliziwe
 
Unalilia katiba, lakini inaweza kubadilishwa kinyume na ulivokua unategemea na ukanyonywa zaidi. Cha msingi ni kuandaa wazalendo tu
 
CCM hawataki KATIBA.
SI mama wala wajumbe, wana damu mikononi mwao, wanaogopa tume mbalimbali zilishatoa majibu hasa mauaji ya zanzibar, kifo cha akwilina , mtwara, kibiti na mizoga ya koko beach, hawawezi kubali.
Tuendelee kupaza sauti, tusikate tamaa
 
Kiukweli ktk hili tusitegemee kama kuna rais anaweza kuthubutu kukifanya. Yaani anoe kisu cha kumkata yeye na chama chake?? Never!!
Kwa mara hii inawezekana hasa kutoka kwa Wazanzibari ambao mara nyingi wanaongelea kuwa wanataka ZNZ yenye Mamlaka Kamili. Ni fursa ya ZNZ sasa kuweza kuifanya ZNZ isimame na ijipange kiuchumi
 
ZANZIBAR hiwezi ondoshwa kwenye mnnungano ,never, ila kuna namna ambavyo iounguziwe msaada kutoka bara, inatunyonya sana.
 
Samia anayo nafasi ya kusomwa na vizazi vya nchi hii milele.
penati amepewa kazi kwake.

Zanzibar awatoe kwenye mauaji wanayofanyiwa na MaCCM , kila baada ya miaka 5 ya uchaguzi.

Afute masheria yanayoumiza wapinzani wa CCM. Atuletee katiba mpya.
 
J K Nyerere alikuwa Pan Africanist na hicho ndicho kilicho mpamanua dhidi ya wenzie kama akina Jomo Kenyatta au Milton Obotte. Miaka yote alifikiria kuunga mkono mapambano ya nchi zinazopigana na wakoloni.

Mwinyi alikuwa mwana Diplomasia mliberali na ndiyo maana akafungua milango ya uchumi wa soko huria miaka ya 1985-95 na kujipatia jina la Ruksa. Uanzishaji wa Madaladala na uuzwaji wa mitumba uliopo mpaka leo ni moja kati ya maamuzi yake bora kabisa.

Mkapa alikuwa Mwandishi na Mwana Diplomasia mbobezi na muumini wa uchumi wa sekta binafsi. Alijipambanua kwa ile sera ya "Uwazi na Ukweli" na tukaona magazeti na vituo vya TV na Radio binafsi vikishamiri. Na tukashudia na kasi kubwa ya kuuzwa kwa mashirika ya umma (privatisation). Ni baba wa mapinduzi ya uchumi huu wa kisasa tulionao.

Kikwette alikuwa Mwanasiasa aliyegeuka Mwana Diplomasia. Alibebwa na kauli ya "Maisha Bora kwa Watu Kila Mtanzania". Na kwa kusema ukweli alijitahidi kuwa kila mtu aweze kupata riziki kutokana na mazingira aliyopo. Tutamkumbuka kwa kupanua Uhuru wa maoni, demokrasia na usuluhishi wa migigoro kwa majadiliano.

Magufuli alikuwa ni Mkemia aliyejihuisha kuwa mhandisi wa miundombinu. Kwa miaka aliyohudumu kama Waziri kwenye Awamu ya Mkapa na Kikwette alijenga barabara barabara na madaraja mengi kuliko kiongozi yeyote. Hiyo ndiyo ilimpambanua na kuwa Rais wa miundombinu katika kipindi chake cha u-Rais kwa kauli yake ya "Hapa Kazi Tu". Aliona miundombinu ndiyo itakuwa chachu ya kujenga uchumi. Lakini kipindi chake kifupi kimeacha majeraha mengi kwenye haki za kiraia, Utawala bora, ukandamizaji demokrasia, utekwaji wa WAKOSOAJI, uwapo wa kikundi cha WASIOJULIKANA, dhuluma kwa wafanyabiashara kupitia TASK FORCE na mengine mengi.

Aidha ile kauli ya Baba wa Taifa mwaka 1982 kuwa "Katiba hii imenipa Madaraka makubwa sana, siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na kuwa kama Mungu", ilijidhihirisha kipindi cha Magufuli.

Kimsingi kila Rais au kiongozi falsafa yake hujengwa na kile alichokifanya sana au kile kilichomjengea umaarufu.

Je Rais Samia Ni Nani?
Rais Samia ni Public Administrator ambaye amehudumu kama Waziri wa Mazingira na Muungano kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais kipindi cha Jakaya Kikwette.

Lakini hicho siyo kilichomjenga kuweza kuwa Mgombea Mwenza na hatimaye Makamu wa Rais wa Tanzania kwenye awamu ya Magufuli.

Mwaka 2014 SSH alichaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge Maalum la Katiba (BMLK) chini ya Samuel Sitta (RIP). Hii kazi aliyoifanya kama Naibu Spika wa BMLK ndiyo imemjengea haiba aliyonayo.

SSH anaamini katika kufanya mambo kwa kufuata katiba, anaamini katika Utawala wa Sheria. SSH anataka kila Mtanzania atendewe haki, hapendi dhuluma kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa Taifa. Ana amini katika Uhuru wa vyombo vya habari na ukosoaji chanya. Ana amini katika ushirikiano wa kimataifa utakuza uchumi kupitia uwekezaji.

Kwa maoni yangu yote anayofanya Rais SSH ni mazuri lakini yasipowekwa kwenye MUSTAKABALI SAHIHI yatapotea.

Kitu pekee kitakacho yafanya mambo anayosimamia yabakie kuwa ya kudumu ni KUMALIZIA mchakato wa KATIBA, kile ambacho ndiyo kinajenga haiba yake.

Kwenye Ilani ya CCM ya 2015, kulikuwa na ajenda ya kumalizia mchakato wa KATIBA. Kwa hiyo CCM kama Chama kinataka Katiba mpya ya wananchi.

Bahati mbaya mtangulizi wake Magufuli hakunona kama ni KIPAUMBELE kwa kuwa haiba yake ilijengwa na miundombinu.

JK hakumaliza mchakato wa KATIBA mpya kwa sababu alikuwa DHAIFU (Hili tusibishane, kwa kuwa hata JJ Mnyika aliwahi kutamka Bungeni).

Nini Afanye Samia?
Anaweza kuwapata wataalamu wa Sheria na Katiba ambao siyo ndumila kuwili (kama Polepole + Kabudi) wakazi huisha Rasimu zile 2 ya Warioba na ya Sitta/ Chenge). Wakaangalia katika vipengele vinavyokinzana ni vipi vina masilahi mapana ya Taifa letu la Tanzania. Kisha wakaipeleka kwenye hatua ya REFERANDUM

Namsihi Rais SSH kama anapita humu JF au wasaidizi wake wamwambie kuwa Yeye ni Tunda la BMLK, na Tanzania itamkumbuka milele na milele kama atatuachia KATIBA mpya ya wananchi.

Atakumbukwa kwenye UKURASA mmoja na J K Nyerere hata kama atakaa kipindi kimoja cha miaka 5.

Afrika Kusini na Kenya wanafaidi matunda ya Katiba ya Wananchi. Kule tumeona namna Institutions zilivyo STRONG kuliko PERSONALITIES. Magufuli alikuwa VERY STRONG person akazizidi na Institutions zetu zote za Mahakama, Bunge, Polisi, Magereza, nk

Tanzania HATUTAKI VIINGOZI WENYE NGUVU tena Ila tunataka TAASISI ZENYE NGUVU
Watu wengine akili zao zimepakatwa na wengine. Hivi kwa jinsi ilivyo katiba ya tanzania inapungua nini hadi mtu uamini hushindi uchaguzi kwa sababu ya katiba. Viongozi wa chadema wanajua kwa nini wanashindwa uchaguzi ila wamewaaminisha nyumbu wao eti hawashindi kwa sababu ya katiba.
Nachowaeleza hata ikiandikwa katiba mpya chini ya serikali ya ccm haitawasaidia wapinzani kuingia madarakani. Na kama lengo la wapinzani ni serikali tatu wala hilo halitatokea chini ya ccm au chama kingine kinachopenda kuwepo muungano. Lengo la madai ya serikali tatu ni ili kurahisisha kuvunja muungano.
 
Usiende nje ya hoja. Katiba Mpya ya wananchi ni jambo kisheria siyo suala la CDM. Rudi ukasome ILANI ya CCM ya mwaka 2015 utakuta suala la Katiba limetajwa.

Katiba ya nchi siyo suala la uchaguzi tu lakini bali hata masuala ya haki za wanananchi, namna ya kupata wawailishi, tunu za Taifa, elimu afya nk.

Ila mtoa hoja kmbwembwe Kama umesoma elimu ya Sekondari naamini suala la Katiba utakuwa umesoma kwenye Civics. Ila kama wewe ni la 7 B basi tena Ni bahati mbaya
 
Huwa nasikitika wana chadema na ccm tunapoongelea katiba mpya wao wanakimbilia kwenye uchaguzi. ,,Japo ni sawa bila uchaguzi wa haki na halali hatuwezi pata viongozi tunaowahitaji. Lakini katiba mpya ni zaidi ya hapo. Tunahitaji Taasisi zenye nguvu kuiongoza nchi na si akili ya mtu mmoja.
Zile tabia za marehemu hata kujikuta anakuwa dikteta ni kwasababu ya udhaifu wa katiba.
Muungano ni muhimu, mimi naamini sana kwenye muungano ,, na siyo Zanzibar peke yake bali ningependa hizi nchi zetu za EA ziungane ziwe nchi moja. Muungano ni nguvu- lakini tutumie hoja na si nguvu kuulinda Muungano.

Tuione future ya nchi yetu ambapo kiongozi hajifanyii anavyotaka bali afate sheria.
 
Huyo jamaa ni moja ya hasara tulizonazo hapa nchini.
 
Njia nzuri ya katiba ni kufanya AMENDMENT na katiba haitakiwi kuwa kana gazeti la zamani la mzalendo au kitabu cha ABBOTT au kitabu cha VINE AND REES cha plant and animal biology al maarufu kama mkate

Katiba ni ka kitabu kadogo saana

Mambo mengine huwekwa kwenye sheria nyingine husika sasa kuna majitu yanapenda maandamano zaidi ya ubwabwa yanataka kila kitu kiwekwe kwenye katiba

Niliiangalia ile rasimu ya warioba nikasema hii sasa itakuwa katiba au penal code, civil procedure act, contract act, law of marriage act au cpa

Angalieni katiba ya marekani ni kadude kadogo sana

Kuna majirani zetu nao walitengeneza gazeti lao la mzalendo lakini from day one ilianza kuleta matatizo

Sasa endeleeni kusikiliza makanjanja wa sheria walio kimbilia nchi na wengine wenye uraia wa nchi za ulaya ambao wamesomea huko ama mzazi mmoja wapo ana asili ya huko.

Watu wapate mwanya wa kufanya kazi sio maandsmano na harakati zisizo na msingi

Kama kuna suala linahitaji mabadiliku ya katiba lifanyike kwa njia ya amendment maana sio vifungu vyote ama misingi yote ya katiba imepitwa na wakati ndio maana kwa ubora wa katiba iliyopo bado hao hao wanaharakari na wanasheria uchwara wamekuwa wakivinukuu vifungu vya katiba hii
 
Tufikirie Muungano hata wa Serikali 3 ili ZNZ iwe na mamlaka kamili. Haijalishi kama Rais SSH atabakia kama Gorbachev just in case Muungano utavurugika
 
Njia nzuri ya katiba ni kufanya AMENDMENT na katiba haitakiwi kuwa kana gazeti la zamani la mzalendo au kitabu cha ABBOTT au kitabu cha VINE AND REES cha plant and animal biology al maarufu kama mkate

Katiba ni ka kitabu kadogo saana

Mambo mengine huwekwa kwenye sheria nyingine husika sasa kuna majitu yanapenda maandamano zaidi ya ubwabwa yanataka kila kitu kiwekwe kwenye katiba

Niliiangalia ile rasimu ya warioba nikasema hii sasa itakuwa katiba au penal code, civil procedure act, contract act, law of marriage act au cpa

Angalieni katiba ya marekani ni kadude kadogo sana

Kuna majirani zetu nao walitengeneza gazeti lao la mzalendo lakini from day one ilianza kuleta matatizo

Sasa endeleeni kusikiliza makanjanja wa sheria walio kimbilia nchi na wengine wenye uraia wa nchi za ulaya ambao wamesomea huko ama mzazi mmoja wapo ana asili ya huko.

Watu wapate mwanya wa kufanya kazi sio maandsmano na harakati zisizo na msingi

Kama kuna suala linahitaji mabadiliku ya katiba lifanyike kwa njia ya amendment maana sio vifungu vyote ama misingi yote ya katiba imepitwa na wakati ndio maana kwa ubora wa katiba iliyopo bado hao hao wanaharakari na wanasheria uchwara wamekuwa wakivinukuu vifungu vya katiba hii
avogadro kweli unaiponda Katiba ya Kenya wakati tumeshuhudia juzi tu Mahakama Kuu ikipiga chini BBI ambayo imeasisiwa na Rais Uhuru?

Tuliona vile vile Kenya Mahakama Kuu ikipiga chini matokeo ya uchaguzi ya Kenya ya mwaka 2017.

Na USA haiwezi kuwa ndiyo model ya kila kitu. Siyo kwamba Kwa kuwa Katiba yao ni ndogo basi kila kitu kiko vizuri. Tunachogombea kwenye Katiba ni strong institutions
 
Back
Top Bottom