Rais Samia awapa shavu Wazanzibar: Ajira asilimia 21 za Muungano kuwa za Wazanzibar

Halafu cha ajabu, ikitangazwa kazi inayohusu mambo yasiyo ya muungano, bado wazenji wanaapply na hawawekwi pembeni sababu ya uzanzibar wao, Wanakuwa treated sawa na vijana wa Tanganyika.
Wapo watendaji wa serikali za Mitaa huku bara ni Wazanzibar, japo TAMISEMI siyo jambo la muungano!
Halafu wakipewa kazi wanafika kazini saa tano mchana na ijumaa wanafunga ofisi
 
Hapa namuunga mkono Samia kwa kufanya HAKI bin HAKI huu Muungano tuliingia kwa lengo la kuwameza Wazanzibari sasa Mungu katugeuzia Kibao😂😆

Kwa hakika akandamize hapo hapo na akiongeza itapendeza zaidi 😁😁
 
Ulitaka wasipewe

79 kwa 21

Hizi roho mbaya Jamani tuzitafutie dawa yaani hii ni Zaidi ya Uchawi

Katika 79 kuna 21 Ngapi?

Kwani katika 60m kuna 1.5m ngapi?

Wewe hujui kwanini mapendekezo ni kuwa akandamize zaidi hadi akili nawe ikiungie?

"Mama Samia kandamizi 50/50 au zaidi bado misukule tupo hatujakusoma 😁😁."
 
Niko Zanzibar mwaka wa kumi Sasa Kila nikiomba kitambulisho cha uzanzibar mkaaz naambiwa Sina sifa hivyo siwez kuajiriwa Wala kumiliki ardhi Zanzibar cha ajabu wazanzibar Tamisemi wakitoa ajira wanaomba na wanapata vizur tu achilia mbali hizo ajira za Jw, polisi, uhamiaji na ardhi pia bara wanamiliki Bila bugudha , hii sio haki kabisa.
 
Muungano huu wa kipuuzi ulitokana na mawazo ya mtu mmoja tu(Nyerere) na kwa ubwege wa viongozi wengine wa wakati huo walivyokuwa wanamuogopa walishindwa hata kutoa ushauri wa kuweka kipengele cha kufanya majadiliano upya angalau kila baada ya miaka kadhaa ili kuendana na mahitaji ya wakati huo matokeo yake ndio haya sasa tunaishia tu kulalamika lakini hakuna mlango wa kutokea.
 
10 tena kwa mama Sukuma Gang waisome namba vizuri.
Mungu amejibu maombi ya upinzani .
 
Kwa hii ratio, wanzanzibari hawatakuwa na tatizo la ajira kamwe. Nadhani viongozi wetu hawajui hesabu. Ili haki itendeke walitakiwa waangalie population ya Wazanzibari against Watanganyika. Hiyo population ndio ingekuwa determinat factor ya kujua asilimia kiasi gani ya ajira iende visiwani na asilimia ngapi ibaki bara. Hii ya kusema tu 21% iende Zanzibar ni baseless, useless and groundless. It is purely thumbsuck.
Hii inaonyesha ni jinsi gani kwenye mikataba tunavyoliwa. Kama Zanzibar tu inatushinda kunegociate nao kenye kugawana ajira eti kesho kuna mtu ataamini tumeweza kwenye Bandari ya Bagamoyo ....!!
 
View attachment 2015004

Watu milioni 58 wanagombania asililia 79 ya Ajira

Ila watu milioni 1.5 unawapa asilimia 21 ya Ajira

Hongera mama, Charity begibs at home.

Watanganyika huu ni muda wa kukaa na kutafakari huu muungano una faida na sisi au la?

Hebu tazama

1. Mzanzibar ana haki ya ardhi yote ya Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ila wewe Mtanganyika unaweza kupata ardhi kwa masharti ya wageni

2. Mzanzibar anahaki na Ajira zote za mambo hata yasiyo ya muungano kwa mfano TAMISEMI

3. Mzanzibar anaweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi huku Tanganyika hata kwa mambo yasiyo ya muungano kwa mfano balozi wa nyumba kumikumi lakini Mtanganyika hawezi kuwa shehia kule Zanzibar

4. Ajira zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni exclusive kwa ajili ya Wazanzibar, Yaani Wao wanakula kotekote Tanganyika na kule Zanzibar

5. Wao wamepambana kuondoa mafuta kwenye mambo ya muungano, lakini sisi Ardhi yetu wanaitaka, na wanaienjoy sana tu kwa sababu nawajua Wazanzibar wanaomiliki ardhi TZ

Sasa katika hali kama hii, Huu muungano una faida kwa Watanganyika kweli
It is their time babeee....

Mama songa mbeleee
 
Hapa namuunga mkono Samia kwa kufanya HAKI bin HAKI huu Muungano tuliingia kwa lengo la kuwameza Wazanzibari sasa Mungu katugeuzia Kibao😂😆
Yani mi nabariki kabisa...

Wacha tuvune tulichopanda.
 
Zanzibar nchi ndogo ina watu wachache lakini ina serikali yake, ajira katika hiyo serikali ni. za wazanzibar pekee.
Zanzibar ardhi yake ni kwa ajili ya Wazanzibar peke yao

Ila ardhi ya Tanganyika ni ya WOTE including wazanzibar.

Ajira za Tanganyika kwenye mambo yasiyo ya muungano ni ya WOTE including Wazanzibar.

Sasa huu muungano gani wa Chao chao, chetu chao?
 
Hata Mimi nawashangaa Watanganyika wenzangu. Hii asilimia 21 iliwekwa na awamu ya 4. Awamu ya 5 wakagoma kuitekeleza. Huyu hangaya wanamuonea bure tu.



upuuzi huu uliafikiwa kwenye kikao hicho hapo juu wa maelekezo ya mama maushungi na wala sio kipindi cha awamu ya 5
fuatilia yaliyoafikiwi kwenye hicho kikao kuna maupuuzi mengi sana ya kuwapendelea wanzazibar ndio maana hata yaliyojiri yalifichwa .
moja wapo ya maafikiano ya kikao hicho ni huu upuuzi,wa ajira ila yapo mengi sana,

jafoo na mr planning ni watu wapuuzi sana
 
View attachment 2015004

Watu milioni 58 wanagombania asililia 79 ya Ajira

Ila watu milioni 1.5 unawapa asilimia 21 ya Ajira

Hongera mama, Charity begins at home.

Watanganyika huu ni muda wa kukaa na kutafakari huu muungano una faida na sisi au la?

Hebu tazama

1. Mzanzibar ana haki ya ardhi yote ya Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ila wewe Mtanganyika unaweza kupata ardhi kwa masharti ya wageni

2. Mzanzibar anahaki na Ajira zote za mambo hata yasiyo ya muungano kwa mfano TAMISEMI

3. Mzanzibar anaweza kushika nafasi yoyote ya uongozi huku Tanganyika hata kwa mambo yasiyo ya muungano kwa mfano balozi wa nyumba kumikumi lakini Mtanganyika hawezi kuwa shehia kule Zanzibar

4. Ajira zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni exclusive kwa ajili ya Wazanzibar, Yaani Wao wanakula kotekote Tanganyika na kule Zanzibar

5. Wao wamepambana kuondoa mafuta kwenye mambo ya muungano, lakini sisi Ardhi yetu wanaitaka, na wanaienjoy sana tu kwa sababu nawajua Wazanzibar wanaomiliki ardhi TZ

Sasa katika hali kama hii, Huu muungano una faida kwa Watanganyika kweli?
Wapinzani hawachoki kuibua mambo wakishindwa hili wanaibua lile. Wao walitaka serkali tatu ambayo kila mtu angebaki kwao, ikakataliwa.
 
Back
Top Bottom