Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Watu milioni 58 wanagombania asililia 79 ya Ajira
Ila watu milioni 1.5 unawapa asilimia 21 ya Ajira
Hongera mama, Charity begins at home.
Watanganyika huu ni muda wa kukaa na kutafakari huu muungano una faida na sisi au la?
Hebu tazama
1. Mzanzibar ana haki ya ardhi yote ya Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) ila wewe Mtanganyika huko Zanzibar unaweza kupata ardhi kwa masharti ya wageni
2. Mzanzibar anahaki na Ajira zote za mambo hata yasiyo ya muungano kwa mfano TAMISEMI
3. Mzanzibar anaweza kushika nafasi yoyote ya uongozi huku Tanganyika hata kwa mambo yasiyo ya muungano kwa mfano balozi wa nyumba kumikumi lakini Mtanganyika hawezi kuwa kiongozi wa shehia kule Zanzibar
4. Ajira zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni exclusive kwa ajili ya Wazanzibar, Yaani Wao wanakula kotekote Tanganyika na kule Zanzibar
5. Wao wamepambana kuondoa mafuta kwenye mambo ya muungano, lakini sisi Ardhi yetu wanaitaka, na wanaienjoy sana tu kwa sababu nawajua Wazanzibar wanaomiliki ardhi TZ
Sasa katika hali kama hii, Huu muungano una faida kwa Watanganyika kweli?