Ifutwe Zanzibar tuwe na Tanzania au uwepo Muungano usiohusisha urais

NANCA

Member
Jun 23, 2023
92
100
Haiwezekani yani haiwezekani, haiwezekani wazanzibar wawe na haki ya kutawala kote, Tanganyika na Zanzibar afu watanganyika tusiwe na haki ya kutawala Zanzibar, sa huo ndo muungano gani wa kinyonyaji, hiyo hapana na hatutaki tena.

Leo hii watanganyika tunapigwa mande, kule kwao visiwani ni mzanzibar na huku tanganyika ni mzanzibar kwa kivuli cha Tanzania, Kiasi kwamba Kama Rais anakasumba ya udokozi na ujanjaujanja kwa katiba hii inayompa umungu si anaweza kuiba Tanganyika na akapeleka kwao Zanzibar kwa kigezo cha muungano na utanzania?

Kama Hayati Magufuli aliweza kupeleka chato kwa kigezo cha kote ni Tanzania, huyu anashindwaje kufanya hvyo kwa kigezo cha Tanzania na utetezi wa chawa wake?

-Kama mnautaka muungano basi tukubaliane yafuatayo:

1. Kwa muundo huu tulionao wa bila Tanganyika, basi Rais wa Zanzibar atoke popote, yaani awe mtanganyika au mzanzibar na rais wa Tanzania iwe kama ilivyo sasa.

2. Watanganyika wawe na haki sawa katika umiliki wa ardhi kama ilivyo kwa wazanzibar huku bara.

3. Au Zanzibar ifutwe Kama ilivyofutwa tanganyika na ibaki Tanzania na Rais awe mmoja ambae atapigiwa kura na watu wote wenye sifa nchi nzima.

Kwa tafsiri kwamba Zanzibar iwe Kama mkoa au kitongoji cha Tanzania, isiwe na serikali yake yenyewe.

4. Kama hamtaki vyote basi muungano katika mambo ya kisiasa ikiwemo kushea marais na mawaziri ufe, hivyo Tanganyika iwe na Rais wake na Zanzibar iwe na Rais wake na tushirikiane kwa kuunda jumuiya ambayo itaainisha mambo ya kushirikiana.

NOTE: Ni unyonge na ujinga kwa watanganyika kukubali kutawaliwa na mzanzibar ili hali wazanzibar hawataki kutawaliwa na watanganyika.

Haikubaliki Rais wa Zanzibar awe mzanzibar tu afu Rais wa tanganyika awe yeyote kwa kivuli cha Tanzania. Katika hili Nyerere alitukosea sana hasa kwa kuwadekeza wazanzibar, kuwaonea aibu na kudhani mfumo utakua vilevile Kama alivyoufikiria yeye.
 
watanganyika wengi sana walishaifutaga kwenye akili zao, imebakitu kwenye makaratasi. jambo ambali ni kazi ndogo ya kumalizia imebaki endapo tutakubaliana kufanya hivyo. kuna mtu anataka muungano hapa, ukiondoa wale wazanzibar wenye maslahi bara.
 
Hili jambo mi nilishawahi kusema hapa kundini watu hawakunielewa

Labda ni Kwa namna nilivyo liwadirisha.

Mi naona Kwa jinsi muungano ulivyo ebu tufute serikali ya Zanzibar tubaki na Tanzania
Zanzibar ibaki mikoa kama ilivyo kigoma, Kilimanjaro n.k
 
Watanganyika wengi tatizo lenu muungano hamjajishughulisha nao wala hamuujui kwa sababu haujawahi kukipeni athari yoyote
 
Huu Muungano uvunjike tu. Maana hauna manufaa yoyote yale kwa Tanganyika.
Hasa pale mzanzibar anaweza kuwa Rais Bara,ila Mtanganyika hawezi kuwa Rais Zanzibar.

Nyerere aliharibu kabisa eti Rais wa muungano akitoka Tanganyika basi Makamu atoke Zanzibar na vice versa.

Na hii aliileta wakati yeye anastaafu. Niliona mahali kipindi cha Nyerere Rais wa Zanzibar alikuwa Makamu wa pili Wa Rais Muungano. Si bora ingebaki hivyo hivyo.

Na huku Muungano Rais na makamu watoke Tanganyika maana kwa kura hakuna mtu kutoka Zanzibar anaweza kutoboa kuwakilisha CCM urais.
 
Muungano uvunjwe tu, Tanganyika irudi kwenye nafasi yake na Zanzibar na Pemba yake ibakie kuwa nchi kama ilivyokuwa.
Tanganyika, ikirudi irudi kwenye mfumo wa majimbo kama ilivyokuwa zamani au mikoa ichukuliwe kama majimbo yanayojitegemea.
 
Haiwezekani yani haiwezekani, haiwezekani wazanzibar wawe na haki ya kutawala kote, Tanganyika na Zanzibar afu watanganyika tusiwe na haki ya kutawala Zanzibar, sa huo ndo muungano gani wa kinyonyaji, hiyo hapana na hatutaki tena.
Hapana ifutwe Tanzania tiwe na Zanzibar. Hili ndilo jina kongwe kuliko Tanganyika yenu.
 
Siku ccm inatoka madarakani tunachukua wilaya zetu za unguja na pemba tunampeleka mkuu wa wilaya akazisimamie
machotara na hizbu tunawapeleka kwao Oman.
 
Yote haha ni Kwasababu ya dini, dini mbili tofauti haziwezi kuchangamana!
 
narejea maombi ya kakobe , mambo ya wanzanzibar yanajadiliwa na wanzanzibar , mambo ya Tanganyika yanajadiliwa na Nani !? jibu ni hayupo !! Sasa huu muungano ulikuwa niwa nchi ipi na ipi Kama Tanganyika haionekani na Wala mambo yake hayaonekani !!
Kama Tanganyika haiopo , ilienda wapi !? na tuliambiwa ni muungano wa nchi 2!? kwanini Zanzibar ndo inapewa fursa ya kujadili mambo yake huko visiwani na wakati nchi ya Tanganyika haionekani popote kupewa fursa ya kujadili mambo yake , yaani iwe na bunge lake Kama ilivyo Zanzibar!!?
Hili Giza ndo linatumiwa kuhujumu maliasili za Tanganyika ,kwa kuwa hayupo wa kujadili kuhusu Mali za Tanganyika ,na Tena nchi yenyewe ilishayeyushwa kiaina aina !!
 
Tatizo ni mfumo wenyewe wa Muungano ulivo Tanganyika wameivalisha koti la muungano kwa hiyo Tanganyika ndio Muungano
 
narejea maombi ya kakobe , mambo ya wanzanzibar yanajadiliwa na wanzanzibar , mambo ya Tanganyika yanajadiliwa na Nani !? jibu ni hayupo !! Sasa huu muungano ulikuwa niwa nchi ipi na ipi Kama Tanganyika haionekani na Wala mambo yake hayaonekani !!
Kama Tanganyika haiopo , ilienda wapi !? na tuliambiwa ni muungano wa nchi 2!? kwanini Zanzibar ndo inapewa fursa ya kujadili mambo yake huko visiwani na wakati nchi ya Tanganyika haionekani popote kupewa fursa ya kujadili mambo yake , yaani iwe na bunge lake Kama ilivyo Zanzibar!!?
Hili Giza ndo linatumiwa kuhujumu maliasili za Tanganyika ,kwa kuwa hayupo wa kujadili kuhusu Mali za Tanganyika ,na Tena nchi yenyewe ilishayeyushwa kiaina aina !!
Wale wote wanaolalamikia Mikataba mibovu baina ya Serikali ya Tanzania na makapuni Ni hivi Mkataba wa Muungano ndio Mkataba mbovu kuliko Mikataba yote Tanzania ni kauli ya Makoma wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar mhe Othman Masoud Othman aloitoa jana mkwajuni kaskazini unguja
 
Back
Top Bottom