PreGE2025 Rais Samia Awaahidi Wananchi Uchaguzi Mkuu Utakuwa Wa Amani, Huru, na Wa Haki, Kama Ulivyokuwa wa Serikali za Mitaa 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,934
Hotuba ya Rais Samia, jana usiku, pamoja na mambo mengine, aliongelea kuhusu uchaguzi mkuu wa 2025, akisema kuwa Serikali yake itahakikisha uchaguzi mkuu wa 2025 utakuwa wa amani, huru na wa haki. Maneno haya pia Rais Samia aliyatamka mwaka 2024 wakati akiwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kwa hiyo tukitaka kujua maana ya amani, kadiri ya uelewa wa Rais wetu Samia, tuangalie amani iliyokuwepo kwenye uchaguzi wa 2024. Kuua baadhi ya wagombea wa upinzani. Mifano michache ni kuwa kule Singida mgombea wa nafasi ya umwenyekiti wa kitongoji kupitia CHADEMA, aliuawa na askari. Kule Mbeya aliuawa kada wa CHADEMA. Kwa Rais Samia, hiyo ndiyo amani, ndiyo anayoipigania iendelee na kwenye uchaguzi mkuu 2025.

Watanzania walishudia nchini kote, kwenye uchaguzi uliosimamiwa na na wizara ya Mchengerwa, wagombea wa upinzani kwa maelfu wakienguliwa na wasimamizi wa uchaguzi ambao ni waajiriwa wa TAMISENI. Na baadhi ya maeneo wagombea wa kupitia vyama vya upinzani, hata wale kwa udhahiri kabisa walionekana kushinda, lakini TAMISEMI kwa kutumia jeshi la polisi walilazimisha wagombea kupitia CCM ndiyo watangazwe. Kule mkoa wa Rukwa mgombea kupitia CHADEMA, aliyepata kura 960, hakutangazwa kama mshindi, akatangazwa mgombea kupitia CCM aliyepata kura 600, chini ya mtutu wa bunduki wa polisi wakiongozwa na RPC. HIYO NDIYO MAANA YA UCHAGUZI HURU NA HAKI, KWA KADIRI YA UELEWA WA RAIS SAMIA.

TUJIULIZE:
Kama maneno aliyoyatumia Rais Samia mwaka 2024 kuhusiana na uchaguzi wa 2024, ni yale yale ameyatumia jana kwaajili ya uchaguzi mkuu wa 2025; Tujiulize, kama Mchengerwa ambaye ni waziri wa TAMISEMI, watendaji wake ndio waliosimamia uchaguzi wa 2024, na ndio hao hao watakaosimamia uchaguzi wa 2025; Tujiulize, kama Polisi ni wale wale waliosimamia maovu mbalimbali kwenye uchaguzi wa 2024, ndio hao hao watahusika kwenye uchaguzi wa 2025; kwa nini tutegemee mambo yatakuwa tofauti kwenye uchaguzi mkuu wa 2025?
Mazingira ni yale yale, watu ni wale wale, maneno ni yale yale, lazima uwe huna akili kabisa, kuamini kuwa uchaguzi wa 2025 utakuwa tofauti na ule wa 2024.

Mchengerwa, kama wizara yake ingekuwa imefanya tofauti kabisa na matarajio ya Rais Samia, mara baada ya uchaguzi wa 2024, angeondolewa kwenye nafasi yake, kwa sababu ameharibu. LAKINI kitendo cha Rais Samia kumwacha Mchengerwa kwenye nafasi ile ile, ina maana ama Rais Samia alifurahishwa na kuridhishwa sana na yale ambayo TAMISEMI walifanya kwenye uchaguzi wa 2024, AMA Waziri Mchengerwa alitekeleza kikamilifu maagizo na maelekezo ya Rais Samia ya namna uchaguzi wa 2024 alitaka uwe.

NB: Juzi tumeshuhudia kwa uwazi kabisa jeshi la polisi likifanya kazi kama kikundi cha kigaidi, kukamata watu, kuwapiga na kwenda kuwatupa porini. Kama waliokamatwa na polisi wangekuwa na hatia, polisi wangewakamata na kuwapeleka mahabusu na kisha kuwafungulia mashtaka. LAKINI kitendo cha kuwapiga na kwenda kuwatupa porini, inamaanisha wahusika hawakuwa na hatia, bali polisi inachofanya ni ku-terrorize watu. Je, jana usiku mlimsikia Rais Samia akitoa kauli yoyote kulaani matendo hayo ya uvunjaji wa katiba ya nchi yanayofanywa na jeshi la polisi?

Eneo la mahakama, ni mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka, na ndiyo yenye mamlaka ya kutoa maelekezo kwa yeyote anayekuja kushiriki kusikiliza kesi, lakini jeshi la polisi kwa uharamia mkubwa limewakamata watu eneo la mahakama na kwenda kuwapiga, na kuwatupa maporini, je, mmemsikia Rais Samia jana kwenye hotuba yake akikemea uharamia huo wa polisi?

Tumesikia jinsi magereza inavyomnyima haki za msingi za kisheria na kikatiba mh. Lisu, je, mlimsikia Rais Samia akiyakemea mambo hayo?

Kutokukemea na kuyaacha yaendelee, inamaanisha haya yote, kwa Rais Samia ndiyo amani na ndiyo haki na uhuru anaouongelea kuwa Serikali yake itajitahidi inausimamia kuelekea na wakati wa ucjaguzi mkuu wa 2025.

CHA KUJIULIZA:
Je, na sisi wananchi, huu uharamia wote unaofanywa tunaona ndiyo haki? Kama sivyo, bado tuna sababu ya kuziamini kauli za Rais Samia? Kwa sababu ya nafasi yake, naweza kushindwa kusema ni mwongo, labda tuseme Rais Samia ama hasemi ukweli, au ana tafsiri tofauti kuhusu amani, haki na uhuru!! kwani kauli zake wakati wote huwa ni kinyume kabisa cha matendo ya Serikali yake. Tunahitaji Kiongozi mkweli wa nafsi ambaye anatembea juu ya maneno yake.

Mungu wabariki watanzania ambao licha ya dhuluma kubwa ya haki zao, wameendelea kuwa wavumilivu, licha ya watawala kufanya jitihada kubwa ya kuwalazimisha wananchi kuvunja amani kutokana na yale wanayoaatendea, ambayo ni wazi yapo kinyume cha sheria na katiba ya nchi yetu.
 
CHADEMA mpaka wajambe cheche laana ya Magufuli inawatafuna na Samia wao watamwagana damu sana tu.
 
Rais Samia ni muongo bila katiba mpya na tume huru, uchaguzi hauwezi kuwa huru chini ya utawala wa serikali ya ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…