kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imempitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mwaka 2022 hadi 2027 na jina lake litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu December 07 kwa ajili ya kupigiwa kura.

Katika mkutano huo pia umeridhia Makamu Mwenyekiti anayemaliza muda wake Ndugu Abdulrahman Kinana kugombea tena miaka 5.

1670335547196.png
 
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imempitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mwaka 2022 hadi 2027 na jina lake litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu siku ya kesho December 07 kwa ajili ya kupigiwa kura.

Na kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Halmashauri Kuu imempitisha Kinana kuwa Mgombea kwa kiti cha Makamu Mwenyekiti Bara na Dkt. Hussein Mwinyi kwa upande wa Zanzibar.

Taarifa hiyo ya chama imetolewa na Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka leo December 06, 2022 wakati akitoa taarifa ya kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM December 07 na 08 jijini Dodoma.
 
Hakika mama ameikamata nchi, anakubalika ,anapendwa, na Sasa anakisuka chama akiyaondoa magugu na kuweka ngano.

Viva mama viva.
Hatujamaliza CCM .... Mlete Samia....Mlete Samia.....Mlete Samia
 
CCM imemteua Rais Samia Suluhu Hassan kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana ameteuliwa kuwa mgombea wa Makamu wa Mwenyekiti Tanzania Bara. Dr. Hussein Ally Mwinyi ameteuliwa kuwa mgombea wa Makamu Mwenyekiti Tanzania Zanzibar ambaye atamokea Dr. Shein ambaye anakamilisha uongozi wake Desemba 7, 2022

Halamashauri kuu ya CCM imewateua wanachama 251 kugombea nafasi 15 za ujumbe wa Halmashauri kuu Tanzania Bara. Pia wanachama 123 wa kutoka Tanzania Zanzibar ili kugombea nafasi 15 za ujumbe wa halmashuri kuu kwa Tanzania Zanzibar.
 
Tunasonga kwenda 2025

WeMarchTo2025
WeParadeReadyTo Defend CCM
 
CCM haina mvuto ukizingatia sasa wazanzbar walio wachache ndo wapo kwenye sehemu nyeti.Upinzani wangekuwa makini wangekuwa popular sana. Sema nao hawaeleweki.Eti Dr Samia.
Kila zama na kitabu chake.
Hushangai mikutano mingi kupelekwa Chato na Zanizbar?

Atayekuja naye atafanya hivo hivo maana wenzake washaanzisha
 
Kwenye watu milion 60 majina 200 yatapigiwa kura,kwenye watu million 2 majina 123 yatapigiwa kura.
Hivi kwa nini Zanzibar isiwe mkoa ?
Yaani Nyerere alizidiwa akili na Karume kwa kweli.Si kwa muungano wa usio na uwiiano kabisa.
 
Back
Top Bottom