Uteuzi: Rais ateua Makatibu Wakuu Watatu na Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,294
17,137
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewateua wafuatao:-
i) Amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

ii) Amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS). Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi
wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (CASSOA).
Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila
ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

iii) Amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa
ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge na Uratibu); na

iv) Amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Uteuzi huu umeanza tarehe 12 Juni, 2023.
Screenshot_20230613-181031~2.jpg
 
Mbona hii inakanganya kidogo mhandisi wa mambo ya anga na Barabara wap na wapi kwanini asitolewe mtu ndani ya taasisi (Tanroads) anaeifahamu fika maana CEO lazima ajue miradi yote ya kimkakati na ambayo sio ya kimkakati pia aweze kubuni mingine pia napata shida kidogo na huu uteuzi wajuvi watakuja kuelezea kidogo.
 
Back
Top Bottom