Sioni mapendekezo ya tume ya taasisi za Haki Jinai yakifanyiwa kazi

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,505
Raisi aliunda tume nazania iliongozwa na Wabobezi wakina Jaji mstafu,yule IGP mstafu Said Mwema na wengineo.

Tume ilikudanya maoni na ikaandas report na kukabidhi,na tukaambiwa kuna baadhi ya mapendekezo hayahitaji kupelekwa Bungeni bali ni ya kufanyia kazi papo kwa hapo.

Ile tume maoni mengi yalikuwa juu ya Jeshi la polisi hasa kwenye Kubambikia watu kesi,kutesa watuhumiwa,kuto pelekea watuhumiwa mahakamani kwa wakati na Mambo ya Rushwa.

Sasa ni miezi kadhaaa sasa sijaona badiliko lolote pale Polisi.Ubambikiaji wa kesi uko pale pale. Polsi kutumika kuko pale pale rejea ishu ya Gekuli alivyo litumia Jeshi la Polisi kwa manufaa yake binafisi. Kuto paleke watuhumiwa mahakani kwa wakati kuko pale pale,kutesa watuhumiwa kuko pale pale.

Rushwa iko pale pale, sasa hii tume ilikuwa na maana gani? si bora hizo pesa zingeenda hata kujenga matundu ya vyoo?

Unatumia pesa mingi kufanya kazi ambayo mwisho wa siku,haifanyiwi kazi inakuwa ni hasara kwa Taifa.
 
Back
Top Bottom