BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Rais Samia Suluhu Hassan amemaliza mgogoro wa ardhi yenye ukubwa wa ekari 7,495.74 uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu kati ya vijiji vya Kata ya Kingale, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Gereza la King'ang'a.

Mgogoro huo umetatuliwa baada ya kiongozi huyo kuagiza eneo lenye ukubwa wa ekari 3,272.4 libaki kwa wananchi kwa shughuli za kilimo, mifugo na kiuchumi na eneo lililobaki lichukuliwe na Magereza.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, aliwasilisha jana taarifa hiyo kwa niaba ya Rais Samia mbele ya wananchi na viongozi wa kata hiyo ambayo ardhi yake inasifika kuwa na rutuba inayofaa kwa shughuli za uzalishaji.

"Ardhi yote ni mali ya serikali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipofika hapa alifikisha hili jambo kwa Mheshimiwa Rais aamue na Rais Samia ametoa suluhu kwa Wanakingale," alisema Senyamule.

Alisema Rais Samia ameagiza ndani ya mwezi mmoja, watu wa ardhi waonyeshe utaratibu wa maeneo yaliyogawanywa, yapimwe na kuweka alama zinazoonekana kwa kila mmoja.

Vilevile, aliwasihi wanavijiji na Magereza kutunza mipaka na kuzuia mwingiliano wa matumizi kwa kuwa wananchi wapo upande wa Bonde linalofaa kwa umwagiliaji.

"Wizara ya Kilimo mfanye utaratibu wa kujenga mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji na mifugo pia, mjenge majosho kwa ajili ya kuosha mifugo ya wananchi," aliagiza Senyamule.

Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi na Magereza kutumia fursa hiyo na miundombinu itakayojengwa kufanya shughuli zenye kuleta maendeleo.

Mbunge wa Kondoa Mjini, Ally Makoa, alimshukuru Rais Samia kwa uamuzi alioufanya kuwa umefuata mapendekezo waliyoyatoa kwake ya kupatiwa eneo kutoka kwenye mpaka wa Magereza.

Vilevile, Ally alimshukuru Rais Samia kwa kuwapelekea wataalamu kutoka wizarani kwa ajili ya kujenga miundombinu kwenye eneo hilo.

NIPASHE
 
Rais Samia amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu zaidi ya miaka 30 dhidi ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74. mgogoro huo ni kati ya wananchi wa kijiji cha Kingale kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya kondoa na Gereza la King'ang'a, Katika mgogoro huo Rais Samia Suluhu amezingatia mahitaji ya wananchi maana eneo hilo linafaa kwa uzalishaji hivyo hivyo amewakabidhi wananchi eneo hilo ili walitumie katika uzalisha.


Watanzania tunabahati sana kuwa na Rais Samia Suluhu imagine zaidi ya miaka 30 mgogoro ulishindwa kutatuliwa lakini Rais Samia Suluhu ametatua mgogoro huu ndani ya miaka 2 tu ya utawala wake kweli naamini Tanzania ni salama na Samia.
 
Back
Top Bottom