Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro Amegawa TV Kwenye Vijiwe na Mabunge ya KAHAWA Wilayani Ngara ili Wananchi Waendelee Kupata Taarifa Muhimu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro Amegawa TV Kwenye Vijiwe na Mabunge ya KAHAWA Wilayani Ngara ili Wananchi Waendelee Kupata Taarifa Muhimu

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mh. Ndaisaba George Ruhoro anapenda kuujulisha umma na Wananchi wa Jimbo la Ngara kuwa anaendelea na Zoezi la ugawaji wa Television (TV) kwenye vijiwe/mabunge ya kahawa yaliyopo Wilayani Ngara.

Lengo kubwa ni kuwawezesha Wananchi kupata taarifa za Mambo mbalimbali yanayoendelea Duniani na Nchini, pamoja na kuwafanya waone kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan .

Kwa sasa Mbunge wetu amegawa TV Kwenye Kijiwe cha Kahawa Ngara mjini na muda si mrefu atagawa Rulenge, Junction na Benaco.

TV itafanya watu wengi kuvijua vijiwe vya kahawa, Kuhudhuria vikao vya kujadili mambo mbali mbali ya Maendeleo na kubwa kuliko yote, kuwafanya Watanzania kuanza kunywa Kahawa ambayo wanaizalisha wenyewe na hivyo kutengeneza soko la Ndani la wanywaji wa Kahawa.

Mbunge wa Wanangara hapoi, hategemei kupoa, kasi ni ileile. Watu wanaseme “ KEEP" BOMBING ”

Sarah Keneth
Kaimu Katibu wa Mbunge
WhatsApp Image 2023-12-20 at 11.56.33.jpeg
 
Wananchi kushinda Vijiweni ni dalili za ukosefu wa Ajira solution sio kuwawekea TV ni kubuni miradi itakayozalisha Ajira.

Ngara ina Nickel na Cobalt nyingi na imethibitishwa na ndio Black Gold mpya kwanini Wananchi washinde vijiweni huku uchumi wa Mabilioni ya Dola wameukalia.
 
How low of him? Cheap politics
Kwanza thread haina content nzuri mwandishi unasema mbunge kanunua TV wilaya nzima kumbe tv Moja tu.

Pili Kuna baadhi ya siasa ukifanya zinaonyesha ni jinsi gani unawadharau wananchi wako

Tatu kijiwe Cha kawaha ni kwa ajili ya kuongea mambo ya kiutamaduni na kijamii sio kijiwe Cha TV kwa ninachojua Mimi labda huko ngara kwenye vijiwe vya kahawa ndo wanaangalia TV sababu hawana majumbani

Nne. Mwandishi ulieandika hiki Rudi shule ukajifunze ubunifu ili uvutie kwa wasomaji sio kuandika tu kama unamuandikia demu wako
 
Back
Top Bottom