Ngara: Walimu Wakuu wa Shule za Wilaya ya Ngara, Wachangishana Fedha kwaajili ya Fomu ya Urais ya Rais Samia 2025 na kwaajili ya Mbunge Ndaisaba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Walimu wakuu wa Shule mbalimbali za Wilaya ya Ngara kwa niaba ya Walimu wote wa Wilaya ya Ngara wamekutana Katika Kikao maalumu cha Wakuu wa Shule ambapo kwa kauli Moja wameonyesha kuridhishwa na Utendaji Kazi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan na Kuahidi kuwachukulia Form za Kugombea nafasi zao.

"Kila Mwalimu Mkuu atatoa Shilingi 10,000. Asilimia 60 ya makusanyo itachangia Fomu ya Urais ya Dkt. Samia Suluhu Hassan na Asilimia 40 itachangia fomu ya Ubunge ya Ndaisaba George Ruhoro katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025" - Mwalimu Allen Deogratius, Mwenyekiti CWT Wilaya ya Ngara.

"Walimu Wilaya ya Ngara walikuwa hawajapandishwa madaraja kwa kipindi kirefu, lakini kupitia Serikali sikivu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan walimu wameweza kupandishwa madaraja, hivyo wanamshukuru sana Rais Samia" - Mwal. Allen Deogratius, Mwenyekiti CWT Wilaya ya Ngara.

Wakuu hao wa Shule wakiongozwa na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Ngara Mwalimu Allen Deogratias Marton wameahidi kwa kauli Moja kuwa mabalozi wa Serikali ya Awamu ya Sita Katika maeneo yote watakayofika ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walimu hao pia wametuma Salamu kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Kumuomba awarejeshee Jembe lao Ndaisaba Ruhoro ambaye amekuwa kimbilio la walimu wa Ngara katika kupigania Masalahi yao hususani suala la Kikokotoo.

Akiwahutubia Walimu Wakuu hao kwa niaba ya Walimu wote wa Wilaya ya Ngara, Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amewashukuru walimu hao kwa Imani kubwa waliyonayo kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Lakini pia, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amewashukuru walimu hao kwa Upendo Mkubwa waliomuonyesha na akaahidi kuwapigania stahiki zao kadri ya uwezo wake wote.

Pamoja na hayo Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amegawa Mitungi ya gesi kwa Shule zote za Serikali Katika ngazi ya Msingi na Sekondari.


#SamiaTena2025
#NgaranaNdaisabaDamDam
 

NGARA: WALIMU WAKUU WA SHULE WILAYA YA NGARA WATANGAZA KUMCHUKULIA FORM YA URAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN NA MBUNGE WA NGARA MHE. NDAISABA GEORGE RUHORO.

Walimu wakuu wa Shule mbalimbali za Wilaya ya Ngara kwa niaba ya Walimu wote wa Wilaya ya Ngara wamekutana
Hivi wakichangiahana kwa ajili ya Mbowe au Lissu watabaki ofisini kweli?
Upuuzi mkubwa lulazimisha kada za kitaaluma kufanya siasa mahala pa kazi
 
Kwa hizi akili ni halali hata elimu yetu ikose viwango kimataifa kama walimu ndo hawa wa kujikomba kwa wanasiasa na ikifika may mosi walie changamoto zao hazitatuliwi.

Shenz sana hii nchi sio leo kupiga hatua!
 
Hivi walimu wetu ni kweli hamna akili kiasi hiki??? Sitaki kuamini. Ualimu ni moja ya Tasnia iliyokuwa inaheshimika sana enzi hizo, ila mkiendelea na akili za namna hii sidhani kama kwa miaka ijayo kuna mtu atatamani kuitwa mwalimu
 
Kiukweli tunawakati mgumu kama taifa

Hizo pesa busara wangelizielekeza hata kwenye matundu ya vyoo wangalionekana wa maana saana

Hakuna Jimbo lipo hoi kihuduma za jamii kama Jimbo la NGARA lakini kwa kuwa labda wao vipaumbele vyao ni pombe tena za kienyeji sioni ajabu
 
Nyongeza za mishahara,madarasa mazuri kujengwa,increment kurudishwa,semina za walimu kurudi,vishikwambi kwawalimu wote,kutolewa vitisho hakupo Tena...yawezekana vituhivi vimewavutia walimu kumpenda sana Samia. Enzi za mwendazaka walimu walisiginwa saaana hivyo labda furaha imewazidiaa wakajisahauu!!
 
Back
Top Bottom