Rais Samia anasifiwa kupita kiasi

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,102
2,717
Kila siku utasikia,"Rais kajenga barabara hapa:Rais katujengea zahanati."
Watu wanamwabudu Rais,na yeye hafanyi kitu chochote kuwazuia. Haya ndiyo mambo yanayomchukiza Mungu.

Kwa ajili Uchaguzi Mkuu unakaribia,acha watu wanisifie zaidi na zaidi.

Magufuli hakuwa anasifiwa namna hii; ingawa watu walikuwa wanasema huyu mtu kaongoza nchi siku kidogo tu,lakini nchi yetu imepata maendeleo kama Ulaya.

Marekani utasikia mara moja moja wanasema,"The Biden Education Programme,au The Biden Housing Project,lakini hii ni kwa sababu Kuna strong Opposition Party,na wanataka kutofautisha mambo.

Kikwete mara moja tu walikuwa wanaongea kuhusu " mamilioni ya Kikwete". Lakini kila siku tunasikia kuhusu " mamilioni ya Samia".

Hata ukimpa mtoto mdogo peremende,lazima uhakikishe kwamba yule mtoto anamsifu Mungu.

Kwa hiyo wajihadhari hawa watu wote wanaotaka kuitwa "superstar"
 
Huu utoaji wa sifa zilizopitiliza kwa mkulu badala ya kutoa pongezi za kawaida kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake ya kikatiba, zilianza kutollewa wakati wa utawala wa JPM. Yaani kila jambo lililofanywa na serikali lilikuzwa na kupambwa mno, ili liwe na "personal attribution" kwake.

Sifa, heshima, mamlaka, na utukufu wote alipewa yeye tu, kwa kile kilochooneka kuwa ni fadhila anazozitoa kwa wale wanaonekana kupendezwa naye ama kupata kibali mbele ya macho yake. Katika siku hizo, ole wao ulikuwa kwa wapinzani wa maono yake! Walikiona cha mtema kuni!

Pale madhaifu ya serikali ama taasisi ya urais yanapotokea, rais anakingiwa kifua, wanaolaumiwa ni wasaidizi wake wa karibu kuwa ndiyo wamemshauri vibaya. Wana CCM wanajitoa ufahamu kuwa maamuzi ya Baraza la Mawaziri huendeshwa kwa uwajibikaji wa pamoja.

Katika siku za uhai wake, Mzee Mkapa aliwahi kukemea sifa kama hizi zinazotolewa kwa rais kwa njia unafiki ama kujipendekeza. Aliwaasa kuwa ni vyema wana CCM, hasa mawaziri wanapoongelea juhudi kubwa inayofanywa na serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo kupitia kodi zao, basi wapeleke pongezi zao kwa serikali inayoundwa na chama tawala chini ya uongozi wa rais aliyepo madarakani.
 
Kila siku utasikia,"Rais kajenga barabara hapa:Rais katujengea zahanati."
Watu wanamwabudu Rais,na yeye hafanyi kitu chochote kuwazuia. Haya ndiyo mambo yanayomchukiza Mungu.

Kwa ajili Uchaguzi Mkuu unakaribia,acha watu wanisifie zaidi na zaidi.

Magufuli hakuwa anasifiwa namna hii; ingawa watu walikuwa wanasema huyu mtu kaongoza nchi siku kidogo tu,lakini nchi yetu imepata maendeleo kama Ulaya.

Marekani utasikia mara moja moja wanasema,"The Biden Education Programme,au The Biden Housing Project,lakini hii ni kwa sababu Kuna strong Opposition Party,na wanataka kutofautisha mambo.

Kikwete mara moja tu walikuwa wanaongea kuhusu " mamilioni ya Kikwete". Lakini kila siku tunasikia kuhusu " mamilioni ya Samia".

Hata ukimpa mtoto mdogo peremende,lazima uhakikishe kwamba yule mtoto anamsifu Mungu.

Kwa hiyo wajihadhari hawa watu wote wanaotaka kuitwa "superstar"
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni 🐒

ili kutofatisha na wengine, rais comrade Dr SSH anapiga kazi na for sure ana mipango na ana malengo na waTanzania,

ukweli usemwe,
kiuchumi Dr.SSH yupo mstari wa mbele kabisa kuupaisha,
kisiasa Dr SSH yupo mstari wa mbele sana kuimarisha demokrasia,

kijamii Dr.SS yupo mstari wa mwanzo kabisa kuhakikisha miundombinu na huduma za jamii zinawafikia waTz wote kwa uhakika na zinawatisheleza 🐒

anaachaje kusifiwa kila uchwao 🐒

na vip wale wa mihemko na malalamiko kwa kila lililo jema kwao baya 🐒
 
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

ili kutofatisha na wengine, rais comrade Dr SSH anapiga kazi na for sure ana mipango na ana malengo na waTanzania,

ukweli usemwe,
kiuchumi Dr.SSH yupo mstari wa mbele kabisa kuupaisha,
kisiasa Dr SSH yupo mstari wa mbele sana kuimarisha demokrasia,

kijamii Dr.SS yupo mstari wa mwanzo kabisa kuhakikisha miundombinu na huduma za jamii zinawafikia waTz wote kwa uhakika na zinawatisheleza

anaachaje kusifiwa kila uchwao

na vip wale wa mihemko na malalamiko kwa kila lililo jema kwao baya
Mwingine huyu hata usingizi hapati, akilala anaota kusifia, akiamka ni kusifia tu mchana kutwa, hii tabia inaweza kuwaathiri kisaikolojia, iacheni kwa usalama wa afya zenu.
 
uvivu ni adui mkubwa sana kwa ujenzi wa Taifa 🐒

Amka ufanye mazoezi ya mwili kidogo uwahi ibadani,

upo unahemka tu na kughadabishwa na Ukweli wa mambo ya Dr SSH🐒
.
au kibando kina expired as soon as possible 🤣

weka kanamba bas ubustiwe
 
Kila siku utasikia,"Rais kajenga barabara hapa:Rais katujengea zahanati."
Watu wanamwabudu Rais,na yeye hafanyi kitu chochote kuwazuia. Haya ndiyo mambo yanayomchukiza Mungu.

Kwa ajili Uchaguzi Mkuu unakaribia,acha watu wanisifie zaidi na zaidi.

Magufuli hakuwa anasifiwa namna hii; ingawa watu walikuwa wanasema huyu mtu kaongoza nchi siku kidogo tu,lakini nchi yetu imepata maendeleo kama Ulaya.

Marekani utasikia mara moja moja wanasema,"The Biden Education Programme,au The Biden Housing Project,lakini hii ni kwa sababu Kuna strong Opposition Party,na wanataka kutofautisha mambo.

Kikwete mara moja tu walikuwa wanaongea kuhusu " mamilioni ya Kikwete". Lakini kila siku tunasikia kuhusu " mamilioni ya Samia".

Hata ukimpa mtoto mdogo peremende,lazima uhakikishe kwamba yule mtoto anamsifu Mungu.

Kwa hiyo wajihadhari hawa watu wote wanaotaka kuitwa "superstar"
Kuna cku nliwakuta vjana flani wakinywa "banana" zao baada ya kutoka porini walikoenda kukata majani ya ng'ombe wakixema "namshukuru mama, nimefikisha mzigo wa watu salama", na mwenzao akaitikia "hata mimi"!! inatia kinyaa-hata wenye akili zao wanasujudu hadharani ...dah!
 
uvivu ni adui mkubwa sana kwa ujenzi wa Taifa

Amka ufanye mazoezi ya mwili kidogo uwahi ibadani,

upo unahemka tu na kughadabishwa na Ukweli wa mambo ya Dr SSH
.
au kibando kina expired as soon as possible

weka kanamba bas ubustiwe
Mimi nimeshaamka sio wa kuamshwa na chawa, hiyo namba uweke wewe unaeimba mapambio ya Samia zaidi ya hayo unayoenda kuimba huko ibadani.
 
Tatizo wabongo wasahaulifu sana, sifa zisipomwagwa mnasahau mapema. Mkiachiwa tu free hamchelewi kwenda kupuyanga hovyo kwenye box la kura.
Kwa hiyo wako sahihi kuwakumbusha mara kwa mara kila inapobidi
IMG-20240224-WA0026.jpg
 
Kila siku utasikia,"Rais kajenga barabara hapa:Rais katujengea zahanati."
Watu wanamwabudu Rais,na yeye hafanyi kitu chochote kuwazuia. Haya ndiyo mambo yanayomchukiza Mungu.

Kwa ajili Uchaguzi Mkuu unakaribia,acha watu wanisifie zaidi na zaidi.

Magufuli hakuwa anasifiwa namna hii; ingawa watu walikuwa wanasema huyu mtu kaongoza nchi siku kidogo tu,lakini nchi yetu imepata maendeleo kama Ulaya.

Marekani utasikia mara moja moja wanasema,"The Biden Education Programme,au The Biden Housing Project,lakini hii ni kwa sababu Kuna strong Opposition Party,na wanataka kutofautisha mambo.

Kikwete mara moja tu walikuwa wanaongea kuhusu " mamilioni ya Kikwete". Lakini kila siku tunasikia kuhusu " mamilioni ya Samia".

Hata ukimpa mtoto mdogo peremende,lazima uhakikishe kwamba yule mtoto anamsifu Mungu.

Kwa hiyo wajihadhari hawa watu wote wanaotaka kuitwa "superstar"
Awamu hii watu wanaiba sana fedha na hawafanuwi chochote ndo manan Kila mwizi anamusifia
 
Mkuu
Siku hizi viongozi wetu ni waraibu ama mateja wa kupenda kusifiwa. Ukitaka teuzi wewe inua sauti yako tamka imposibilities za mkubwa kuwa kafanya hakika atakupa umiliki kwenye miliki yake
 
Awamu hii watu wanaiba sana fedha na hawafanuwi chochote ndo manan Kila mwizi anamusifia
wakosoaji hawaelewani, hawaaminiani, wamegawanyika, ni mahasimu na maadui wakubwa miongoni mwao na kwahivyo kubwekabweka kwao ni kelele za kawaida tyuu, zinakuepo zinaisha, hamna mahali wanaenda, hamna kitu watafanya wala kufanyika 🐒

ni sawa tu na vita vya panzi anaefurahika na kunufaika ni kunguru...🐒

sasa panzi kumvimbia kunguru si ni yaleyale tyuuuu 🐒
 
Tuna manafiki tele hii nchi jitu linaomba Hela yakula nduguze maskini LAKINI linakwambia mama anaupigia mwingi! Mama huyo anawaambia wateule wake akiwemo mkwewe wale lkn wasivimbiwe...
Serikali haipongezwi anapongezwa mtu yaani umeme ukikatika waziri na tanesco wanatukanwa LAKINI umeme ukiwepo anapongezwa rais binafsi kuwa anaupigia mwingi!!!
Nchi ikikosa elimu Bora ni majanga matupu
 
Niwakumbushe kitu tu kwamba chimbuko la praise team.

Sote tuliohai tunatambua kwamba siku zote serikali inawajibika kwa raia wake na inaeleweka vyema kupitia chama tawala kwa awamu ya kwanza hadi ya 3 serikali ilikuwa imara ila ilipofika awamu ya 4 mambo yalibadilika kwa namna flani ikawa viongozi wamefocus zaidi kwenye matumbo yao kuliko mahitaji ya raia ikafikia stage kila mdau ni mpiga dili au dalali wa kuuza rasilimali zetu kwa wageni kujilimbikizia utajiri tu. Haki za wanyonge kuporwa na wenye mali zikakithiri. Kiufupi taswira ya chama ikachafuka sana na hakuna mtu alikuwa anataka kuisikia CCM so ilibidi waje na masterplan mpya.

Katika kikili kakara ndio akapitakana Magufuli maana ndie angalau alikuwa na haiba ya kukubalika na raia. Kwa kua watu walikuwa na chuki sana na chama ndipo Magu akaamua kujiposition yeye kama yeye ili kuleta relevance kwa chama. Ndio mfumo wa praise team ulianzia hapo. Lengo lilikuwa kuleta relevance ya uongozi wa CCM ili raia nyongo ziwapungue maana walikuwa washaichoka mno na ilibaki nukta tu waipe chadema nchi.

Magu alikubalika na kuirudisha CCM kwenye chart baada ya kuamua kutawala kinyume na awamu ya 4 kabisa kutokana na mfumo wake wa ku favour wananchi zaidi kuliko wanasiasa na matajiri. So wengi walimsifia sana na alikuwa akijinadi yeye kama kiongozi mkuu wa serikali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom