Rais Samia anasifiwa sana, hawaju wateule wake kama Jeneali Ulimwengu anavyodai?

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Mimi ni mpenzi wa harakati za Jenerali Ulimwengu katika utetezi wake wa demokrasia, utawala bora na haki za binadamu.

Ninachofurahia kuhusu yeye ni kuwa katika kipindi ambacho wengi walinywea na kurekebisha maoni yao yaendane na mazingira ya utawala uliokuwepo katika awamu ya tano, yeye aliendelea ukweli anaoumini.

Kingine ambacho napenda kuhusu Ulimwengu ni kuwa hajihariri mawazo yake ili tu kupendezesha watu. Katika kumfuatilia, yapo mambo ambayo akiyasema watu humtukana sana, ikiwemo zile nyakati anapoeleza udhaifu wa utawala uliopita wa awamu ya tano. Hata hivyo, Ulimwengu amekuwa hajali matusi.

Mimi nawajua wanasiasa wengi, wakiwemo hata wasomi wa ngazi za uprofesa na udaktari wa falsafa, ambao misimamo yao hubadilika kutokana na mazingira na nyakati. Hawa ni binadamu wabaya kabisa. Ingekuwa bora kwao kunyamaza kuliko kusema wasiyoyaamini kwani huo ndio unafiki 101. Kama unasema kinyume na mawazo yako ya awali, bais iwe kwa sababu kutokana na ushahidi mpya ulioupata unmebadili msimamo na unaamini tofauti na ulivyoamini awali.

Kwa hayo niliyoyataja, Jenerali Ulimwengu, analiishi jina lake na kulitendea haki ingawa nachelea pia nisimsifu sana. Nahofia kuwa nisije kupitiliza kumsifu hali ya kuwa kwani yeye mwenyewe hivi karibuni kasema hapendi kusikia watu wanasifiwa sifa za kupitiliza.

Hata hivyo, Kwenye hili la sifa, yeye kukariri mara kwa mara kauli yake ya kutopenda kusikia rais anasifiwa nadhani anaweza kuwa amepotoka kwa namna fulani. Binafsi nimewahi kumsikia mara mbili, kwanza kwenye kipindi chake cha Jenerali Ulimwengu Exclusive on The Chanzo kilichorushwa kupitia YouTube ambapo alikuwa akitoa maoni juu ya mada isemayo: Siasa za Tanzania: Tulikotoka na Tunapoelekea.

Jenerali alitoa maoni kama hayo pia katika Kumbukizi ya Maalim Seif Shariff Hamad ambapo alinukuliwa akisema: “Mimi inanichosha kusikia sifa za Rais kila dakika. Rais ni mtu mwema, nadhani; lakini sio lazima tukae tunamsifu, tunamsifu, tunamsifu. Kama huna critical thinking (fikra tunduizi) juu ya mkuu wako na kila siku ni kumsifu, naanza kuwa na shaka kuwa hata akikosa utakuwa unamsifu tu,” na akafafanua kuwa kufanya hivyo ni kumcheza shera.

Tahadhari ya mzee Ulimwengu ni nzuri sana, lakini sidhani kama kinachofanywa leo na viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake ni kigeni sana.

Kwa kumbukumbu yangu, marais wote walisifiwa sana; na katika wote aliyesifiwa sna ni mwalimu Julius Nyerere ambaye mzee Ulimwengu anadai kuwa alikuwa hapendi kusifiwa, jambo ambalo sikubaliani nalo. Kiukweli, kama Ulimwengu alivyochoka kusikia aliyopo anasifiwa, nami kuna kipindi nilichoka kusikia Nyerere akisifiwa kila atajwapo na hapo alishastaafu. Fikra ya kumfanya mtakatifu, naamini ni matokeo huko kusifiwa!

Wakati ni rahisi kusema hupendi kusifiwa (kama vile kusema ‘nisiitwe mtukufu’), changamoto halisi ni kutenda kama kiongozi asiyependa kusifiwa. Waswahili wanasema: Zilongwa mbali, zitendwa mbali.

Kiongozi asiyependa kusifiwa. atatengeneza mazingira ya kutambuliwa michango ya kipekee ya watu mbalimbali katika safu zake za uongozi, lakini ukiona watu wanazungumza zidumu fikra za huyo mtu mmoja, na ni yeye peke yake anachomoza, ujue kuna tatizo. Ingekuwa kweli hakupenda kusifiwa, Nyerere angelikataa wadhifa wa baba wa taifa, ambao utahitaji hoja nzito kunishawishi kuwa anastahili.

Kwa upande mwingine, nadhani sifa ‘zilizopitiliza’ kwa Samia ziangaliwe katika muktadha wa siasa za ushindani. Kimsingi kinachifanyika ni kuanza kumjenga kiongozi ambaye CCM wanajua baadae wataenda kumuuza majukwaani, na hakuna ubaya katika hilo.

Ulimwengu ameonesha wasiwasi mkubwa kuwa hao viongozi watakuwa hawamwelezi ukweli bosi wao kutokana na tabia yao hiyo ya kusifusifu. Mimi husikia mawaziri na viongozi wengine wakiapa kuwa watamshauri rais kwa hekima na uaminifu, lakini nadhani huu ushauri, hasa kama umekaa kiukosoaji, si lazima uwe hadharani kama ilivyo kwa siasa za sifa. Na kama wasaidizi hao wanashauri kinafiki, basi kuna tatizo kubwa, labda kama tuna rais ambaye ana uwezo usio wa kawaida wa kujua kila kitu kiachotokea kila mahali.

Jambo muhimu zaidi lililonivutia kuchangia kwenye maoni ya Ulimwengu ni hoja yake kuhusu teuzi nyingi anazozifanya rais na namna zinavyokuwa kikwazo katika kusukuma maendeleo kwa sababu hawajui watu wenyewe. Yeye, Ulimwengu, kwa kuwa kwake serikalini miaka ya nyuma anajua zaidi kuliko mimi, lakini nashangaa anapofikiria kwamba rais kujuana binafsi na hao anaowateua ni muhimu!

Nahitaji kuelimishwa zaidi, lakini mimi nilidhani urais ni taasisi yenye idara na watumishi wengi ambao humsaidia rais kutenda kazi zake, na kwa hivyo si lazima rais amjue kila mteuliwa wake.

Kimsingi, nakubaliana na fikra kwamba rais amepewa watu wengi wa kuwateua, na pengine ingekuwa bora madaraka yangetawanya ikiwemo kwa wananchi kuchagua viongozi wao. Lakini, hoja ya Ulimwengu inapingana na hili kwa sababu ‘mtu’ mmoja afanye hiyo kazi.

Mi nadhani ukiacha umuhimu wa katiba mpya katika kubadili mifumo, kinachohitajika ni kuweka taratibu nzuri zaidi za kutafuta hao wenye sifa na kutoka maeneo maalumu yalizoainishwa kwa ajili ya kufikiriwa kuteuliwa kupitia mamlaka zilizopo zinazopaswa kumsaidia rais.

Najua rais anateua kada kadhaa za kitaaluma, akitegemea vyombo maalumu vya kiushauri. Kama haiku hivyo, kwa kada hizi za wakuu wa mikoa, makataibu tawala, wakuu wa wilaya, maafisa tawala na hata wakurugenzi, taratibu za namna hiyo ziwekwe pia ili isiwe mambo ya kila mtu kupeleka mtu wake.

Vinginevyo, rais kutowajua binafsi wateule wake, sidhani kama ni hoja yenye nguvu na mashiko, na wala siamini hilo linakwamisha mrejesho kupitia ripoti mbalimbali na hivyo wala halizuii ufanisi.
 
Anateua na kutengua atakavyo! Tena baada ya muda mfupi! Au kuhamisha apendavo bila kujali gharama, ni kw raha zake. Zamani tliskia ktu knaitwa "vetting" kabla ya kuteua, siku hizi ni mwenye kuimba mapambio vzr na wanachama wanashindana kutunga na kuimba. Anaishia kuteua ambao analazmika kuwatengua baada ya mda mfupi nk...!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom