Rais Samia anasifiwa kupita kiasi

Rais Samia anasifiwa kupita kiasi

Niwakumbushe kitu tu kwamba chimbuko la praise team.

Sote tuliohai tunatambua kwamba siku zote serikali inawajibika kwa raia wake na inaeleweka vyema kupitia chama tawala kwa awamu ya kwanza hadi ya 3 serikali ilikuwa imara ila ilipofika awamu ya 4 mambo yalibadilika kwa namna flani ikawa viongozi wamefocus zaidi kwenye matumbo yao kuliko mahitaji ya raia ikafikia stage kila mdau ni mpiga dili au dalali wa kuuza rasilimali zetu kwa wageni kujilimbikizia utajiri tu. Haki za wanyonge kuporwa na wenye mali zikakithiri. Kiufupi taswira ya chama ikachafuka sana na hakuna mtu alikuwa anataka kuisikia CCM so ilibidi waje na masterplan mpya.

Katika kikili kakara ndio akapitakana Magufuli maana ndie angalau alikuwa na haiba ya kukubalika na raia. Kwa kua watu walikuwa na chuki sana na chama ndipo Magu akaamua kujiposition yeye kama yeye ili kuleta relevance kwa chama. Ndio mfumo wa praise team ulianzia hapo. Lengo lilikuwa kuleta relevance ya uongozi wa CCM ili raia nyongo ziwapungue maana walikuwa washaichoka mno na ilibaki nukta tu waipe chadema nchi.

Magu alikubalika na kuirudisha CCM kwenye chart baada ya kuamua kutawala kinyume na awamu ya 4 kabisa kutokana na mfumo wake wa ku favour wananchi zaidi kuliko wanasiasa na matajiri. So wengi walimsifia sana na alikuwa akijinadi yeye kama kiongozi mkuu wa serikali.
Kusifia sahivi imekuwa ni lazima
 
Tuna manafiki tele hii nchi jitu linaomba Hela yakula nduguze maskini LAKINI linakwambia mama anaupigia mwingi! Mama huyo anawaambia wateule wake akiwemo mkwewe wale lkn wasivimbiwe...
Serikali haipongezwi anapongezwa mtu yaani umeme ukikatika waziri na tanesco wanatukanwa LAKINI umeme ukiwepo anapongezwa rais binafsi kuwa anaupigia mwingi!!!
Nchi ikikosa elimu Bora ni majanga matupu
Yale majangili yanaiba ndiyo yanaanza kusifu
 
Kila siku utasikia,"Rais kajenga barabara hapa:Rais katujengea zahanati."
Watu wanamwabudu Rais,na yeye hafanyi kitu chochote kuwazuia. Haya ndiyo mambo yanayomchukiza Mungu.

Kwa ajili Uchaguzi Mkuu unakaribia,acha watu wanisifie zaidi na zaidi.

Magufuli hakuwa anasifiwa namna hii; ingawa watu walikuwa wanasema huyu mtu kaongoza nchi siku kidogo tu,lakini nchi yetu imepata maendeleo kama Ulaya.

Marekani utasikia mara moja moja wanasema,"The Biden Education Programme,au The Biden Housing Project,lakini hii ni kwa sababu Kuna strong Opposition Party,na wanataka kutofautisha mambo.

Kikwete mara moja tu walikuwa wanaongea kuhusu " mamilioni ya Kikwete". Lakini kila siku tunasikia kuhusu " mamilioni ya Samia".

Hata ukimpa mtoto mdogo peremende,lazima uhakikishe kwamba yule mtoto anamsifu Mungu.

Kwa hiyo wajihadhari hawa watu wote wanaotaka kuitwa "superstar"
Acha upotoshaji wa kijinga, mauasisi wa hizi sifa za kikuda kwa rais ni Magufuli. Kwa Sasa chawa wa mama nao wanafuata nyendo za enzi za propaganda za kipindi Cha Magufuli.
 
Niwakumbushe kitu tu kwamba chimbuko la praise team.

Sote tuliohai tunatambua kwamba siku zote serikali inawajibika kwa raia wake na inaeleweka vyema kupitia chama tawala kwa awamu ya kwanza hadi ya 3 serikali ilikuwa imara ila ilipofika awamu ya 4 mambo yalibadilika kwa namna flani ikawa viongozi wamefocus zaidi kwenye matumbo yao kuliko mahitaji ya raia ikafikia stage kila mdau ni mpiga dili au dalali wa kuuza rasilimali zetu kwa wageni kujilimbikizia utajiri tu. Haki za wanyonge kuporwa na wenye mali zikakithiri. Kiufupi taswira ya chama ikachafuka sana na hakuna mtu alikuwa anataka kuisikia CCM so ilibidi waje na masterplan mpya.

Katika kikili kakara ndio akapitakana Magufuli maana ndie angalau alikuwa na haiba ya kukubalika na raia. Kwa kua watu walikuwa na chuki sana na chama ndipo Magu akaamua kujiposition yeye kama yeye ili kuleta relevance kwa chama. Ndio mfumo wa praise team ulianzia hapo. Lengo lilikuwa kuleta relevance ya uongozi wa CCM ili raia nyongo ziwapungue maana walikuwa washaichoka mno na ilibaki nukta tu waipe chadema nchi.

Magu alikubalika na kuirudisha CCM kwenye chart baada ya kuamua kutawala kinyume na awamu ya 4 kabisa kutokana na mfumo wake wa ku favour wananchi zaidi kuliko wanasiasa na matajiri. So wengi walimsifia sana na alikuwa akijinadi yeye kama kiongozi mkuu wa serikali.
Sipingani na maelezo yako, ila hapo kuwa magu aliirudisha ccm kwenye chart imebidi nicheke sana. Aliirudisha kwenye chart, au alitumia madaraka Yale vibaya kuhakikisha ccm tu ndio inafanya siasa? Kama aliirudisha ccm kwenye chart, kipi kilimfanya anajisi chaguzi?
 
sio inajihusisha na ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama vile ya afya, elimu, maji na mengineyo,
bali pia inawajengea uwezo na mazingira bora zaidi makundi mbalimbali mathalani wafanyibiashara, wakulima, wavuvi n.k ili wafanye shughuli zao si tu kwa ufanisi zaidi bali pia kwa uhakika na ubora tajika....

watu wa miujiza ni nyinyi mnao jipa matumaini na kujifarij kila uchwao eti mnaweze take over dhidi ya utawala uliopo 😀

my friend,
hakuna muujiza...
unayoyona ya kawaida ndio mipango yenyewe hiyo....

si hua mnashangaa hata wanachama wa ccm kugalagala kwa mahaba ya chama chao, viongozi waandamizi kula kwa mama nitilie, au kupiga magoti ni ushamba au maigizo😀

mipango ya ushindi huanzia mbali nyie mkiwa mnapiga myayo tu na maandamano uchwara....
Wasigalegale chini tu, watembee hata uchi, Ili mradi tume iwe huru, kisha uje ulete mrejesho. Sio mnaleta danganya toto, kisha nyuma ya pazia mnalazimisha mtangazwe washindi kwa shuruti.
 
Mkuu;

Kwenye hoja yako umechanganya mambo mengi ambayo kiuhalisia sivyo yalivyo.

Ukisoma katikati ya mistari ya hoja hii, unaona mtoa hoja anaakisi uhalisia wa hisia na tabia ya watanzania wengi wenye uelewa mdogo wa siasa, walio shiba ujamaa uchwara, wenye chuki dhidi ya matajiri na wenye kufurahia maumivu ya wengine!

Magufuli alikuwa muumini kindakindaki wa kundi hili, alikuwa ni miongoni mwa kundi hili, alikuwa yeye ndiye habari, na habari ndio yeye! Yaani alipenda sifa! Alipenda asifiwe hasa!

Mwendazake alibana vyombo vya habari mpaka mazungumzo ya kawaida ya watu vijiweni. Kuna vyombo vingi vya hahari vilifungiwa.

Huyu max Melo wa JF hii ni shahidi na kuna watu wengi vijiweni walifunguliwa mashtaka na kufungwa jela kwa kumkosoa Mwendazake tu!

Kipindi cha Jakaya na cha sasa cha Samia, vyombo vya habari vipo huru na watu wapo huru.

Mtoa hoja nashindwa kutofautisha sifa zinazotolewa watu walio huru na sifa zinazotolewa na watu waliokandamizwa!
Maelezo yako ni sahihi kabisa kwa 100%. Ukitazama vizuri Magufuli aliimua kucheza na hisia za masikini, ndio maana akawa anakomoa matajiri wasiomsujudia. Na alihakikisha anatumia madaraka yake kumuumiza yoyote asiyemsujidia, wakati huo huo akawa anataka atangazwe kwa mazuri tu, tena mengi yakiwa ya data za uongo zaidi.

Nakumbuka Kuna wakati alikuwa anatengeneza propaganda za wazi kabisa kuonyesha kuwa makampuni kadhaa ya umma yanapata faida Hadi yakawa yanatoa gawio. Watu wengi walikuwa wanajua ule ni uongo, lakini akawa anamwagiwa sifa za wazi kwa uongo huo! Kibaya zaidi waliokuwa wanamwaga sifa hizo za uongo ni wasomi!
 
Ukiona hivyo jua uwezo shida.Na wajanja wanatembea na chaki ili wajipigie vya kutosha.
 
Wasigalegale chini tu, watembee hata uchi, Ili mradi tume iwe huru, kisha uje ulete mrejesho. Sio mnaleta danganya toto, kisha nyuma ya pazia mnalazimisha mtangazwe washindi kwa shuruti.
baki ukishanaga na kulalamikia wenye mipango na nia ya kishika dola na kuunda serikali, ukadhani malalamiko na porojo zako sijua za kuporwa uchaguzi, sijui nyuma ya pazia kuna nini, ukadhani eti kuna anae weza kukuzingatia wakati wa harakat na mapambano ya kushika dola....

kwa shuruti ama kwa shirati, mipango ya ccm kushika dola iko pale pale kwa uzito na maandalizi mazito vile vile....

porojo na stori zako za maandalizi ya kushindwa uchaguzi, kila siku baki nazo na chama chako...

Rais comrade Dr.SSH atasifiwa sana tu bila mbambamba yoyote kitaifa na kimataifa kwa kazi zake njema na nzuri sana kwa maslahi mapana ya waTanzania wote.....

na nyinyi kamsifieni kibaraka wenu kule, si yupo
 
Hana uwezo wa kusifiwa kimataifa, labda nyie chawa ndio mtamsifia, ili awatengeneezee ñjia yenu ya kuelekea chooni.
 
inafahamika bayana mnaumia sana moyoni na kibaraka wenu......

na kusIfiwa huko kwa Rais Comrade Dr.SSH ni trela tu, picha lenyewe bado halijaanza...
 
Tunaumia au tunawadharau kwa sifa za kipuuzi?
 
Mimi nadhani hizi sifa anazosifiwa ni nje tu ila yao hazipo
 
Kila siku utasikia,"Rais kajenga barabara hapa:Rais katujengea zahanati."
Watu wanamwabudu Rais,na yeye hafanyi kitu chochote kuwazuia. Haya ndiyo mambo yanayomchukiza Mungu.

Kwa ajili Uchaguzi Mkuu unakaribia,acha watu wanisifie zaidi na zaidi.

Magufuli hakuwa anasifiwa namna hii; ingawa watu walikuwa wanasema huyu mtu kaongoza nchi siku kidogo tu,lakini nchi yetu imepata maendeleo kama Ulaya.
Subiri akishuka ngazi watakavyomnanga
 
Tunaumia au tunawadharau kwa sifa za kipuuzi?
dharau ni jambo zuri, la muhumu na la maana sana kwa mtu asie na dira wala uelekeo na ndio hua chimbuko la mihemko, ghadhabu na unyumbu wake baada ya kuangukia poa kwa kila kitu mwisho wa siku, kwasababu anakua anakua na liburi na amepotoka....

sie hatunaga dharau, mzaha, wala haya, kwa mtu au chama chochote tunapokua tunapotafuta tunacho hitaji kwa maslahi mapana ya waTanzania wote....

Rais Comrade Dr.SSH ndie kiongozi anaependwa zaidi barani Africa kwa sasa...
 
Maelezo yako ni sahihi kabisa kwa 100%. Ukitazama vizuri Magufuli aliimua kucheza na hisia za masikini, ndio maana akawa anakomoa matajiri wasiomsujudia. Na alihakikisha anatumia madaraka yake kumuumiza yoyote asiyemsujidia, wakati huo huo akawa anataka atangazwe kwa mazuri tu, tena mengi yakiwa ya data za uongo zaidi.

Nakumbuka Kuna wakati alikuwa anatengeneza propaganda za wazi kabisa kuonyesha kuwa makampuni kadhaa ya umma yanapata faida Hadi yakawa yanatoa gawio. Watu wengi walikuwa wanajua ule ni uongo, lakini akawa anamwagiwa sifa za wazi kwa uongo huo! Kibaya zaidi waliokuwa wanamwaga sifa hizo za uongo ni wasomi!
🤝
 
Kila siku utasikia,"Rais kajenga barabara hapa:Rais katujengea zahanati."
Watu wanamwabudu Rais,na yeye hafanyi kitu chochote kuwazuia. Haya ndiyo mambo yanayomchukiza Mungu.

Kwa ajili Uchaguzi Mkuu unakaribia,acha watu wanisifie zaidi na zaidi.

Magufuli hakuwa anasifiwa namna hii; ingawa watu walikuwa wanasema huyu mtu kaongoza nchi siku kidogo tu,lakini nchi yetu imepata maendeleo kama Ulaya.

Marekani utasikia mara moja moja wanasema,"The Biden Education Programme,au The Biden Housing Project,lakini hii ni kwa sababu Kuna strong Opposition Party,na wanataka kutofautisha mambo.

Kikwete mara moja tu walikuwa wanaongea kuhusu " mamilioni ya Kikwete". Lakini kila siku tunasikia kuhusu " mamilioni ya Samia".

Hata ukimpa mtoto mdogo peremende,lazima uhakikishe kwamba yule mtoto anamsifu Mungu.

Kwa hiyo wajihadhari hawa watu wote wanaotaka kuitwa "superstar"

Ngoma ikilia sana huwa ina tabia mbaya ya kupasuka...na ukiona moshi, jua kuna moto
 
Haifanyiki kwa bahati mbaya ni mkakati maalum wa wale wanaofaidika na utawala wake
 
Back
Top Bottom