Niwakumbushe kitu tu kwamba chimbuko la praise team.
Sote tuliohai tunatambua kwamba siku zote serikali inawajibika kwa raia wake na inaeleweka vyema kupitia chama tawala kwa awamu ya kwanza hadi ya 3 serikali ilikuwa imara ila ilipofika awamu ya 4 mambo yalibadilika kwa namna flani ikawa viongozi wamefocus zaidi kwenye matumbo yao kuliko mahitaji ya raia ikafikia stage kila mdau ni mpiga dili au dalali wa kuuza rasilimali zetu kwa wageni kujilimbikizia utajiri tu. Haki za wanyonge kuporwa na wenye mali zikakithiri. Kiufupi taswira ya chama ikachafuka sana na hakuna mtu alikuwa anataka kuisikia CCM so ilibidi waje na masterplan mpya.
Katika kikili kakara ndio akapitakana Magufuli maana ndie angalau alikuwa na haiba ya kukubalika na raia. Kwa kua watu walikuwa na chuki sana na chama ndipo Magu akaamua kujiposition yeye kama yeye ili kuleta relevance kwa chama. Ndio mfumo wa praise team ulianzia hapo. Lengo lilikuwa kuleta relevance ya uongozi wa CCM ili raia nyongo ziwapungue maana walikuwa washaichoka mno na ilibaki nukta tu waipe chadema nchi.
Magu alikubalika na kuirudisha CCM kwenye chart baada ya kuamua kutawala kinyume na awamu ya 4 kabisa kutokana na mfumo wake wa ku favour wananchi zaidi kuliko wanasiasa na matajiri. So wengi walimsifia sana na alikuwa akijinadi yeye kama kiongozi mkuu wa serikali.
Mkuu, kumbu kumbu zako zipo 'hot' sana, pamoja na ufafanuzi uliouweka ni sahihi 100% .
Na kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 nembo ya mgombea wa Ccm, haikuwa na jina la chama bali ilikuwa na picha ya mwenge, Magufuli pamoja na M kubwa kumaanisha Magufuli, siyo Ccm.
Baada ya kuwa Rais, aliendelea kutawala kama Rais aliyetokana na mgombea binafsi, akiitaja Ccm kwa nadra sana, nadhani kiubinadamu aliona haya kuitaja na kuinadi Ccm ya mafisadi, hadi pale kwenye mkutano wa marais wastaafu, Mkapa alipoikaripia kanuni hiyo ya kutawala anayoifuata Magufuli ya kujitaja yeye badala ya chama, lakini kanuni hiyo tayari ilikuwa imekwisha kutamalaki.
Baada ya hapo ndipo Magufuli akaanza kuiweka Ccm mdomoni mwake, ingawa vitendo vyake havikuendana kabisa na viongozi na makada wa Ccm watangulizi wake tunaowajua sisi.
Ni kweli kabisa kuwa huu 'msamiati' mpya wa ...'Rais kafanya, Rais kajenga, Rais katoa mabilioni'... ulianzia kwake.
Sasa, kwa walamba viatu kauli hizi zimefika mahali pake maana zinafupisha na kurahisisha maneno ya kujikomba.
Je ni kweli pamoja na sifa za usomi walizonazo Mawaziri pamoja na Wabunge wote, hawana uelewa wa lugha sahihi ya kuelezea uwajibikaji wa Serikali katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo hadi wammwagie sifa Rais kama anatoa fedha zake za binafsi mfukoni mwake?
Tena hawataji 'title' ya Rais tu, ni lazima wamtaje kwa title pamoja na majina yake yote matatu kanakwamba yupo mTz asiye elewa jina la Rais!