Rais Samia anaendelea kuwalambisha asali

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Sifa ya asali ni utamu, Ila katika Serikali ya Rais Samia Suluhu ni faida wanazopata wananchi kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita. Katika moja ya hotuba zake Rais Samia alisema moja ya mipango ya Serikali ni kuendelea kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii wa tiba kwa Afrika.

Katika safari hiyo tumeona wahudumu wa sekta ya afya wakijitahidi kufanya mambo makubwa ikiwemo upasuaji uliofanyika karibuni wa kutenganisha watoto waliungana Neema na Rehema, MOI kuja na teknolojia mpya ya kutengeneza mikono kwa teknolojia ya umeme ambayo haikuwepo Tanzania lakini pia Tanzania kuwa nchi ya tano kwa uzalishaji wa mionzi dawa Afrika.

Serikali ya Rais Samia ina mchango mkubwa katika safari hii, Kwa sasa wanafunzi watakafaulu kupewa ufadhili wa 100% katika masomo, Serikali inaboresha hospitali zote za Rufaa katika mikoa yote, Serikali kusogeza huduma za kibingwa mpaka kwenye ngazi za mikoa.
 
Uchawa ni sifa ya watu wapumbavu. Kulamba asali kwa gharama za maisha kupanda mara dufu ?!! Hivi waTanzania wamelogwa na popo bawa gani, uchawa mwingiii ni kusifia sifia tu, au kulamba asali kwa kuiuza Ngorongoro kwa waarabu na kula urefu wa kamba ?! Brainless UVCCM.
 
Nchi ya walaaniwa uzao wa mazuzu. Uchawa ni sifa ya watu wapumbavu. Kulamba asali kwa gharama za maisha kupanda mara dufu ?!! Hivi waTanzania wamelogwa na popo bawa gani, uchawa mwingiii ni kusifia sifia tu, au kulamba asali kwa kuiuza Ngorongoro kwa waarabu na kula urefu wa kamba ?! Brainless UVCCM.
 
Back
Top Bottom