GE2025 Rais Samia amuondolea hadhi ya Ubalozi Ndg Humphrey Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.

Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
Hata hainogi kabisa. Kizimkazi naona kachemka kweli kweli. Unatenguaje mtu Ubalozi na kumwachisha utumishi wa umma mtu aliyejiudhuru kwa hiari yake. Naona lengo ni kumnyima haki zake za kiutumishi.

Amtengue basi na wanachama wa chama cha mambuzi.
 
Chura Kiziwi na genge lake, wametafuta mahali au mlango tu wa kutoke from their mess...

Lakini bahati mbaya hata huo walioupata wakidhani umewatoa nje, wamejikuta wametokea kwenye ua uliozungushiwa ngome ya ukuta wa Yeriko....!

Utenguzi wa tarehe 16/7/2025 ndo unautangaza baada ya karibu mwezi mzima kupita..!!!???

Ndiyo maana tunasema huyu Chura Kiziwi na genge lake la utekaji na mauaji hafai kukalia kiti cha u - Rais hata kwa sekunde moja tu ijayo...!
Kwani haujui mkuu kuwa serikali hukata kona kama Meli? Hizo ni procedure za kiserikali (ziko hivyo ili kuondoa dhana ya one man show).. hata sioni sababu ya kumuattack samia katika hili. Ilifahamika baada ya HP kufanya vile hadhi yake ya ubalozi ingeondoshwa na hatakiwa wa kwanza wala wa mwisho.
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.

Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
Hii haiwezi kuwa breaking news hata kwa sekunde. Ilitarajiwa mapema kabisa toka ile barua iliposambaa.
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.

Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
Samia bwaana!
Screenshot_20250729-090555~2.png
 
Hata hainogi kabisa. Kizimkazi naona kachemka kweli kweli. Unatenguaje mtu Ubalozi na kumwachisha utumishi wa umma mtu aliyejiudhuru kwa hiari yake. Naona lengo ni kumnyima haki zake za kiutumishi.

Amtengue basi na wanachama wa chama cha mambuzi.
Bila shaka Polepole alikuwa anajua ni nini kinatokea. Na wengi tunajua kuwa kinachofuata ni kufukuzwa uanachama wa CCM.
 
Nadhani unachanganya kati ya mtu kuwa balozi na mtu kuwa balozi. Hadhi ya balozi haitoi sifa nyingi kati ya hizo ulizoandika.
Uko sahihi kabisa. Jamaa anachanga wakati mtu anapokuwa balozi wa nchi fulani na baada ya kumaliza muda wake na kubaki kama mstaafu.
 
Back
Top Bottom