GE2025 Rais Samia amuondolea hadhi ya Ubalozi Ndg Humphrey Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.

Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
So inasaidia nini, ni mwendawazimu tu ambae asingejua hili kutokea , nafikiri watz wengi walijua na Pole pole alilijua hilo, so what ,ilihali hata fundi viatu anaishi bila cheo chochote na maisha yanaenda, vyeo ni kidunia tu.
 
Katengua au kakubali barua yake?
HP si alishajiuzulu na akawapa makavu yao!!?
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.

Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
Hatuna Rais!
 
Huo ni ujinga au ulimbukeni? Unawezaje kumfuta kazi mtu ambaye tayari ameacha kazi?
 
Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.
Walisoma kweli barua ya Polepole? Si alishajiuzulu?!
 
Back
Top Bottom