GE2025 Rais Samia amuondolea hadhi ya Ubalozi Ndg Humphrey Polepole

GE2025 Rais Samia amuondolea hadhi ya Ubalozi Ndg Humphrey Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dk Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.

Aidha, Rais Samia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya utumishi wa umma amemuachisha kazi Polepole kwa manufaa ya umma.

Kwa mujibu wa barua hiyo, uamuzi huo umeanza tangu Julai 16, 2025.
Tulitegemeee hili ni swala la mdaa tuuu.

Na walaa halina madhara maana Ndugu yetu alishasepaa

Na udhubitisho kwamba hapendi wakosoaji wake. Naa hii ni uthibitishoo
 
Maybe diplomatic passport? Kupita na diplomatic bags airport ambazo hazikaguliwi? Immunity from prosecution nchi unayoenda? Preferential treatment kwenye huduma zote za serikali za ndani na nje I guess
Si hadi uwe na akili ya biashara sasa kama hauna mishe au upo nje ya mfumo wa kula Kodi za wananchi utaitumia wapi hio passport
 
Back
Top Bottom