Rais Samia amewatuma Mabalozi wakaulize wenzetu wamefanya uchawi gani kukua haraka kiuchumi

“Mtuambie wenzetu wamefanya uchawi gani kukua kiuchumi,na sisi tunakosa nini, tuna rasilimali hatuzitumii? au kitu gani, ila niseme ni wazi wenzetu wamepiga hatua kubwa sana licha ya kuwa sisi tumewazidi kwenye rasilimali diplomasia ya uchumi ifanye kazi hapa, tujiulize tuliachwa wapi?” - Rais SuluhuSamiaView attachment 2718932

Haiwezekani tuna kiongozi mkubwa wa nchi bado anaamini masuala ya giza katika kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi , it look like hana a,b, c yoyote ili nchi ipate maendeleo ya kiuchumi ifanye nini ?

Hivi hili ni taifa la namna gani mtu yoyote asiwe na uelewa na masuala ya nchi kupiga hatua anapewa nafasi kubwa ya kuwa kiongozi wa nchi katika dira ya maendeleo.

Nikisema kuwa hili taifa linaongozwa na kipofu wa masuala ya maendeleo na uongozi nitakuwa nakosea jamani ?

Kwamba Rais hafahamu kuwa ili China, Russia, Qatar, U.S.A, Germany, Singapore, Malaysia, Korea, Japan n.k walifanya nini ili kupata maendeleo yao ya kiuchumi ?

Kwa kumsaidia nampa hawa watu wawe walimu kwake, ni nini kifanyike ili taifa lipate maendeleo makubwa ya uchumi na aache kuwatupia mzigo mabalozi ambao hata yeye akiaamua kuwa serious anaweza kujifunza nini kutoka kwa hawa viongozi mazuri yao economically na kutuvusha hapa tulipo:-
Francisco Franco
Park Chung Hee
Chiang kai shek
Deng Xiaoping
Urho Kekkonen
Mahathir Mohamad
Muammar Gaddafi
Lee Kuan Yew
Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum
Alishasema alifeli mtihani wa kidato cha nne
 
Samahani mwandishi nadhani utakuwa ni miongoni mwa watu wenye akili ndogo sana hapa duniani kama kauli ndogo kama hii ya Mh.Rais umeshindwa kuitafsiri.
Kweli kabisa ,neno uchawi ni maarafu sana mitaani hata katika maongezi ya kawaida ikimaanisha maajabu au njia ya mkato sometimes mfano mtu anaweza kuwaambia wanafunzi "hakuna uchawi soma ufaulu"na mifano ipo mingi kama vile ; "mchawi pesa"

Kwenye uzi huu mtoa hajaonyeshwa kiwango kidogo cha akili peke yake bali pamoja na chili zisizo za msingi.

"Kuchukiana na watu kusipelekee kukosa uadilifu" (Quoted from Qur'an)
 
Mojawapo ya sifa kuu ya nchi zilizopiga maendeleo ni vita vikali dhidi ya rushwa na ufisadi. Yaani hawacheki na fisadi. Ukifisadika aisee ama unafungwa maisha au unauliwa tu maana hakuna namna. Na pesa yote uliyoiba lazima utairudisha wewe na ukoo wenu wote ikiwezekana. Hii ndiyo siri yao kuu mojawapo.

Halafu wana viongozi wazalendo, wenye maono na wasiotetereka. Ili kuendelea unahitaji viongozi ambao wanapigania legacy na siyo matumbo yao. Kiongozi yupo tayari asitajirike lakini anawaza miaka 200 ijayo wananchi wa Thailand watanikumbukaje; na siyo kuwaza utajiri wa familia yangu utakuwaje.

Nenda Thailand leo. Nenda Singapore. Nenda Malaysia. Wote hawa tulipata nao uhuru karibia miaka sawa lakini wako mbali mno. Wanajitambua. Wanajithamini. Wanasonga mbele.

Sisi bila kukomesha/kupunguza rushwa na ufisadi kamwe hatutakaa tuendelee. Bila viongozi wazalendo hatutakaa tuendelee. Bila watu wetu kuwa na mvuvumko wa kifikra na kimaendeleo mambo hayatabadilika.

View attachment 2718967

Tunakomeshaje ufisadi? Tunapataje viongozi wazalendo? Ukipitia bandiko hili hapa chini bila shaka angalau utapata mahali pa kuanzia. Siyo kazi rahisi, ni ya muda mrefu, inakatisha tamaa lakini inabidi tuifanye kama kweli tunataka siku moja tuweze kuendelea.

Tumekupata kikolo,chana!
 
Kipo clear kuwa yeye mpaka sasa hafahamu ili kupata maendeleo ya kiuchumi nini kifanyike ? Na anafikiri kuwa ni mazingaombwe China, Korea, U.S.A, Japan kuwa pale zilipo ? Si atoke sasa ikulu awaachie wanaojua ?
Wewe unahisi raisi katumia neno uchawi akimaanisha mazingaombe? Hapa unakatisha tamaa kabisa
 
“Mtuambie wenzetu wamefanya uchawi gani kukua kiuchumi, na sisi tunakosa nini, tuna rasilimali hatuzitumii? au kitu gani, ila niseme ni wazi wenzetu wamepiga hatua kubwa sana licha ya kuwa sisi tumewazidi kwenye rasilimali diplomasia ya uchumi ifanye kazi hapa, tujiulize tuliachwa wapi?” - Rais SuluhuSamia

View attachment 2718932

Haiwezekani tuna kiongozi mkubwa wa nchi bado anaamini masuala ya giza katika kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi , it look like hana a,b, c yoyote ili nchi ipate maendeleo ya kiuchumi ifanye nini ?

Hivi hili ni taifa la namna gani mtu yoyote asiwe na uelewa na masuala ya nchi kupiga hatua anapewa nafasi kubwa ya kuwa kiongozi wa nchi katika dira ya maendeleo.

Nikisema kuwa hili taifa linaongozwa na kipofu wa masuala ya maendeleo na uongozi nitakuwa nakosea jamani ?

Kwamba Rais hafahamu kuwa ili China, Russia, Qatar, U.S.A, Germany, Singapore, Malaysia, Korea, Japan n.k walifanya nini ili kupata maendeleo yao ya kiuchumi ?

Kwa kumsaidia nampa hawa watu wawe walimu kwake, ni nini kifanyike ili taifa lipate maendeleo makubwa ya uchumi na aache kuwatupia mzigo mabalozi ambao hata yeye akiaamua kuwa serious anaweza kujifunza nini kutoka kwa hawa viongozi mazuri yao economically na kutuvusha hapa tulipo:-
Francisco Franco
Park Chung Hee
Chiang kai shek
Deng Xiaoping
Urho Kekkonen
Mahathir Mohamad
Muammar Gaddafi
Lee Kuan Yew
Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum
Hiyo ni tafsida ya lugha, sio kama unavyotaka kumtuhumu. Angeweza nyofoa neno uchawi akaweka neno "mbinu". Simkubali Sa100 lakini sijaona kosa kwenye sentensi hii
 
Magu tulikuwanae office Moja kwanini twende mbali, wakati tunaona ndani ya miaka mitano mambo makubwa yaliyofanyika tujiulize alifanyaje.
 
Mama hajamaanisha uchawi kama matunguri lakini mbinu,Kinachoshangaza mkuu wa kaya za Tanzania hajui jinsi gani tufanye kama nchi tupate maendeleo ina maana miaka yote 61 ya uhuru chama chao hakina dira ya kukuza uchumi wa nchi hapa tumepigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je,Rais kutaja mabalozi wenye majina ya kiislam watakwenda nchi za kiarabu na hao wengine watakwenda mataifa mengine kamaanisha nini?
 
Uchawi waliotumia wenzetu nikukataa kuwa mawakala wa shetani, kila mtu analazishwa kufanya mambo kwa kiasi, kutenda haki na kutoa sadaka siyo kusubiri kupewa, Sasa sisi tupo kinyumenyume, kuwa na familia kubwa sana mpaka tunakosa kutoridhika muda wote unataka mpaka vitu visivyovyako, hatufanyi haki Yale tusiyopenda kufanyiwa sisi tunawafanyia wengine, dhuruma, chuki mpaka mtu anafikia kufanya uchawi ili mwenzie aumie, sisi kila mtu ni ombaomba haridhiki na chake Wala kuishi ndani ya bajeti yake na ikitokea amekopa harudishi.

Sasa viongozi wa dini wanaongoza kufundisha mafanikio ya mali na serikali nayo inapamba na mtu kumiliki mali, na kufundisha dhambi yaani watu waache dhambi wanasahau hakuna haja ya kufundisha mtu yeyote kuacha dhambi Bali wanatakiwa wafundishe kutenda haki maana haki huinua taifa na haki inainua mtu mmojamoja maana yake kila mtu akimtendea mwenzie haki basi Mungu atabariki sehemu hiyo, hata amri kumi za Mungu zipo kwenye mfumo wa kutendea haki ndo maana huoni kule wanasema usilewe, maana unaweza kulewa lakini ukawa unatenda haki, Sasa dhambi ipo kwaajili ya mtu na Mungu na dhambi inampa mtu husika na aibu yake hata maandiko yamesema hivyo, Sasa Africa ni kichaka Cha Mambo ya kishetani kila kitu kinyumenyume na haki haitendeki kwa mtu mmojamoja na hata vyombo vinavyojiita vya kutoa haki kwenye nchi vinafanya dhuruma kwa kunyima watu haki zao, Sasa hebu warudi kufundisha haki kwa wote na kuitendea kila mahali waone nchi itavyoneemeka.
 
Back
Top Bottom